Ben Saanane anavyoteseka na kivuli cha unafiki...

Ben Saanane anavyoteseka na kivuli cha unafiki...

Ben Saanane muda wako wa kuonekana unafiki wako umefika, nilisema jana kwamba wewe ni mnafiki na msaliti namba moja. Shaaaaaaaaaaaame!!!!! Kijana wa aina yako kutumika kama Condom.
 
Swali la msingi....je Zitto amedanganya JF kuwa hamjui Ben?? Maelezo yanaelekea kuonyesha kumchafua ZZK zaidi na si Chama.
BEN YUPO KAZINI taarifa zinadai kuwa ametumwa na mpinani mkuu wa zitto kwenye mbio za urais 2015.
 
Aibu ipo kwa wale akina TUNTEMEKE"Tuliomba Mungu huyu Tuntemeke afe,oh Mungu ni mwema
hatimaye Tuntemeke amekufa watu sasa wamejiunga kwa real Id.

hakika Mungu ni mwema na hatimaye leo wameamua kuja na their real names.
 
nimesoma nyuzi zote kuanzia ila ya Mamuya, ya Zitto, ya Ben na hii ya Mchange jambo ambalo nimegundua si kweli kwamba Ben Saanane na Zitto hawajawahi kuonana kama Zitto alivyojaribu kutuaminisha

Mchange kakurupuka sana kujibu mapigo kwa Ben jambo ambalo limefanya kutojibu hoja badala yake ameanza kurusha makombora hovyo

Ben alidokeza kuhusu Zitto kumpigia simu Kitila baada ya kuona ule uzi wa Mamuya na kumwambia Kitila azungumze na Ben ili aje akanushe habari zilizoletwa na Mamuya, baada ya Kitila kumwambia Ben na Ben kukataa ndipo Zitto akaja huku kutuonyesha umahiri wake kwenye mambo ya tunguri. Bado kuna wakuamini kwamba Zitto ajawahi kukutana na Ben????
 
Asante sana kamanda Mchange kwakuleta huu ufafanuzi, maana haya uliyoyaandika ndiyo nilkiyotaka kuyatolea ufafanuzi japo bado nitatoa ufafanuzi wangu kuhusu hizi shutuma ambazo kwangu mimi nachokiona ni sawa na mtu kuchimba shimo halafu akatumbukia yeye mwenyewe.

Suala la Ben kutumiwa kimkakati katika harakati zakumchafua zitto na sisi ambao wao hutuita masalia wala halijaanza leo, huu ni mkakati unaoratibiwa dhidi ya Zitto pamoja na vijana ambao wanamuunga mkono Zitto, nazidi kusisitiza kwamba Ben Saanane anatumia uongo kuuaminisha umma kwamba anamfahamu Zitto kitu ambacho hata nafsi yake nina hakika inamsuta.

Ben acha kukimbia kivuli chako, sio rahisi kumchafua Zitto kama unavyoweza kudhani, japo mnajitahidi sana lakini hamtofanikiwa.

Palipo ukweli, uwongo hujitenga .

Hahaha na wewe umekurupuka kudadadeki mtajitokeza wote mamluki wa chama.
 
BEN YUPO KAZINI taarifa zinadai kuwa ametumwa na mpinani mkuu wa zitto kwenye mbio za urais 2015.

hizo ni akili za abunuasi, kwani kipindi mnaanzisha kile kikundi chenu cha MP7 zitto alikuwa tayari ameshatangaza nia ya urais?
Jibuni hoja za kijana Ben acheni uingiza watu wasiohusika kwani mliyafanya gizani sasa mchana kweupe yamewekwa.

TULIANZA NA MUNGU NA TUTAMALIZA NA MUNGU.
 
Mnakivua nguo chama hadharan nyie wadogo, yan mnaanika mambo yenu hiv?mnawarahisishia kaz magamba kuwamaliza


Nakuunga mkono sana kwani huu ujinga wanaofanya ni sawa na mume na mke watoke katikati ya mtaa waanze kugombana na kuelezana yaliyotokea wakiwa chumbani. Ni Mental immaturity kubwa sana inayoonyeshwa hapa na imeniudhi mno kwani CCM wanakusanya silaha za bwerere za kutosha huku wakichekelea jinsi watakavyowamamliza.

Ongeeni kwenye vikao vya nidhamu vya ndani ya Chama acheni utoto...............!!!! mmeboa
 
Kwa hiyo wewe ulitaka juliana akae kimya?kwani hajatajwa hapa.Julina hana watu wa kumwambia kinachoendelea hapa jf?
Ben saanane aseme ni wapi alikutana na ZItto kama mAMUYA ALIVYOSEMA kuwa walikutana ARusha.
Ujue ben saanane ni mwongo kiasi gani.

Siasa ni mchezo mchafu!!!! yaani umekuja na ID hii kwajili ya kumchafua Ben na kujitahidi kusafisha kundi lenu la PM7 ? JF ni zaidi ya uijuavyo ndugu.... Endeleeni kazi yenu tunawafutilia tararibu hatuna haraka na nyie
 
Wewe bint ndiyo umeharibu kila kitu na kudhihirisha kuwa Mchange ni muongo. Mchange anatuambia kuwa yeye ndiye aligundua na kuja kuwaambieni kuwa Ben Saanane huwa anawa record, wewe unatuambia kuwa Zitto alikuwa ana jirecord mwenyewe.
Je unamaanisha kuwa Mchange anataka kujipa sifa juu ya jambo ambalo si la kweli?
soma vizuri bwana ulicho kikopi...mbona mimi sioni sehemu juliana alipomtaja zitto kuwa amejirekodi?..

quote_icon.png
By Juliana Shonza

kama ben anasema amerudi kundini baada yakuwa muasi basi anatumia uwongo ule ule aliokuwa anautumia wakujirekodi yeye mwenyewe mipango na mikakati yake na kisha kuwapelekea wahusika kwamba ni mipango ya masalia kuvuruga chama.that is nonsense....

hicho ndicho alichokisema juliana, mbona tunakimbilia kujadili vitu bila hata kuvisoma sawa sawa.
 
Binafsi namshukuru Mungu Yehova (Muumba wa mbingu na nchi) kwa hiki kinachotokea leo. Leo tumejionea wazi wazi kile kilichokuwa kimefichika. Naomba wote (wakiwemo wanaojadiliwa hapa) tutafakari yafuatayo:


  1. Hakuna anaepinga kuwa kuliundwa kundi la kuchafua viongozi wa CHADEMA (na kuwachonganisha Mh Mbowe na Dr Slaa) intended beneficiary akiwa ni Mh Zito Kabwe.
  2. Kumekuwa na threads nyingi tu humu za kuwachafua viongozi wa CHADEMA na kudai kuwa Mh Zito anaandamwa/anachukiwa ndani ya Chama. Hata viongozi wa ccm na wapenzi wake wamekuwa wanashadidia "kuchukiwa" kwa Mh Zito (japo nikiri awali nilichukulia kuwa ni sehemu ya "singo" ya "ukanda, udini na ukabila" wa CHADEMA -rejeeni kauli ya mukama wakati wa msiba wa Mzee Bob Makani)
  3. Hakujawa na kauli kutoka kwa Mh Zito kukanusha kuwa yeye anaandamwa (nitafurahi kuonyeshwa ushahidi ili kuthibitisha kuwa nilichosema hapa si sahihi). Rejeeni posts za TUNTEMEKE.
  4. Ben Saa Nane kakiri na KUTUBU kuhusika (na watajwa hawapingi) kuhusika na mkakati wa kuwachafua viongozi wa wakuu CHADEMA.

So what do these four issues tell us? Mh Zito, you need to own up this sad state of affairs. You may actually be innocent, but your (including of those who have been doing their best - which has so far achieved to reinforce the negative perspective on your part) deeds and words hardly help your cause. Simama hadharani, own up and let us move forward.

Mchange, Taswira, Juliana et al; Ben (au inawezekana ni mjumbe mwingine) katuambia ana ushahidi na anakusudia KUUTOA KWENYE VIKAO VYA CHAMA, so why can't you guys wait and nail him there if you are so sure of what you are telling us here?????
 
nimesoma nyuzi zote kuanzia ila ya Mamuya, ya Zitto, ya Ben na hii ya Mchange jambo ambalo nimegundua si kweli kwamba Ben Saanane na Zitto hawajawahi kuonana kama Zitto alivyojaribu kutuaminisha

Mchange kakurupuka sana kujibu mapigo kwa Ben jambo ambalo limefanya kutojibu hoja badala yake ameanza kurusha makombora hovyo

Ben alidokeza kuhusu Zitto kumpigia simu Kitila baada ya kuona ule uzi wa Mamuya na kumwambia Kitila azungumze na Ben ili aje akanushe habari zilizoletwa na Mamuya, baada ya Kitila kumwambia Ben na Ben kukataa ndipo Zitto akaja huku kutuonyesha umahiri wake kwenye mambo ya tunguri. Bado kuna wakuamini kwamba Zitto ajawahi kukutana na Ben????

Mkuu hakuna jiwe litalobaki juu ya jiwe.
 
Ben Saanane muda wako wa kuonekana unafiki wako umefika, nilisema jana kwamba wewe ni mnafiki na msaliti namba moja. Shaaaaaaaaaaaame!!!!! Kijana wa aina yako kutumika kama Condom.

Ben saanane Njoo hapa haraka kabla kitila mkumbo hajashusha unafiki wako hapa
 
habari, nimeona mchango wangu huu niuanzishie uzi ili tujadiliane kwa mapana..

mpaka tuufikie tunaouita ukombozi wa pili, basi tuna kazi na safari ndefu sana!

kama vijana tunaweza tukainuka na kuanza kuporomosha mashtaka na kutaja majina ya watu bila hata facts, basi kazi ipo ndugu zangu.

Ufahamu wangu ni kuwa ili tufanikiwe kuwaondoa ccm madarakani lazima tufanye kazi hiyo kama timu moja, mawazo yangu ni kuwa hatutaweza kufikia hatua yoyote ikiwa tutakuwa na vijana wa namna hii.

Vijana wa aina ya ben saanane wanaoweza kukaa, kutengeneza mgogoro, kubuni njia za kuuendesha mgogoro, kutafuta suluhu na hatimaye kwenda kuuza huo mgogoro kwa viongozi wengine huku akiamini kuwa anakinusuru chama hakika anakosea sana.

Vijana wa aina ya saanane ambao kazi yao nikutumia muda na akili zao nyingi kuwarubuni na kuwagombanisha vijana wa chama na viongozi wa chama ni hatari pengine kuliko ukoma.

Kwa kuwa mara kadhaa amekuwa akinitaja kwenye mijadala yake yote. Bila hata kuangalia namna ninavyohusika, na kwa kuwa na leo hii ameamua kunitaja na kunihusisha moja kwa moja, na kwa kuwa viongozi, vijana na wanachama wengi wa chadema wamekuwa wakinihusisha mimi kuwa karibu sana na zitto kabwe. Leo nitasema kitu kwenye hili.

1. Naomba niweke wazi hapa leo, kuwa sikuwahi kumfahamu mtu anayeitwa ben saa nane kabla mwezi wa nne 2011.
Sijawahi kumsikia jina wala kumuona sura yake.(hawezi kubisha kwenye hili)

2. Ben ndiye alikuwa wa kwanza kunipigia simu, kati kati ya kipindi cha kampeni za uchaguzi wa bavicha - 2011 mimi nikiwa nagombea uenyekiti na yeye akiwa ni mgombea wa kimkakati(alitumwa na baadhi ya viongozi kuja kuuvuruga uchaguzi-uthibitisho upo) ambapo aliponipigia simu na kunieleza kuwa tuna haja ya kukaa kama wagombea na kuangalia namna tunaweza shiriki salama kwenye huo uchaguzi kwa madai kuwa amepata tetesi makao makuu wanamgombea wao na wanajiandaa kukata majina ya watu, jina lake na langu yakikiwemo. Nilimsikiliza na kumpuuza.

3. Baada ya hapo sijawahi kuwasiliana nae tena ben saa nane, mpaka usiku wa siku jina langu limekatwa na kamati kuu ya chama, tena aliwasiliana na mimi kupitia grayson nyakarungu, aliyekuwa swahiba wakecha kusikitisha ni kuwa mwana mkakati ben aliwashauri mwampamba, nyakarungu na kisandu kuungana, akanishirikisha na mimi. Huku nikijua dhamira yake kuwa ni unafiki. Nikamsikiliza kwa kuwa sikuwa tena na cha kupoteza (nimeshaenguliwa tayari).

Masikini ya mungu ben akawahadaa vijana wa watu (mwampamba na nyakarungu) wakaenguliwa huku yeye akiwa ni wa kwanza kukiri kuwa wameamua kuongeza nguvu.

4. Unafiki wa saanane uliendelea siku ya tatu baada ya kuisha kwa uchaguzi wa bavicha maana baada ya kukatwa jina langu, wanafiki wengi walifikiri ningetoa tamko la kukipinga chama ama kuhama chama, sikufanya hivyo, kwangu mimi uchaguzi ule haukuwa ligi, ilikuwa ni mechi tu ya kirafiki. Hapo mwenyekiti wa chadema wilaya ya kibaha akaomba kukutana namimi, nikakubali, nikakutana nae ubungo plaza, tukiwa hapo tulikuwa na mwampamba na nyakarungu, aliposimuliwa saa nane kuwa tunaenda kukutana ubungo plaza, akaandika humu jamii forums kwa kutumia id fake yake kuwa tumekutana na mimi nina mpango wa kuhama chama.

Nlimwambia mwampamba kuwa saa nane ana kazi maalum, mwampamba hakunielewa, akanipinga sana sana sana, naamini leo atanielewa vizuri sasa.

5. Kwa kipindi chote hicho saa nane alikuwa anaitisha vikao vya kila aina, saa nane anatukana na kutoa kejeli za kila aina kwa viongozi wa kuu hasa katibu mkuu na mwenyekiti (lengo ni kutaka kluthibitisha kuwa kuna vijana wanawapinga viongozi hawa). Ninataja maeneo machache ambayo saa nane alipenda kuitishia vikao vyake, kwa john fedha-kinondoni, blue pearl hotel-ubungo plaza na luch time hotel-ubungo external.naomba nikiri hadharani hapa, si mimi, mwampamba wala juliana anayemsema aliyewahi kwenda kukutana na saa nane akajinunulia kinywaji wala chakulakwa saa nane huwa tukifika tunakula, tunakunywa mpaka tunapochoka saa nane yeye hulipia-tukambatiza jina tukamwita manji. (lakini siku zote nimekuwa nikiwaambia wenzangu kuwa kaeni chonjo na huyu jamaa ana kazi maalum---leo wamejionea)

6. Kati kati mwaka jana 2011 mwenyekiti wetu wa taifa freeman mbowe alikamatwa kwa kilichodaiwa kutokutii amri ya mahakama hapa napo saa nane akafanya vitu vyake, kama kawaida yake, akawakusanya vijana wake wote ambao yupo nao kwa kazi maalum akaanza kuwajaza ujinganaomba nikiri tena hapa kuwa usipokuwa makini ni rahisi sana kuingia kwenye kumi na nane za huyu jamaa. Ni lalzima uwe makini kama mchange kumshinda na ndio maana ananichukia sana sana.

Mimi nimefundishwa kuwafahamu wanafiki. Hasa ninapokuwa naongea nao uso kwa macho saa nane kwangu alikuwa mnafiki kwa hiyo sikumpa nafasi hata chembe.

7. Katika kipindi chote hiko sijawahi kumsikia mwana mkakati saa nane akiwasema vizuri viongozi wa chadema. Mtu pekee aliyekuwa anamsifia alikuwa ni zitto.

saa nane na zitto
nimeshtushwa sana na maandishi aliyoyaandika saanane leo, hii inatokana na ama kuchanganyikiwa au kujihami kutokana na kushushuliwa na kuonekana mwongo. Naomba nieleze vizuri hapa.

1. Ben saanane ndiye alikuwa muitishaji mkuu wa vikao vya hotelini(makutano) akiwa na saa yake ya kurekodi aliyonunuliwa na kiongozi mmoja wa chama kwa kinachoitwa kazi ya ushushu. Yeye ndiy aliyekuwa mwenyekiti wa vikao na mwandishi wa kila kinachosemwa.

2. Ni ben saanane ndiye aliyewashawishi na kuwalazimisha wenzie anaowasema leo ni wasaliti waunde kikundi. Hakuishia hapo, akakitunga mpaka na jina. Kuwa ni patriotic movement seven na akakifupisha pm7. Akashawishi kikundi hicho kizunguke nchi nzima kuhamasisha viongozi wa huko kufanya mageuzi ndani ya chama. Saa nane unafiki utakupeleka pabaya.

3. Ni ben saanane ndiye aliyegawa majina ya kuitana miongoni mwa wana kikundi hiko, yeye akajipa jina la cobra, mimi akanipa mdude (kwa kuwa nilikuwa naijua dhamira yake niliendelea kumkeli)

4. Ni ben saanane ndiye aliyeshauri namna ya kuhakikisha kikundi hicho kinapata pesa, wakati mimi nilimpinga ku anzia kuanzisha hiko kikundi mpaka namna ya kukusanya kwake pesa..wakati yeye alikuwa anasisitiza kwenye njia ya kukusanya michango, tena tuwachangishe viongozi wa chama na watu wengine maarufu.

5. Akiwa mkweli atakumbuka na kukiri kuwa nilimwambia kuanzisha kikundi hicho ni sawa na kuanzisha chama ndani ya chama, aliumizwa na misimamo yangu sana.

6. Ni ben saanane ndiy aliyekuwa anasisitiza tuombe kukutana na zitto kabwe ili tumuombe ufadhili wa kufadhili kikundi chetu kilichoasisiwa na saanane na akanipa jukumu la kuhakikisha ninamwambia na kumshawishi zitto tukutane nae tufanye nae kikao, sababu yake kubwa ni kwamba zitto ni rafiki yangu sana na itakuwa rahisi kumpata. Hapa tulirumbana sana, mimi nilielewa dhamira yake na nikiri leo hadharani kuwa nilimshauri zitto asikubali kukutana na kikundi hiki, na niukamwambia kabisa kuwa lengo la kikundi hiki ni kuthibitisha makundi ndani ya chama.-leo yametimia.

7. Ni saanane aliyewaapia kujito a kwenye kikundi alichokianzisha mwenyewe kwa sababu ya kutokumpata zitto kwenye kikao, siku ambayo saa nane alipendekeza zitto tukutane naye zitto alikwenda marekani kuzindua tawi la chadema, ni saa nane ndiye aliyenilaumu sana kuwa kwa nini sikumuarifu kuwa zitto hatokuwepo, nilimjibu sio wajibu wangu kuwaambia watu kuwa zitto yupo ama hayupo.

8. ni saanane huyu huyu mnafiki tuliyerumbana naye hasa mimi nay eye juu ya namna ya kumshirikisha zitto kwenye michango ya kikundi chake cha pm7. Naomba ninukuu mabishano yetu..mimi  kama swala ni kukusanya pesa, kwanini tumfuate zitto kwanza na sio mtu mwengine yeyote?...saa nane..kwa sababu zitto ni kijana na ana mitazamo chanya kwa vijana wenzie na pia tunafanana nayo mitazamo hiyo sio kamakina mnyika wao status quomimi..kama zitto tumemwomba tuonane naye na amesafiri bila kutujibu hauoni kuwa anatuudharau, kwanini tujipeleke kwa zitto tunayemnungunikia kila leo?..saa nane..  hapana ni lazima atusaidie, zitto kwa vyovyote lazima agombee uenyekiti, na hatuwezi fanya hii kazi tukamfungulia milango bila nay eye kutoka jasho lake, ni lazima atupe pesa.mimi sasa kwanini tunakataa wenzetu kutumiwa halafu na sisi tunajitumikisha wenyewe kwa zitto?saa nane..mchange, hakuna jinsi tunaweza acha mshirikisha zitto, mwisho wa siku zitto atakuwa beneficiary kwenye huu mpango ukifuatilia kwa makini mazungumzo yetu ambayo kwa bahati nzuri nimeyarekodi kuanzia siku ya kwanza mpaka ya mwisho utaweza kumuelewa saanane kuwa alikuwa na kazi maalum.

Niseme hapa kuwa wote kwa pamoja, saa nane na zitto kila mmoja ameniambia kwa mdomo wake kuwa hawajawahi kuonana uso kwa macho, zitto yeye anasema kuwa anaweza akakutana leo na saa nane barabarani na akapishana nae bila kumfahamu.

Wote kwa pamoja wameniambia kuwa mawasiliano yao huwa ni kwa simu hasa sms na mara chache kwa emails.

Na moja kati ya malalamiko aliyokuwa ananipa saa nane nimpe zitto ni kuwa..
1.kwa nini hapokei simu za wapiganaji wake akiwemo yeye?...
2..kwanini anakuwa na mpiganaji kama saa nane na hataki kuonna nae.
3kwanini hataki kukifadhili kikundi cha pm7.?

kwa mtiririko wa matukio ulivyo, na kwa jinsi saa nane alivyoandika mashtaka yake dhidi ya zitto huku akizani anamchafua, hakika amejidharirisha sana.

Mtu mmoja mpinzani mkubwa sana wa zitto amenitumia sms kwenye facebook, ananiambia jf vipi maana computer yangu haifungui..huyu nae ni mjinga sababu anashabikia ujinga.

Kumshambulia zitto kwa mashtaka ya uwongo namna hii kuna mfanya zitto awe na nafasi ya kuonekana anasingiziwa mamba mengi sana hasa ndani ya chama.

Kwa mimi ninayemfahamu saanane nje na ndani, na ninayefahamiana na kufanya kazi na zitto, kwa mashtaka haya ya uwongo, basi hakika nitazidi kumuamini zitto.

Nitazidi kuamini kuwa zitto amesingiziwa mambo mengi sana ndani na nje ya chama, ninazidi kumuamini na kumtia moyo kwamba hizi ni hatua za mwisho za watu wanaokupinga, wakishindwa kukupinga kwa facts, watakupinga kwa uwongosaa nane amekubali kutumika vibaya kwa kisingizio cha kuwa anakilinda chama na viongozi wake.

Napata mashaka kama anakielewa anachokisema, huwezi kumtenganisha zitto na uongozi wa chama. Zitto ni naibu katibu mkuu wa chama, hivyo sio rahisi kumchafua zitto ukaacha kukichafua chama.

Nimemwona saa nane anajitetea kutishiwa kuuawa, saa nane, zitto akiwa na mimi amenusurika kuuawa kwa ajali ya gari hivi karibuni tukitokea morogoro kwenda iringa(siku ya kumbukumbu ya kifo cha mwalimu nyerere) baada ya wapinzani wake ndani ya chama kwenda kufungua nati za tairi la nyuma ili afe, kweli zitto ameaga kwao, kweli zitto hataweza kufa kwa mipango ya mungu, hatukufika mbali tuliushtukia mchezo tukarudi morogoro mjini na zitto akaendelea na retreat yao mpaka kesho yake tukarudi dar wala hakuitangaza hii sababu aliwadharau na mbinu dhaifu.

Sio rahisi kuitoa roho ya mwanadamu mwenzio, sio rahisi kumuua zitto kama mlivyojaribu mara kadhaa na timu yenu ..

Nasikitika sana kama vijana sasa tunaeza kusimama kidete na kuandika uwongo na kuutetea bila hata woga kama ndugu yangu saanane.

Hasira yako ya mimi kukushtukia na kuwaambia kina mwampamba na juliana kuwa wewe kila siku una warekodi na kwenda kuuza habari kwa kiongozi mmoja wa juu ambaye humtumia hawara wake kutuma sms za matusi kwa watu, isiwe sababu ya kuanza kuwachafua watu ndugu yangu.

Mchafue zitto kama unahisi una sababu ya kufanya hivyo kwa mambo ambayo una ushahidi nayo.

Saanane acha tabia ya kubuni mgogoro, kuuanzisha, kuuendeleza, na kisha kuutumia kama chanzo chako cha kupata pesa.

Saa nane, waislam wanasema sifa za mnafiki tatu (ayatul munafiq tharasa).
1. Akiongea huongea uwongo..
2..akiaminiwa hajiaminishi/hudhiaki..na ..
3..akiahidi hatimizi..

oh my god
hii inaonyesha ni vipi vijana wa nchi hii mnavyonuka majungu mwili mzima,wanafiki,msio na akili pamoja na kwamba labda mmekwenda shule kidogo lakini hata hiyo shule haiwasaidii kama kweli ndivyo mlivyo nchi hii kuikomboa kutoka ccm ni ndoto
vijana badala ya kuwa nguzo ya ukombozi mmekuwa wanafiki,wapika majungu hata wachawi tumeona sasa hata uchawi mmo leo mko hivyo si nyie ndio mafisadi yajayo? Mnajidai mko tayari kuwasaidia watanzania kuwa huru kutokana na ukandamizaji wa ccm kumbe mmekwenda kupeleka shida zenu na majungu na uchawi? Kazi ya siasa haiwafai mnafaa kuwa waganga wa kienyeji tu haya sasa kila kitu mmeeleza mnavyofanya siasa zenu za majungu,kichawi hata wazazi wenu nawahurimia waliwapeleka shule mkawe wachawi au majungu na kujipendekeza kwa watu ndio kinachowaweka hapo dar make bila majungu na kijipendekeza kwa viongozi hamuwezi ishi dar? Si rudini kwenu mkalime? Acheni upumbavu mmetuchosha na thred yenu mbovu
ndio mnalalamika kwamba wazee hawztaki kuachia nafasi vijana wafanye kazi mtafanya kazi gani kama mawazo yenu ni majungu,uchawi? Shame on you f***k you
 
Kwanza nimefurahi kuona kondoo wa bwana wanazidi kkurudi zizini,

Maelezo yako yote yamekuja kuthibitisha tu kile alichokisema Ben Saanane na Mamuya,
Ben Saanane na Mamuya wamekiri wazi kuwa walikuwa kwenye hilo kundi na walifanya kila aina ya maovu kwa chama,

Sasa wamemrudia Mungu wao nae amewaweka HURU.

Kimsingi unacholalamika ni kwanini wamewageuka tu,

Nashindwa kujua kwanini huombi radhi hapa ili jamii ikusamehe kama ilivyowasamehe akina Ben na Mamuya?

Unasubiri ukaombe radhi kwenye vikao vya chama? Kkumbuka jamii itaendelea kukuona msaliti tu. Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu,

Fungua UZI mwingine na uwaombe radhi wana jf na watz wote!

Karibu sana kundini bila shaka nawe umejirekebisha!

Bosi wenu Zitto anajutia, yupo msalabani anavuna alichopanda!
 
Hivi hiki chama hakina wenye busara? wale wazee wa matamko na makaripio wako wapi au wanaota jua subuhi hii.

mkuu.....lazima uone mbali zaidi ya kukurupuka kukemea na kuwaziba midomo hawa vijana balehe.
hapa ni wazi kwamba kuna maji moto yamemwagwa kwenye shimo la panya, sasa panya wanahaha.
fikiri, why now? think about that.

watu wanakuwa wepesi sana kuhukumu. Tujiulize, kama Mchange alikuwa anahudhuria vikao vyote vya PM7 mpaka akapewa jina, anajiondoaje kwenye hili sakata la uasi na mapenzi ya individual politician badala ya mapenzi kwa CHADEMA kama institution??!.
 
hizo ni akili za abunuasi, kwani kipindi mnaanzisha kile kikundi chenu cha MP7 zitto alikuwa tayari ameshatangaza nia ya urais?
Jibuni hoja za kijana Ben acheni uingiza watu wasiohusika kwani mliyafanya gizani sasa mchana kweupe yamewekwa.

TULIANZA NA MUNGU NA TUTAMALIZA NA MUNGU.

Asante Msemaji wa Ben Saanane ....Vp X-Mass simnakutana ROMBO
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom