AdvocateFi
JF-Expert Member
- Jan 15, 2012
- 11,492
- 5,050
Adha ya vijana kutumika kuchafua watu ndio hii?
Umewahi msikia Ben saanane kwenye mkutano wowote?au M4C yoyote ya kichama?
Unamisikiaga hapa kwenye usaliti,mara TISS n.k hii ndio kazi ya Ben saanane pale chadema.......
Naomba msaada yeyote aniwekee ule uzi uliomuibua Ben saanane na usaliti wake kule india kwa watanzania wenzetu na kukimbia na hela........
Mkuu changia mada. Mimi sio CCM ila nina kadi niliyoitunza kwa kumbu kumbu kama anavyofanya slaa........
Hivi huko CHADEMA hakuna mtu uwezo wa kuwakanya hawa "vijana" waache haya malumbano kwenye hii mitandao?.......
Hicho ndiyo chama makini kimejaa vijana wasomi kutoka chuo kikuu........
Lakini ninyi hapa mna mu attack Ben kwa kusema tu kwamba amesema uongo? Hamjajibu hoja zake.Mwenzenu yuko tayari kwenda kwenye vikao vya chama.Ninyi mnakimbia kivuli chake na leo mmetumwa na Zitto kuja huku kwa kasi kumtetea.Ben has evidence,nilitegemea kama una busara kama makamu m/kiti BAVICHA.Ungeenda kupeleka suala hili kwenye Chama.Swali,Kwa nini ulikua kwenye kikundi hicho,na mission yenu ilikuwa nini?........
Muulize Ben saanane walionana wapi na zitto(eneo) waliongelea nini??
Mamuya amesewa walipo onana na zitto,Je ben walionana wapi?
Akikujibu hili swla njoo hapa nikupe zwadi.Ben ni mnafiki na mwongo wa kimataifa
Nyani Ngabu: Waliotakiwa kuwakanya wamewagawa katika makundi, kuna vijana wanaothaminiwa michango yao na vijana wengine hawana thamani yeyote mbele ya watu hao. Kama Dr. Mkumbo aliingilia kati yakashindikana unategemea nini. Mimi nadhani watu kama nyinyi( wewe, Mzee mwanakijiji etc) wasio na upande labda mkiitwa mnaweza mkatatua mgogoro huu.
those who tried to bring us together also brought this poverty and corruption we witness today, may be these have different vision of splitting us into 'manageable groups' hence see if we can move forward. For sure Africa has got a lot to do!I don' t know why
I keep believing
That one day, they' ll bring us together
When they' ve shown
In more ways than one
That all they care about is the TSHS.
KWAHERI CHADEMA CHAMA KINA WENYEWE HIKI.
hizo ni akili za abunuasi, kwani kipindi mnaanzisha kile kikundi chenu cha MP7 zitto alikuwa tayari ameshatangaza nia ya urais?
Jibuni hoja za kijana Ben acheni uingiza watu wasiohusika kwani mliyafanya gizani sasa mchana kweupe yamewekwa.
TULIANZA NA MUNGU NA TUTAMALIZA NA MUNGU.
Mnazidi kuonyesha mko kundi gani. Wazee wenu wako wapi nyie, mnavuana nguo mbele za watu.
R.I.P CHADEMA tulikupenda lakini ndio hivyo tena.
kama ben anasema amerudi kundini baada yakuwa muasi basi anatumia uwongo ule ule aliokuwa anautumia wakujirekodi yeye mwenyewe mipango na mikakati yake na kisha kuwapelekea wahusika kwamba ni mipango ya masalia kuvuruga chama.that is nonsense
Mtiririko wa hizi story nauita Chapters za Kitabu kiitwacho "Kuibuka na Kuzama kwa Upinzani wa ndani ya Chadema"
Najisikia fahari sana kuona kuwa pamoja na upinzani wote huu wa ndani ya chama, Mwenyekiti Mbowe na Katibu Dr Slaa wamesimama kidete bila kutetereka, nastareheshwa na namna waumini makundi haya ya upinzani wa ndani wanavyofunguka wenyewe bila kulazimishwa wala kushurutishwa. Naamini kauli mbiu ya kimapambano inayoongoza harakati za Taasisi ya Chadema "Peoples Power" kuwa ni kauli iliyoasisiwa na Mungu Mwenyewe, maana endapo ingeasisiwa na fikra za kibinadamu hakika isingeweza kukabiliana na upinzani huu.
Kwa mujibu wa historia, jambo lolote jema hupata upinzani wa ndani. Kabla ya TANU palikuwapo vyama vingine kama AA. TAA nk, lakini watu walijitenga navyo na kusonga mbele. Wapinzani wa ndani ya chadema nao wanafuata mkondo ule ule wa historia ili maandiko yatimie kuwa HAKUNA wa kuidanganya historia, wala hakuna wa kujidanganya mwenyewe na katu hakuna wa kumdanganya shetani hata wanafiki wanaotajwa na Quarani.
Chadema_Peoples Power_God's Voice
Long live chadema
Kama Ben anaevidence(ujumbe wa kurekodi aliotumwa aufanye) si apeleke mbele ya chama.Hapo ndipo utakapo sikia nani ni mnafiki.|
Jana nasikia makamu mwenyekiti taifa ametupa kadi ya chama chini.Anatajka kuidhuru,chadema kipo tena????
Siasa za kukimbilia majukwaani na kujitafutia sifa binafsi kwa viongozi vimewafikisha hapa CHADEMA,ombwe la uongozi linahitajika kuokoa jahazi lisizame.Nyani Ngabu: Waliotakiwa kuwakanya wamewagawa katika makundi, kuna vijana wanaothaminiwa michango yao na vijana wengine hawana thamani yeyote mbele ya watu hao. Kama Dr. Mkumbo aliingilia kati yakashindikana unategemea nini. Mimi nadhani watu kama nyinyi( wewe, Mzee mwanakijiji etc) wasio na upande labda mkiitwa mnaweza mkatatua mgogoro huu.
Mlikuwa wapi siku zote hizo msiyaseme hayo hadi msubiri Ben aje kuwaumbua hapa? na baada ya siku mbili ndio mnajipanga kuja kumchafua badala ya kujibu hoja zake?
Hivi mnajua hiki mnacho kifanya sasa nia hatari zaidi kwa upande wenu kuliko Ben? Ben ameonekana hapa kuwa smart zaidi yenu na hata hivi viroja mnavyo kuja navyo sasa inathibitisha uwezo wenu mdogo mlionao...