Benjamin Mkapa: Watanzania mtanikumbuka

Benjamin Mkapa: Watanzania mtanikumbuka

kuna mdau kanishangaza! Anasema Kikwete ni mzalendo aliyeamua kuleta mapinduzi ya fikra kwa style hii!! Ameniambia Kikwete hatumjui vizuri!! Atatushangaza!
 
Ndiyo, tutamkumbuka kwa jinsi alivyofisadi nchi yetu na kuwawezesha mafisadi wenzake kuendeleza libeneke. Ni Mkapa huyu huyu aliyekuwa akiapa kila kukicha kuwa "over my dead body," kuhusu Kikwete kuukwaa urais. Sasa atueleze ilikuwakuwaje?
mimi namkubuka zaidi kw tangold,meremete,kiwila,deep green,ni rais wa kwanza kutumia ikulu kufanya biashara,kifupi ni kuwa alibaka imani aliyopewa na mwl ni fisadi la kutupwa
 
mimi namkubuka zaidi kw tangold,meremete,kiwila,deep green,ni rais wa kwanza kutumia ikulu kufanya biashara,kifupi ni kuwa alibaka imani aliyopewa na mwl ni fisadi la kutupwa


na mgomo wa madaktari
 
Ben alikuwa anaweza kuzungumza kitu kwa kumaanisha na alikuwa anaweza kutoa maamuzi kama yeye,
M.kwere hafanyi maamuzi hadi ajue watachekelea? hapo atajitahidi hata kwa kupiga fix.
 
Miaka kumi yake ya uongozi ilisaidia kujenga ndoa yake kuliko nchi, alichokifanya ni kuliachia taifa leiende kwenye auto pilot. the plane going to hit mount kilimanjaro and then new country will rebirth....yeah! no more nyang'au.
 
Fisadi mkubwa uyo Jamaa, tena bora ata bana rz ..tatizo mnakurupuka tuu na kumsifia wakati yeye ndie alieuza nchi. Na Bado makubwa zaidi yatatokea tz...
 
Hizi siasa za kunadiwa hazina maana. Mwinyi alipoondoka madaraka alisema MTANIKUMBUKA haya sasa nasikia tena Mkapa pia alisema MTANIKUMBUKA, hivi kwani hawa wote sii viongozi wa CCM iweje waseme mtamkumbuka wakati walikuwa wakitekeleza sera za chama?.. au mtanikumbuka ina maana wanashndana baina yao wenyewe!
- Na kweli tunawakumbuka kwa hasara walizotuachia..
 
Ukiwa unasota ni kawaida kuona "ya leo kali, ya jana ina afadhali". I bet rais atakayekuja anaweza kuwakumbusha watu Kikwete, kwani hata Mkapa naye watu walimsema sana na "kumkumbuka" Mwinyi.

Mimi namkumbuka kwa kukubali Range Rover 5.0 kutoka kwa Andy Chande huku akijidai Mr. Clean wa "Ukweli na uwazi" aliyekataa zawadi za waswahili na hata kumwambia Kitwana Kondo - alipotaka kujipendekeza na vijizawadi vya pongezi- ampongeze kwa kuchapisha tangazo kwenye gazeti.

It's a long fall from Mr. Clean aliyeunda Tume ya Rushwa to Mr. Bean aliyejikwapulia Kiwira.

Pia namkumbuka kwa kunywa Johnny Walker mpaka akalala kitandani Sea View (akiwa Foreign Affairs Minister) huku rais Mwinyi akiwa anamsubiri Uwanja wa Ndege Dar kinyume na itifaki.

Of course aliweza pia kudhibiti mfumuko wa bei, kuanza kukusanya kodi kwa uhakika, kuweka idara ya usalama wa taifa kisheria kuwatukana Waingereza CHOG Australia juu ya Mugabe mpaka Blair akampa shavu, na mengine kama hayo.

Nilienda Kampala nikakutana na Waganda wanasema "bora enzi za Idi Amin"!! Sikuamini.

Kwa hiyo, the grass is always greener on the other side. Kikwete mchovu, lakini hii haibadili rekodi ya Mkapa.
 
mkapa ni miongoni mwa marais walioiharubu nchi hii kwa sana, alikuwa mbabe mno. kama ubabe ni sifa basi anastahiki

mengi ya machungu tunayoyapata msingi wake ni Ben, msikumbuke maji ziwa victoria tu. kumbukeni na mengine
 
Hatatokea rais bora kama Mkapa Tanzania. Tutamkumbuka daima.
 
umesahau project ya bodi ya mkopo aliisimamisha msingi vasco da gama akaja kujizolea sifa na sasa anaiua taratibu
 
yaani jamani twende mbele turudi nyuma hata kama mzee upara ana mabaya yake alofanya lakini ana mengi aliyofanya ambayo yanatufanya tumkumbuke tofauti na huyu swahiba anayejua kulipa visasi kwa wote waliopita njia zake baada ya kufikikiria afan yaje aiondoe nchi kwenye criss tuliyonayo
 
JK ndo ajue kuwa urais sio kuchekacheka na kutwa kutumiana sms na wanywa kahawa wenzie na mademu
 
Heshima wakuu! Nianze kwa kutoa maelezo. Unapofanya analysis ukitaka usionekane upo biassed unatakiwa ujadili pande zote za jambo ni kama kwenye kuianalyse kampuni kwa SWOT(Strength, Weakness, Opportunity na Threats) kwahiyo tukija kwenye mada hapo juu kuanalyze uongozi wa nchi ni vema tukajadili mazuri, mabaya, impact ya mazuri na impact ya mabaya ili kuweza kuja na majumuisho yenye manufaa.
 
FOR sure President Benjamin Mkapa wa an intelligent person, more focused, pragmatic and with clear vision.During his leadership the national economy prospered, he controled economic shocks such as inflation.And above all, President Mkapa maintained a highest level of discpline within his party.Nowadays things are falling apart in every aspect of life, poor eduation quality, skyrocketing commodity prices, rampant corruption and indiscipline within the state machinery.Kwa kweli tuna kila sababu ya kumkumbuka Mkapa.
Its true that under BMW the economy stabilized. However he was the architect of the corruption we are seeing today. Talk of EPA, KAGODA, KIWIRA, MEREMETA, DEEP GREEN FINANCE, RADAR, TANGOLD, CIS and stupid mining contracts. We are now suffering for what he left behind. Sure for that he will be remembered.
 
Baada ya vyombo vya habari vilivyokuwa vimenunuliwa na genge la mtandao kumsakama sana kwa habari nyingi za kumponda. Mkapa aliwahi sema maneno machache sana kuwa Watanzania tutamkumbuka.

Kwa kweli hali ya nchi iliyopo saizi hakika jamaa tutamkumbuka tu, tutake tusitake. Nchi kila kitu kinaenda hovyo, na wanaonufaika ni wachache waliokuwa vinara wa hilo genge. Hakika sipati picha itakapofika 2014 hali itakuwaje. Saizi hela haina thamani kabisa, naamini soon BOT itaprint note zingine za elfu 20 na elfu 50. Ki ukweli buku 10 haina thamani tena. Ukishachenji imeisha.

Nchi huwa haiongozwi kwa blabla bali inahitaji commitment ya hali ya juu sana.

Kila la kheri.....
hivi jamani watanzania tumelogwa? Mkapa akumbukwe kwa lipi? hakuna cha Mkapa wala Kikwete wote ni mafisadi tu, alikua anafanya biashara ikulu, au tumkumbuke jinsi alivyojiuzia mgodi wetu wa kiwira? au Anben? aende zake huko hakuna atakaemkumbuka chadema tukiingia madarakani wote tutawashughulikia.
 
Ni mkapa yule mchezaji wa yanga au yule rais na sumaye waziri mkuu aliyewauzia kila kitu wazungu na yeyekujiuzia mgodi kama ni huyo mnaye mkumbuka kweli tanzania hakunaga.
 
Back
Top Bottom