Benjamin Mkapa: Watanzania mtanikumbuka

Benjamin Mkapa: Watanzania mtanikumbuka

Mganga/kigagula wa ccm aliwatapeli kuwa Mkweree ndio chaguo la watz! Inawezekana na nao walimdhurumu akageuza ungo!!!
 
Mwaka 1995 Kikwete aliposhinda raundi ya kwanza Nyerere alisema 'bado mdogo' wakati umri wa kikwete wakati huo ni mkubwa kuliko umri wa Nyerere wakati anaukwaa urais 1961. Watu hawakumwelewa Nyerere kuwa alimaanisha Kikwete hawezi urais kistaarabu. Leo ndo tunajua ukweli kile alichokimaanisha Nyerere kuwa ni Kikwete hawezi kuwa Rais tatizo halikuwa umri.
 
Udogo wa ubongo,kufikiri na kufanya maamuzi....si umri
 
silence is the best noise one can make...........mkapa ni kiongozi shupavu sana.......sio kama huyu mwizi, mtoto mwizi na sasa amemfundisha mkewe wizi ( rejea ile hundi feki)
 
Mwanzoni kabisa mwa utawala wa Kikwete (nasita kuweka neno Rais), vyombo vya habari vilimuandama sana kuandika kila kukicha maovu aliyoyafanya ikiwemo kashfa ya Kiwila, kila kukicha utasikia hili na lile kuhusiana na udhaifu wa utawala wa wake, ninaamini mengi yaliyokuwa yakisemwa dhidi yake yalikuwa ya kweli kwasababu hakuwahi kushtaki kwamba anasingiziwa na kushushiwa heshma yake bure, sana sana nakumbuka alisema "Watanzania mtanikumbuka" mmoja wa watu waliokasirishwa na kauli yake hiyo nilikuwa ni mimi maana sikuona tutamkumbuka kwa lipi? kumbe huyu mtu anaona mbali sana yeye binafsi utawala wake ulikuwa una madhaifu mengi tuu lakini aliweza kutabiri kwamba kipindi cha Kikwete hali itakuwa mbaya zaidi yatajitokeza mambo ambayo lazima tutamkumbuka hata kwa udhaifu wake, hebu fikiria yafuatayo katika utawala wa Mkapa.

1. Kasi ya Mfumuko wa bei ilikuwaje? Na spidi ya kuanguka kwa shiringi dhidi ya fedha za kigeni ilikuwaje?
2. Kasi ya ukuaji wa uchumi ilikuwaje?
3. Ni mara ngapi uongozi wake ulikwenda kukopa katika mabenki ya biashara ili kughalamia shughuli za kawaida za serikali kutokana na serikali kutokuwa na pesa?
4. Wakati gani serikali yake iliagiza kila wizara au mkoa ikate bajeti ya matumizi yake kwa zaidi ya 30% kutokana na kukosa uwezo?
5. Deni la Taifa lilikuwaje?
6. Kasi ya ongezeko la mapato ya serikali ilikuwaje? (hivi karibuni TRA wameshindwa kufikia lengo kwa zaidi ya 10?)
7. Ni mara ngapi wananchi walijitokeza hadharani kupinga ugumu wa maisha?
8. Ni miradi mingapi mikubwa ya maendeleo ilianzishwa katika kipindi chake?
9. Kiwango cha ubabaishaji katika uteuzi kilikuwaje rejea "turnover" ya mawaziri.
10. Katika sector ya michezo mkapa hakuwa karibu sana kama kikwete, lakini mkapa alijenga uwanja wa soka na baadaye Kikwete akamleta maximo na kula chakula cha jioni na timu ya taifa mara kadhaa.
11. Ni kiasi ganii neno udini lilitamkwa hadharani aidha na yeye mwenyewe kama kiongozi wa nchi au wananchi.
12. Mara ngapi alijitokeza hadharani kulumbana kisiasa kwa minajiri ya kujisafisha?

Haya ni machache yanayonifanya nimkumbuke Mkapa nikilinganisha na yanayojitokeza ktka utawala Kikwete na yamenifanya niamini kwamba huyu mtu ni mnajimu alijuaje kwamba nitamkumbuka?

wote yale yale tu...

si ni mkapa huyuhuyu juzi aliita wapinzani wa tanzania ni kokoto?
 
Si kweli kuwa jmk kajenga UDOM bali ni mkapa yule yule. sisi ni wamoja wa consultants wa college hiyo na mchakato ulianza mapema takribani 1yr before kumaliza kipindi cha Ben. tuliambiwa kuwa huo ni mradi wa kisiasa utakaosaidia mgombea wa chama cha magamba kupita kirahisi. Ben alikamilisha mipango yote ya sources za fedha toka mashirika ya umma na leo ****** anawadanganya kuwa ni yeye kafanya? Sehemu kubwa ya chuo imejengwa yeye akiwa madarakani lakini plani na fedha kaandaa Ben kama ilivyo kwa miradi mingi ya barabara aliyoiacha Ben imeendelea kujengwa yeye akiwa madarakani. Kubalini tu kuwa mlichagua raisi ambaye umri wake katika ngazi hiyo alikuwa bado mtoto au vinginevyo kama ni karata mmelamba g.l.sa
 
mie simkumbuki mtu hapa wote ni wamoja labda nitamkumbuka shekhe Yahya kuhusu utabiri wake kuwa amemuweka JMK pamoja na Kardinali Penngo aliyesema ni chaguo la Mungu, jamani mbona Mungu anasingiziwa hivi, kweli afisadi hawa wote wanamjua Mungu? angalia leo Mkate wa Sh 400 umepaa Mpaka 900sh, Petroli sh.2300 kutoka tsh 1020 alafu eti atauza unga kilo sh 400 kwa kutumia usafiri upi kutoka sehemu ya panapozalisha nafaka, kwa kuwa Germany wamegundua MKOJO labda tutatumia huo kuweka kwenye Matrector tutekeleze Kauli MBIU ya Kilimo Kuanza sio kwanza
 
kwa Afrika/Tanzania ni bora tuwe na kiongozi 'mwizi',lakini akawa analeta maendeleo kwa wananchi,akawa na misimamo,siyo muoga na anaweza kufanya maamuzi magumu kwa maslahi ya Taifa kuliko kuwa na kiongozi 'asiyeiba',lakini hana vision,muogamuoga,hawezi kufanya maamuzi...
Ndiyo maana bado naamini Lowasa anaweza kuwa Rais mzuri kuliko marais wote waliowahi kuiongoza Tanzania
 
Hii post imenifanya nitoe chozi....kweli kabisa Mkapa tunamkumbuka, zaidi nakumbuka utabiri wa baadhi ya ndugu zangu waliosema kuwa huyu ****** si kitu, wengi wakabisha ingawa mimi kwangu sikouna tofauti bythen........kweli tunaangamizwa.
 
silence is the best noise one can make...........mkapa ni kiongozi shupavu sana.......sio kama huyu mwizi, mtoto mwizi na sasa amemfundisha mkewe wizi ( rejea ile hundi feki)

Mkewe hivi karibuni alikuwa Amerika akitembeza bakuli la NGO yake ya WAMA; inaelekea wamarekani walimstukia kuwa hizo pesa wangezitia kibindoni na ndio maana hawakufanikiwa kupata misaada mingi kama walivyotarajia!
 
mkapa alijua kwa akili finyu za watanzania watampa kilaza uraisi
 
silence is the best noise one can make...........mkapa ni kiongozi shupavu sana.......sio kama huyu mwizi, mtoto mwizi na sasa amemfundisha mkewe wizi ( rejea ile hundi feki)
Unaonaje tuanzishe kampeni ya kumrudisha Mkapa?
 
mwanzoni kabisa mwa utawala wa kikwete (nasita kuweka neno rais), vyombo vya habari vilimuandama sana kuandika kila kukicha maovu aliyoyafanya ikiwemo kashfa ya kiwila, kila kukicha utasikia hili na lile kuhusiana na udhaifu wa utawala wa wake, ninaamini mengi yaliyokuwa yakisemwa dhidi yake yalikuwa ya kweli kwasababu hakuwahi kushtaki kwamba anasingiziwa na kushushiwa heshma yake bure, sana sana nakumbuka alisema "watanzania mtanikumbuka"[/b] mmoja wa watu waliokasirishwa na kauli yake hiyo nilikuwa ni mimi maana sikuona tutamkumbuka kwa lipi? Kumbe huyu mtu anaona mbali sana yeye binafsi utawala wake ulikuwa una madhaifu mengi tuu lakini aliweza kutabiri kwamba kipindi cha kikwete hali itakuwa mbaya zaidi yatajitokeza mambo ambayo lazima tutamkumbuka hata kwa udhaifu wake, hebu fikiria yafuatayo katika utawala wa mkapa.

1. Kasi ya mfumuko wa bei ilikuwaje? Na spidi ya kuanguka kwa shiringi dhidi ya fedha za kigeni ilikuwaje?
2. Kasi ya ukuaji wa uchumi ilikuwaje?
3. Ni mara ngapi uongozi wake ulikwenda kukopa katika mabenki ya biashara ili kughalamia shughuli za kawaida za serikali kutokana na serikali kutokuwa na pesa?
4. Wakati gani serikali yake iliagiza kila wizara au mkoa ikate bajeti ya matumizi yake kwa zaidi ya 30% kutokana na kukosa uwezo?
5. Deni la taifa lilikuwaje?
6. Kasi ya ongezeko la mapato ya serikali ilikuwaje? (hivi karibuni tra wameshindwa kufikia lengo kwa zaidi ya 10?)
7. Ni mara ngapi wananchi walijitokeza hadharani kupinga ugumu wa maisha?
8. Ni miradi mingapi mikubwa ya maendeleo ilianzishwa katika kipindi chake?
9. Kiwango cha ubabaishaji katika uteuzi kilikuwaje rejea "turnover" ya mawaziri.
10. Katika sector ya michezo mkapa hakuwa karibu sana kama kikwete, lakini mkapa alijenga uwanja wa soka na baadaye kikwete akamleta maximo na kula chakula cha jioni na timu ya taifa mara kadhaa.
11. Ni kiasi ganii neno udini lilitamkwa hadharani aidha na yeye mwenyewe kama kiongozi wa nchi au wananchi.
12. Mara ngapi alijitokeza hadharani kulumbana kisiasa kwa minajiri ya kujisafisha?

Haya ni machache yanayonifanya nimkumbuke mkapa nikilinganisha na yanayojitokeza ktka utawala kikwete na yamenifanya niamini kwamba huyu mtu ni mnajimu alijuaje kwamba nitamkumbuka?

hii kauli mimi pia niliona ya kizushi ni juzi tu niliwaambia watu warejee kauli ya bro. Ben ''watanzania mtanikumbuka" kila mtu akashika shavu..hakika alijuwa deveva tuliye mpata ana leseni za kuwasha majenereta na kuendesha bodaboda za wajawito hii ya kuendesha magari ya abiria class c hana..ndiyo maana kila kukicha wana mvisha magamba ya udockta//pole zetu
 
Mkapa alikuwa Rais wa vitendo Kikwete ni Rais wa maneno hajawahi hata siku moja kutekeleza kauli zake mfano MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA leo hata hakumbuki kama aliwahi kusema kwa kifupi ni mbabaishaji.
 
Mwaka 1995 Kikwete aliposhinda raundi ya kwanza Nyerere alisema 'bado mdogo' wakati umri wa kikwete wakati huo ni mkubwa kuliko umri wa Nyerere wakati anaukwaa urais 1961. Watu hawakumwelewa Nyerere kuwa alimaanisha Kikwete hawezi urais kistaarabu. Leo ndo tunajua ukweli kile alichokimaanisha Nyerere kuwa ni Kikwete hawezi kuwa Rais tatizo halikuwa umri.

Habari Kaka Mikel, nakufahamui vizuri sana na nimefurahi kuona picha yako na jina lako kamili hapa jukwaani, inaonyesha ni kiasi gani unajiamini, pia nimefurahi kuona tena uko CDM, this is gopod news too....back to the topic, Ni kweli ****** hawezi kuongoza nchi, sidhani kama ameshwahi kuwa hata monitor darasani, na kama alishawahi kufanya hivyo basi ni wazi alikuwa anawakoroga walimu na wanafunzi
 
Back
Top Bottom