nimesoma nyuzi zote kuanzia ila ya Mamuya, ya Zitto, ya Ben na hii ya Mchange jambo ambalo nimegundua si kweli kwamba Ben Saanane na Zitto hawajawahi kuonana kama Zitto alivyojaribu kutuaminisha
Mchange kakurupuka sana kujibu mapigo kwa Ben jambo ambalo limefanya kutojibu hoja badala yake ameanza kurusha makombora hovyo
Ben alidokeza kuhusu Zitto kumpigia simu Kitila baada ya kuona ule uzi wa Mamuya na kumwambia Kitila azungumze na Ben ili aje akanushe habari zilizoletwa na Mamuya, baada ya Kitila kumwambia Ben na Ben kukataa ndipo Zitto akaja huku kutuonyesha umahiri wake kwenye mambo ya tunguri. Bado kuna wakuamini kwamba Zitto ajawahi kukutana na Ben????