Mtiririko wa hizi story nauita Chapters za Kitabu kiitwacho "Kuibuka na Kuzama kwa Upinzani wa ndani ya Chadema"
Najisikia fahari sana kuona kuwa pamoja na upinzani wote huu wa ndani ya chama, Mwenyekiti Mbowe na Katibu Dr Slaa wamesimama kidete bila kutetereka, nastareheshwa na namna waumini makundi haya ya upinzani wa ndani wanavyofunguka wenyewe bila kulazimishwa wala kushurutishwa. Naamini kauli mbiu ya kimapambano inayoongoza harakati za Taasisi ya Chadema "Peoples Power" kuwa ni kauli iliyoasisiwa na Mungu Mwenyewe, maana endapo ingeasisiwa na fikra za kibinadamu hakika isingeweza kukabiliana na upinzani huu.
Kwa mujibu wa historia, jambo lolote jema hupata upinzani wa ndani. Kabla ya TANU palikuwapo vyama vingine kama AA. TAA nk, lakini watu walijitenga navyo na kusonga mbele. Wapinzani wa ndani ya chadema nao wanafuata mkondo ule ule wa historia ili maandiko yatimie kuwa HAKUNA wa kuidanganya historia, wala hakuna wa kujidanganya mwenyewe na katu hakuna wa kumdanganya shetani hata wanafiki wanaotajwa na Quarani.
Chadema_Peoples Power_God's Voice
Long live chadema