Uchaguzi 2020 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam: Yaliyojiri mkutano wa kampeni wa Dkt. John Pombe Magufuli

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,792
11,953
Baada ya kupumzika kwa siku kadhaa, mgombea Urais wa JMT kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli anaendelea na kampeni leo katika mkoa wa Dar es Salaam katika uwanja wa Benjamin Mkapa.






HOTUBA YA DKT. MAGUFULI
....Gonjwa hili la Corona na kilio cha Wanakenya wakiongozwa na Rais Uhuru Kenyatta katika kuliombea taifa na kumuomba Mungu kuondoa Ugonjwa huu, napo Kenya utaondoka. Kwasababu Mungu ukimuomba hakuna kitakachoshindikana, na Mungu ni mwema siku zote. Mungu hoyeeee! Tanzania hoyeee! Kenya hoyee!

UMUHIMU WA JIJI LA DAR KWA UCHUMI WA TAIFA
Ndugu zangu wana Dar es Salaam, jiji la Dar es Salaam ni muhmu sana hapa nchini. Ni kwasababu jiji hili lina idadi kubwa ya watu kuliko miji mingine yote nchini. Takwimu zinaonesha jiji hili linakadiriwa kuwa na watu milioni 6. Na itakapofika mwaka 2030 linatarajiwa kuwa na watu wapatao milioni 10.

Hii italifanya jiji hili kuwa miongoni mwa majiji manne yenye hadhi ya “Megacity” barani Afrika. Majiji mengine ni pamoja na Lagos, Luanda pamoja na Kinshasa.

Kwahiyo jiji la Dar es Salaam ni jiji muhimu sana. Mbali na kuongoza kwa idadi, Dar es salaam ni jiji kuu la biashara hapa nchini ambalo linachangia mapato mengi ya serikali, lakini pia linatoa mchango mkubwa kwenye pato la taifa.

Takwimu zinaonesha kuwa kwa tarkribani miaka mitano iliyopita Dar es Salaam imekuwa ikiongoza kwa uchangiaji mapato ya serikali, hususani mapato ya kodi.

Takriban 90 % ya kodi yanatoka Dar es Salaam. Nataka nitoe takwimu.

Mwaka 2015/16, mapato ya Dar es Salaam yalikuwa Tshs. Trilioni 11.9 ambayo ni asilimia 89.9

Mwaka 2016/17 ilikuwa Trilioni 12.6, asilimia 88.6

Mwaka 2017/18 ilikuwa Tshs. Trilioni 13.6 ambapo ni asilimia 89

Mwaka 2018/19 ilikuwa Tshs. Trilioni 13. 9 ambayo ni asilimia 88.7

Mwaka 2019/20 ilikuwa Tshs. Trilioni 16.01 ambayo ni asilimia 89.7

Aidha, kwa miaka mitano Dar es salaam imeendelea kuongoza katika kuchangia pato la taifa. Mwaka 2015 ilichangia Tshs Trilion 16.2 ambapo pato la Taifa lilikuwa Tshs. 94.3

Mwaka 2016 Dar es Salaam ilichangia Tshs. Trilioni 18.4 wakati pato la taifa lilikuwa trilioni 108.4

Mwaka 2017 Dar es ilichangia Tshs. 20.5, pato la taifa lilikuwa Trilioni 118.7

Mwaka 2018 Dar es Salaam Ilichangia Tshs. Trilioni 22.5, wakati pato la taifa lilikuwa Trilioni 129.04

Mwaka 2019 Dar es Salaam Ilichangia Tshs. Trilioni 23.9, wakati pato la taifa lilikuwa Trilioni 139. 9

Hii inahihirisha umuhimu wa jiji hili kwa maendeleo ya nchi yetu. Hongereni sana wana Dar es Salaam.

Ndugu zangu wana Dar es Salaam, kama hilo halitoshi, jiji hili ni lango kuu lashughuli za uchukuzi na usafirishaji. Siyo tu kwa hapa nchini, lakini pia kwa nchi nyingi zinanotuzunguka.

Kama mnavyofahamu, nchi yetu inapakana na nchi 8 na nchi 6 hazina bandari, na hivyo kutegemea Bandari ya Dar es Salaam kupitisha mizigo yao.

UTEKELEZAJI WA AHADI ZA MWAKA 2015
Ndugu zangu Wana Dar es Salaam, ni kwa kuzingatia hayo yote nilipokuja hapa Dar es Salaam kuomba kura mwaka 2015. Niliahidi mambo mengi lakini leo nitataja mambo maubwa manne ambayo niliahidi mwaka 2015.

La kwanza, niliahidi kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

Pili, niliahidi kuimarisha miundombinu ili kurahisisha usafiri wa hapa Dar es Salaam lakini pia usafiri wa kwenda mikoani pamoja na nje ya nchi.

Tatu, niliahidi kuboresha huduma za jamii ikiwemo Afya, Elimu, Maji pamoja na Umeme.

Na nne, tuliahidi pia kuboresha mazingira ya biashara kwa ajili ya Wana Dar es Salaam na kwa ajili ya Watanzania wote.

Nafarijika kuona kwamba kwenye hii miaka mitano muliyotupa tdhamana ya kuliongoza taifa, tumeweza kutekeleza ahadi hiyo kwa vitendo.

i. ULINZI NA USALAMA
Wakati tunaingia madarakani, hapa Dar es Salaam, vitendo vya ujambazi hususan vya kutumia silaha vilikuwa vimeanza kushamiri. Ilikuwa mtu ukienda benki kuchukuwa hela, unakuwa na hofu kama fedha zako utazifikisha salama maana uhakika ulikuwa mdogo kwasababu ya ujambazi. Tumefanikiwa kwa kiwango kikubwa sana kudhibiti vitendo hivyo. Sio tu hapa, bali maeneo ya Mkuranga, Rufiji na Kibiti.

Kwa kuimarika hali ya usalama, wananchi wanaendelea na shughuli zao za Maisha bila hofu.

Nawapongeza Wana Dar es Salaam lakini pia navipongeza sana vyombo vya ulinzi na usalama.

ii. MIUNDOMBINU
Mambo mengine ni kuhusu miundombinu…tumefanya mambo mengi sana.

Kwanza, tumejenga barabara za lami kwenye mitaa ya Dar es Salaam. Ukijumlisha hizo barabara zote za lami zilizojengwa na zinazojengwa, ni zaidi ya kilometa 200 ambapo tumetumia zaidi ya bilioni 660.

Ninyi Wana Dar es Salaam ni mashahidi kwamba hivi sasa mitaa mingi ya jiji hili la Dar es Salaam ina lami na nyingine zimewekewa mpaka na taa, ikiwa barabara ya njia nne kutoka Morocco hadi Mwenge inayojengwa kwa gharama ya Tshs. Bilion 74.8; barabara ya Bamaga-Shekilango, na barabara nyingine. Lakini, barabara ya njia nane ya kutoka Kimara-Kibaha inayojengwa kwa Tshs Bilioni 140, nayo inaendelea kwa kutumia fedha zetu.

Kuhusu hii barabara ya Kimara-Kibaha yupo mgombea mmoja wa Urais amesikika akisema eti tunajenga barabara pana sana. Tena anasema yeye ametembea nchi nyingi na hajawahi kuona barabara pana kama hii. Majibu yake ni kwamba si kweli kwamba hii ndiyo barabara pana kuliko zote duniani, kule “Hoston” (Houston), Marekani ipo barabara inaitwa Katty Freeway, ina njia 26.

Lakini, hata kama kwa mfano, ingekuwa barabara yetu ni pana kuliko zote duniani, mimi sioni ubaya wowote. Hakuna ubaya wa Tanzanania kuwa na kitu kikubwa kuliko chochote duniani. Siyo lazima kila kitu kizuri, kikubwa kiwe kipo Ulaya.

Mbona Mwenyezi Mungu aliamua kumuweka mtu wa Kwanza hapa Tanzania? Anashangaa kitu gani?

Mbona Mungu alitupa Mlima mrefu na mti mrefu kuliko yote barani Afrika?

Mbona Mungu aliamua kutupa Tanzanite wakati haipo mahali pengine?

Zaidi ya hapo ndugu zangu, tumekamilisha barabara ya mabasi ya mwendokasi, awamu ya kwanza. Kutoka Kivukoni hadi Kimara na kutoka Magomeni hadi Morocco, kwa gharana ya Tshs. Bilioni 403, na sasa tunaanza ujenzi wa awamu ya pili kutoka Gerezani hadi Mbagala. Nyie wenyewe ni mashahidi munaona barabara inawekewa mpaka nondo.

Lakini vilevile tumejenga daraja la juu pale Mfugale, TAZARA kwa Tshs. Bilioni 101 na daraja la Ubungo kwa Tshs. Bilioni 229.8.

Na tumekamilisha Daraja la Nyerere pale Kigamboni ambalo lilianza kujengwa kwenye awamu iliyopita. Na sasa tunaendelea na daraja la kilometa moja pamoja na barabara yake ya kilomita 7 pale Selander Bridge.

Kwa Tshs. Bilioni 270 na madaraja mengine ya juu pale Gerezani kwa Tshs Bilioni 24.8.

Kuna baadhi ya wilaya, jhasa hizi wilaya mpya za Ubungo na kigamboni tunataka kufumua barabara huko, ndiyo maana tumekuja kuwaomba kura hapa.

Kuhusu miundombinu ya usafiri, jana mumeshuhudia tumeweka jiwe la msingi la mradi mkubwa wa stendi ya kisasa wa stendi ya kimataifa pale Mbezi Louis, yenye uwezo wa kupokea mabasi 3446 kwa siku na ina eneo la kulaza mabasi 1000.

Zaidi ya hapo, kwenye miaka mitano iliyopita tumekamilisha ujenzi wa jengo la tatu la abiria JKNIA kwa gharama ya Tshs. Bilioni 722.5. Jengo hilojipya lina uwezo wa kuhudumia wasafiri milioni 6, wakati majengo mawili ya mwanzo yalihudumia wageni milioni 2 tu. Kwahiyo kwa sasa uwanja una uwezo wa kuhudumia wageni milioni 8 kwa mwaka.

Lakini ninyi ni mashahidi tumenunua ndege 11. Na katika miaka mingine mitano kama mutatupa ridhaa, tumepanga kununua ndege nyingine 5 mpya, ikiwemo ndege kubwa ya kubeba mizigo.

Zaidi ya hapo, kwenye miaka mitano iliyopita tumetumia Tshs. Bilioni 902 kufanya upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam

Uwekezaji mkubwa tulioufanya kwenye sekta ya miundombinu hapa Dar es Salaam umeleta manufaa mengi kwa mwananchi mmoja mmoja lakini pia kwa nchi yetu kwa ujumla. Mathalani, kutokana na kuimarika miyundombinu, tumeweza kupunguza tatizo la msongamano barabarani.

Kwa mfano, mtu wa Kimara alitumia mabasi ya mwendokasi. Licha ya changamoto zilizopo, anatumia dakika 45 tu kufika mjini badala ya kutumia masaa matatu hata masaa manne, suala ambalo “lilileteleza” saa nyingine hata kuharibika kwa ndoa.

Kutokana na upanuzi wa bandari, shehena za mizigo zimengezea kutoka tani milioni 13.1 mwaka 2015/16 hadi hadi tani milioni 16.1 mwaka 2019/20. Hii imeongeza mapato ya Bandari kutoka Bilioni 679.32 mwaka 2014/15 hadi Bilioni 951.02 mwaka 2019/20.

iii. HUDUMA ZA KIJAMII
Mbali na kuimarisha miundombinu ya usafiri, tumeimarisha pia huduma za jamii, hususani Afya, Elimu, Maji na Umeme.

Afya
Nikianza na Afya, kama mutakumbuka ziara yangu ya mwanzooni kabisa ya kustukiza nilenda Muhimbili. Nakumbuka siku ile niliwakuta wakina mama wajawazito na Watoto wakiwa wamelala chini na pia hapakuwepo vifaa tiba vya kutosha. Vilivyokuwepo vilikuwa vingine vibovu, vingine vimeharibika.

Nafarijika kuona katika miaka mitano iliyopita tumefanya mabadiliko makubwa, siyo tu kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili lakini kwenye taasisi zake nyingine ikiwemo Taasisi ya Mifupa ya MOI, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.

Pale Muhimbili tulipeleka vitanda 210 na magodoro 210. Ocean Road tuliongeza idadi ya vitanda kutoka 40 hadi 100.

Tumekamilisha pia jingo jipya la MOI lililogharimu Tshs bilioni 22 na Hospitali ya Mloganzila iliyogharimu Bilioni 206.7 pamoja na vifaa.

Sambamba na hilo tumepeleka vifaa tiba vya kisasa Muhimbili, MOI, JKCI pamoja na Ocean Road.

Tumetumia Bilioni 22.686 kuimarisha huduma ya aftya kwenye ngazi za Wilay, Vituo vya Afya na Zahanati. Tumejenga hospitali za wilaya 4, vituo vya afya 10 na zahanati 14.

Elimu
Tumetumia Bilioni 92.3 kuboresha elimu ya msingi na sekondari hapa Dar es Salaam, ambapo kiasi cha Bilioni 68 zimetumika kugharamia elimu bila malipo.

Tumejenga maktaba na hosteli Chuo Kikuucha Dar es Salaam pamoja na kuimarisha Taasisi ya Teknolojia.

Maji
Katika miaka 5 iliyopita, tumetekeleza miradi ya maji ipatayo 17 yenye thamani ya bilioni 583.2. Miradi hiyo imehusisha mabomba makuu, mabomba ya usambazaji, matenki na kuchimba visima virefu.

Miongoni mwa miradi iliyotekelezwa n wa Ruvu Juu, Mlandizi Kibamba hadi Kisarawe, ulioghalimu Bilioni 105.5. Mradi wa Ruvu Chini unaohusisha mradi wa tenki kubwa Chuo Kikuu uliogharimu Bilioni 131.4, na mradi wa usambazaji kutoka Mlandizi hadi Mbezi Louis na Kutoka Bagamoyo hadi Tegeta uliogharimu Bilioni 52.01.

Miradi mikubwa inayoendelea ni uchimbaji wa visima vikubwa Rufiji na Mpera, Tsh. Bilioni 18. 9, na mradi wa kutoka maji Kisarawe kwenda Pugu, G’Mboto na Ukonga, Tshs. Bilioni 7.3.

Miradi hii imafanya upatikanaji wa maji kuongezeka katika jiji la Dar es Salaam.

Umeme
Kwa upande wa umeme ndugu zangu, katika miaka mitanoiliyopita, tumetekeleza miradi mikubwa miliwili ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia – yaani Kinyerezi 1 na Kinyerezi 2 ambazo zimeongeza kwenye gridi ya taifa Megawatt 425. Zaidi yah apo, kwenye miaka 5 iliyopita, tumeunganishia umeme wateja wapya 317, 517 na hivyo kufanya wateja wa umeme katika jiji la Dar es Salaam 671, 685.

Mipango tuliyonayo miaka 5 ijayo kwa jiji la Dar es Salaam:
Tutaendelela kuhakikisha hali ya utulivu, amani na usalama vinaendelea kudumu,

Biashara na Ustawi kwenye maeneo yenye usalama, ndicho kitu muhimu katika maendeleo ya nchi yoyote.

Tutaimarisha vyombo vaya ulinzi na usalama ikiwepo kuwapatia zana za kisasa, motisha na kuboresha mazingira yao ya kazi.

Miaka mitano ijayo mutegemee maajabu makubwa zaidi katika miundombinu

Musiniletee wapinzani, watanichelewesha.
 
Ila Yohana Mbatizaji, nakukubali sana katika kukipigania chama nambari 1 duniani kote na katika hii Milkyway galaxy. :D :D :D

Inapaswa upokee buku7 Mara 70.

Everyday is Saturday :cool:
 
Hesabu hao watoto waliokimbizwa na kuhahirishiwa masomo halafu ndio uje na Utopia huu. Kama Ana nyomi Ni vipi Basi wanahaha kumfungia Lissu .

Bunge mlifunga ili watu wafanye kazi lakini mikutano ya mkuu mnaandika barua na kuhahirisha masomo, shame on you.
 
Watu wanafuata burudani tu kutoka kwa akina Ali Kiba, Diamond, Harmonize,nk Hakuna jipya.
.
Ndio wanafuata burudani Ila kumbuka CCM Wana akili Mara1000 ya vyama vilivyobaki, wanawajua Watanzania zaidi ya mnavyofikiria nyie,, ili Mtanzania akusikie na kukuelewa kwa makini lazima awe na moroli kwanza na ndo Maana CCM inaanza na burudani kwanza ili kuwandaa raia kwa ajili ya kusikiliza Sera zao.
This bongo joh!
 
Niseme tu kwa kifupi kwamba hii ni funga kazi, misururu ya watu kwa wingi huu kuelekea uwanja wa taifa mara ya mwisho niliona Simba ilipocheza na Stella abidjan ya Ivory coast kwenye fainali ya kombe la CAF....
Kwenye hiyo fainali huo uwanja ulikuwepo?
Halafu mbona unadanganya watu ambao tunaona eneo la tukio?
 
Hivi leo lugha itakayotumika ni ipi...Kiswahili cha kijiji, Kiswahili cha taifa au Kiswahili cha dunia? Mimi ningemshauri atumie Kiswahili cha Dar es Salaam tu kama itawezekana na ajiepushe kuchomekea kile cha dunia.
 
.
Ndio wanafuata burudani Ila kumbuka CCM Wana akili Mara1000 ya vyama vilivyobaki, wanawajua Watanzania zaidi ya mnavyofikiria nyie,, ili Mtanzania akusikie na kukuelewa kwa makini lazima awe na moroli kwanza na ndo Maana CCM inaanza na burudani kwanza ili kuwandaa raia kwa ajili ya kusikiliza Sera zao.
This bongo joh!
Mtu mwenye akili za kiwango hicho ulichokitaja, hawezi kushawishika kuhudhuria na pia kumchagua mgombea kwa sababu tu alimburudisha au kumpa chakula.

Wahudhuriaji wengi wa hilo tamasha watakua ni wale Watanzania wajinga tu mlio watengeneza wenyewe kwa miaka yote hii kupitia elimu duni, sera duni za kiuchumi, kisiasa na kijamii, nk.
 
Watanzania tumeshuhudia maiti za watanzania wenzetu zikiokotwa kwenye fukwe zikiwa zimefungwa mawe na vyuma na nyingine zikiwa kwenye viroba.

Watanzania, tumeshuhudia wenzetu wakitekwa na kupotezwa, wafanyabiashra wakifilisiwa,.

Tumeona ndugu na jamaa zetu wakifunguliwa makesi makubwa na yasiyo na dhamana.

Huyu mtu hatufai kabisa.
 
Back
Top Bottom