Kifo cha Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa katika jicho la tatu

Kifo cha Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa katika jicho la tatu

TumainiEl

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
7,275
Reaction score
14,315
Kifo cha Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya tatu ni moja ya vifo huenda kikazivutia idara nyingi za usalama ktk mataifa makini yanayopenda kulinda uhai wa viongozi wao wakuu wa kitaifa.

Awali ya yote niwape pole nyingi familia ya marehem Benjamin William Mkapa. Nina imani hawakujuwa na hawakutegemea kabisa kifo cha Mzee wetu. Vilevile kwa Watanzania wote nawapa pole nyingi sana.

Naomba sana mada hii isihusishwe na awaye yeyote ila kama idara nyeti za nchi wanaweza isoma na kufanya mabadiliko makubwa katika kulinda afya za viongozi na kuweka taratibu maalumu ktk kulinda afya za wakuu wa nchi basi ningeshukuru. Ni kweli hapa dunian sio kwetu tunapita ila taa ya Mkapa kuzima ni igo kubwa sana ktk siasa za Taifa la Tanzania.

Wastaafu ni hazina kubwa ktk Taifa na ulinzi wa afya za hawa majemedari walioliongoza Taifa ni muhimu sana ili tuweze vuna madini walionayo kwa maslahi mapana ya Taifa. Kifo cha huyu jemedari ni kifo cha kuhuzunisha sana na ni kifo ambacho kama tungekuwa na special unit kuangalia afya za hawa majemedari hakika asingekufa mapema.

Wengine huenda tunajiuliza what is a suddenly cardiac arrest (sca). Hii ni hali mtu moyo wake unasimama ghafla na akikosa support ya wataalam au wasipo detect mapema mgonjwa anakufa.

Kwa maelezo ya msemaji wa Familia SCA ndio iliyochukua uhai wa jemedari huyu wa majeshi yetu ktk awamu ya tatu.

Why nasema uzembe au kutokuwa makini au mazoea yamenyakua uhai wa huyu jemedari wetu wa Taifa?

Nina uhakika Rais Mstaafu alienda hospitali ambayo huenda sio mara ya kwanza kuwenda na huenda kwa aina ya Madaktari na specialists wetu sometimes wanapomuona mtu wanamhudumia kila mara huchukua kama wanajua matatizo yake na kuchukua vipimo as usual while wakimuweka special room but not under special care. Na hapa ndipo nina imani jinamizi lilipounyakuwa uhai wa jemedari wetu.

Ikiwa angekuwa under special care, while anapata huduma wangeweza detect heartbeat before yaliyomkuta. Huenda tangia alipotoka mpaka pale amefika alikuwa anaondoka kidogokidogo na wangewahi kumuweka under special care tungemponya uhai wake.

Mtu aliyekuwa kiongozi mkubwa kama huyu kumuweka mapumziko tu bila kufuatilia afya yake 24 hrs haikuwa afya kwa uhai wake. Tafadhali naomba kama chumba kilikuwa na CCTV angalieni handling yake muone kama hapakuwa na kauzembe fulani ambacho sio cha kukusudia.

Issue ya Malaria nayo ni suala lingine la kufuatilia. Hapa kuna jambo tunahitaji kuangalia, je before hajaanza dawa mwili ulikuwa na status gani katika damu?

Pendekezo

Ni lazima from now onwards kuwe na muongozo wa kiusalama pindi hawa five star wanaumwa. Ni lazima kuwe na aina ya matibabu tofauti na raia wengine; namaanisha akienda anaumwa hata jicho lazima treatment yake iwe same like ICU person yaani level of alert must be high. Nadhani wasomi mmenielewa na Mungu awabariki Sana.

Mzee Mkapa umeondoka ila najua kifo chako kinaenda kubadilisha Sura ya Tanzania ktk mambo mengi Sana. Pumzika Kwa Amani Baba yangu. Amen
 
Siku yako ikifika imefika tu.
Mzee Nyerere alikufa huko kwenye dunia ya kwanza St Thomas Hospital.

Itoshe kusema siku yako ikifika imefika hizi zingine ni Maelezo baada ya Habari.

Sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.
 
Kifo ndiyo mwisho wa safari ya mwanadamu bila kujali kafa vipi au kaugua nini.
Fundisho ni kwa sisi tunaobaki duniani.
 
Sio kwa viongozi tu, watanzania wengi sana wanakufa hospitalini kwa uzembe wa madaktari. Kuna tatizo kubwa kati ya madaktari wengi nchini.
 
Mbona unazunguuuuka...Sema tu huamini kama SCA ndio imemuua basi. Uzembe huo unaousema siamini kama upo. Mkapa ana personal professional doctor na anafanya check up regularly kwa mujibu wa status yake kitaifa, kwaiyo hakuna uzembe hapo. Labda tujiulize, alikuwa analalamika tumbo linamuuma, mara tunasikia malaria mara SCA tuanzie hapo, uzembe upo wapi?
 
Kwanza alipolazwa tu alitakiwa Daktari wake au wa serikali awe hapo chumbani kila minute. Sijui kama alikuwepo. Sote hatuelewi mengi zaidi.
Na sio tu hivyo, cha kujiuliza, hivi hapo hospitalini hata first Aid haikuwepo? Kubonyeza kifua na ku-revive moyo kwa kusukuma mara 35 tu pia ilishindikana? Machine ya defibrillator nayo ilikuwepo, haikuwepo, ilitumiwa au ilikosekana? Ni mambo ya kujiuliza, labda alipewa hiyo first aid, sijui. Cardiac arrest dawa yake ni hiyo tu chest compression na baada ya moyo kuanza kupiga ndo mambo mengine hufuata.
 
Damu ya wapemba ilisaidia cardiac arest!!!Angalau tutapumua watz mwenye chama wameondoka !wamebaki chotara waswahili wenzetu wawili na mrundi mmoja!!Huyu mrundi hatuwezi!!!
 
Maswali ni mengi kuliko majibu tuelezwe kwa nini sababu inatolewa leo ? Je ni hospital ipi? Haki yetu kupata majibu haraka sana
 
Back
Top Bottom