Ben Saanane anavyoteseka na kivuli cha unafiki...

Ben Saanane anavyoteseka na kivuli cha unafiki...

vp zile sku tisini za kuogopana bado ngapi? Huku si tunachanana tu, chama ni uma sio mtu kama mnavoishi chama lenu magamba
Tumezisitisha kwa muda tunasubiri mazishi ya jirani yetu yapite ana hali mbaya sana muda wowote anaweza kututoka. Itakuwa si uungwana kwani ni mwezetu na tumefanyanae mengi pamoja vuta subira mkuu.
 
Mchange Juliana Shonza na Mtela Mwampamba kwanini mlikuwa mnatumia ID ya Tuntemkeke JF kuwatukana viongozi wa chama? Pia yale matusi mliokuwa mkitukana fcbk nayo pia mlitumwa na Ben? Pia yale matishirt yalioandikuwa MOVEMENT 4 CHAGAS mliyoyatengeneza kwa msaada wa mwigulu je nayo Ben aliwatuma?

Inahitaji akili ya maiti kuwaelewa.
anzisha thread mpya uulize maswali hayo ndugu yangu...hapa leo tunajadili namna SAA NANE alivyokubali kutumika ili kumchafua zitto. hayo mengine yaanzishie UZI WAKE.
 
Napata mashaka kama anakielewa anachokisema, huwezi kumtenganisha zitto na uongozi wa chama. Zitto ni naibu katibu mkuu wa chama, hivyo sio rahisi kumchafua zitto ukaacha kukichafua chama.

Nimemwona saa nane anajitetea kutishiwa kuuawa, saa nane, ZITTO akiwa na mimi amenusurika kuuawa kwa ajali ya gari hivi karibuni tukitokea morogoro kwenda iringa(siku ya kumbukumbu ya kifo cha mwalimu nyerere) baada ya wapinzani wake ndani ya chama kwenda kufungua nati za tairi la nyuma ili afe, kweli zitto ameaga kwao, kweli zitto hataweza kufa kwa mipango ya mungu, hatukufika mbali tuliushtukia mchezo tukarudi morogoro mjini na zitto akaendelea na retreat yao mpaka kesho yake tukarudi dar wala hakuitangaza hii sababu aliwadharau na mbinu dhaifu.

Sio rahisi kuitoa roho ya mwanadamu mwenzio, sio rahisi kumuua zitto kama mlivyojaribu mara kadhaa na timu yenu ..

Nasikitika sana kama vijana sasa tunaeza kusimama kidete na kuandika uwongo na kuutetea bila hata woga kama ndugu yangu Saanane.

Hasira yako ya mimi kukushtukia na kuwaambia kina Mwampamba na Juliana kuwa wewe kila siku una warekodi na kwenda kuuza habari kwa kiongozi mmoja wa juu ambaye humtumia HAWARA WAKE kutuma SMS za matusi kwa watu, isiwe sababu ya kuanza kuwachafua watu ndugu yangu.

Mchafue Zitto kama unahisi una sababu ya kufanya hivyo kwa mambo ambayo una ushahidi nayo.

SAANANE acha tabia ya KUBUNI MGOGORO, KUUANZISHA, KUUENDELEZA, NA KISHA KUUTUMIA KAMA CHANZO CHAKO CHA KUPATA PESA.

SAA NANE, Waislam wanasema sifa za mnafiki tatu (ayatul munafiq tharasa).
1. akiongea huongea uwongo..
2..akiaminiwa hajiaminishi/hudhiaki..na ..
3..akiahidi hatimizi..


Nilichogundua kwenye uzi wako huu ni wewe kuja hapa kujaribu kumshambulia Ben na kumsafisha Zitto na wewe kuacha kuzungumzia tuhuma zinazo kukabili..... Kijana acha ujinga, wewe na kundi lenu na Zitto mmeumbuliwa hivyo kuweni wapole mkaombe radhi au mjiondoe kabisa chadema...'

Hizi tuhuma za kujaribu kumuusisha Beni PM7 ni janja yenu ya kupakana matope ili muonekane wote hamfahi
 
Asante sana kamanda Mchange kwakuleta huu ufafanuzi, maana haya uliyoyaandika ndiyo nilkiyotaka kuyatolea ufafanuzi japo bado nitatoa ufafanuzi wangu kuhusu hizi shutuma ambazo kwangu mimi nachokiona ni sawa na mtu kuchimba shimo halafu akatumbukia yeye mwenyewe.

Suala la Ben kutumiwa kimkakati katika harakati zakumchafua zitto na sisi ambao wao hutuita masalia wala halijaanza leo, huu ni mkakati unaoratibiwa dhidi ya Zitto pamoja na vijana ambao wanamuunga mkono Zitto, nazidi kusisitiza kwamba Ben Saanane anatumia uongo kuuaminisha umma kwamba anamfahamu Zitto kitu ambacho hata nafsi yake nina hakika inamsuta.

Ben acha kukimbia kivuli chako, sio rahisi kumchafua Zitto kama unavyoweza kudhani, japo mnajitahidi sana lakini hamtofanikiwa.

Palipo ukweli, uwongo hujitenga .

Kwa hiyo unakubali kuwa kuna kikundi ambacho mmekianzisha cha kumnadi Zitto ndani ya chama. Je huoni kuwa huo ni uasi?
 
9k=
Mpango mzima bila hiki kifaa wewe si mwanachama hai wa PM7 waasi
images

hapo umenena mkuu daa ongera sana ko mlivoshindwa kumuua iringa,bungeni kwa kumnyunyuzia unga mkaamua kumnyonyoa nywere
 
Ukisoma vizuri uandishi wa hawa matutusa utagundua wote yaani Zito, saanane, mchange ni wajinga wajinga tu...
 
kwa nilivyoelewa mimi ni kuwa hizo pesa saa nane alikuwa anadhaminiwa na baadhi ya viongozi wakuu ambao kwao ili chama kiende lazima kuwe na migogoro. ndio maana wakamtumia saa nane, japo naye amefeli kabisa...
lakini pia humu kama nimemwelewa mtoa hoja kuwa amelazimika kujibu baada ya kumuona saa nane kila siku anamshambulia, lakini mchange ametoa hoja zaidi kuliko saa nane aliyejikita kwenye ushirikina.
cha msingi kuzingatia ni kwamba hawa wote ni wanachama wa chama kimoja. hivyo mijadala yao yote izingatie kwenye maslahi ya chama na sio pande zao hizi. wanapopambana tembo wawili. ni nyasi ndio zinaumia.

Mnafiki Mkubwa wewe
Hii migogoro imeanza baada ya uchaguzi wa 2010 hivyo unaposema kuna baadhi ya viongozi wakuu ambao kwao ili chama kiende lazima kuwe na migogoro ni upotoshaji ambao hautofautiani na namna mnavyorusha miguu hapa kujitetea.

Nyie ni wanafiki wakubwa sana, post zenu zote kuanzia kwa kigagula wenu mnajifanya kusimamia kwenye misingi ya umoja na kuiondoa ccm madarakani. mtaumbuka mwaka huu
 
Taswira unaelekea Umasalia flan Am sorry to say, Ben ni Msaliti Sawa Hilo limefahamika na yeye binafsi amekiri hilo na mamlaka husika watajua adhabu ya kumpa.Sasa swali kwa hao wengi Mbona hawajibu hoja ya msingi zaidi ya kutoa ufafanuzi?Shurianeni tu kuwa picha imeshaiungua na imeanzia kichwani. Jipangeni Upya.
ID yakio inasomeka hivi: Join Date : 19th December 2012

Mkuu huyo Taswira ni miongoni mwa wale masalia.
 
Last edited by a moderator:
Ni kwa sababu niliipima akili yake na kujua anachokitaka, na nisingeweza kumkimbia mapema kwa sababu angewasingizia mambo mengi sana wenzake.

Mpaka sasa baadhi ya viongozi wa chama wananichukia sana mimi, wanamchukia mwampamba na wengine, lakini hii ni kwa sababu ya uwongo waliokuwa wakilishwa na SAA NANE, yeye alikuwa anatuita tupumzike ama tupige story, halafu anakibadilisha kinakuwa kikao cha mikakati ya PM7 halafu anaanzisha maada za kujadili kisha anawarekodi na kupeleka kwa hao baadhin ya viongozi, masikini ya mungu viongozi wetu wanaamini na kuanza kuwaona wenzao waongo nakadharika.

Hii ni aina mbaya sana ya kufanya strugle, sisi hapa adui yetu ni CCM tu, tunavyopoteza muda kurekodiana wenyewe kwa wenyewe haisaidii kitu.

Muda alioutumia SAA NANE kuturekodi ili akauze habari angeutumia kufanya maswala ya msingi kwa chama hakika tungezidi kuwa mbali.

Lakini ndio hivyo tena njia ya mwongo fupi, na kila kitu sasa kipo hadharani.....NAENDELEA KU-COMPILE MANENO YAKE NILIYOMREKODI AKISISITIZA UANZISHWAJI WA PM7 NITAYAWEKA HUMU KILA MTU AMUELEWE SAA NANE NI NANI

Binafsi naona unanipa maswali mengi zaidi ya majibu, tafadali nisaidie ufafanuzi kidogo hapa mkuu

Hapo pa zambarau, naona umejibu kwa hoja dhaifu sana, kwa hiyo ulihudhuria ili uwatetee wenzio wasisingiziwe sio?! mbona umesubiri hadi yamekuja haya ndio ukajitokeza? unadhani huku ni kutetea watu ama kujitetea? Uzuri Ben kakiri kabisa kuhusu usaliti wake, wewe unasema eti ulimsoma akili yake ndio maana 'ukashirikiana nae' ila sijui kwanini yeye ndo kawa wa kwanza kuja kuwalipua humu maana kwa tafsiri ya maneno yako ulipaswa kuwa wa kwanza kufuchua mipango yake!?

Hapo pekundu, mtu akianzisha topic ambayo kwa ufahamu wako unaona ni usaliti na unafiki kwa viongozi na chama chako kwa ujumla, mchango wako katika hiyo mada unakuaje? Unapinga? au unaonesha jinsi ya kuufanikisha? maana naona unavyosisitiza juu ya kurekodiwa inaonekana unaelewa extent ya content ya usaliti wenu.

Hapo pa bluu, inaonekana maongezi ya vikao vyenu yalikuwa na uchangiaji ambao una'content iliyo na 'bei' nzuri, na ndio maana ukaweza kuwasilishwa kwa huyo mtu (aliyemtuma labda, kama yupo), ila pia inaonekana kila mmoja wenu ana hofu na kiasi gani kitatolewa kwenye forums kama ushahidi wa uhusika wenu, ndio maana mnakuja nusu nusu.

Binafsi naona kwa kuwa hamkuweza kupinga tokea wakati mnaanza vikao, mkaunda umoja na kupeana majina, mkahudhuria vikao na kupanga mipango kwa siri kuhujumu chama chenu wenyewe na chetu sote wapenda mabadiliko, huu ni usaliti mkubwa sana, na najua mlipaswa kulijua hili toka mwanzo.

Roho inaniuma sana, wananchi wapenda mabadiliko wanachanga shilingi mia tano, elfu,sio kwa kuwa wanazo nyingi, hapana, ila wanajitolea kuleta mabadiliko hasa baada ya kuchoshwa na hali waliyolazimishwa kuwa nayo kwa miaka mingi, leo hii tunagundua kuwa kati ya wale tuliowaamini kuwa wako mstari wa mbele wanashirikiana na adui kutuuza!!

Dhambi hii haitawaacha salama, Muda utaongea.
 
ben hawezi kumuingiza mtu yeyote king kati ya hao anaowataja yeye mwenyewe anajua ,anachofanya ni kutoa report ya uwongo kwa wale waliomtuma ili aonekane amefanikiwa kutimiza lengo.kitu ambacho si kweli.ukweli utajulikana tu.

Lakini ninyi hapa mna mu attack Ben kwa kusema tu kwamba amesema uongo? Hamjajibu hoja zake.Mwenzenu yuko tayari kwenda kwenye vikao vya chama.Ninyi mnakimbia kivuli chake na leo mmetumwa na Zitto kuja huku kwa kasi kumtetea.Ben has evidence,nilitegemea kama una busara kama makamu m/kiti BAVICHA.Ungeenda kupeleka suala hili kwenye Chama.Swali,Kwa nini ulikua kwenye kikundi hicho,na mission yenu ilikuwa nini?
 
Hivi hiki chama hakina wenye busara? wale wazee wa matamko na makaripio wako wapi au wanaota jua subuhi hii.
 
anzisha thread mpya uulize maswali hayo ndugu yangu...hapa leo tunajadili namna SAA NANE alivyokubali kutumika ili kumchafua zitto. hayo mengine yaanzishie UZI WAKE.

wewe mnafiki na msaliti mkubwa, hapa leo ni mbivu mbichi, jibunu hizo hoja hapa tuwaelewe na sio kuanza kutunga mashairi ya kuficha matunguri yenu hayo nyie masalia.
 
Nilichogundua kwenye uzi wako huu ni wewe kuja hapa kujaribu kumshambulia Ben na kumsafisha Zitto na wewe kuacha kuzungumzia tuhuma zinazo kukabili..... Kijana acha ujinga, wewe na kundi lenu na Zitto mmeumbuliwa hivyo kuweni wapole mkaombe radhi au mjiondoe kabisa chadema...'
mimi nimemuelewa vizuri sana mchange, na nimekuelewa vizuri sana pia wewe. ni kwamba mchange ameelezea namna viongozi wa chadema walivyotumia nguvu kuhalalisha kuwa zitto ana kundi ndani ya chama, na kazi hii alikabidhiwa SAA NANe, bahati mbaya kwake hakufanikiwa ndio maana ameingia mitini na kuanza kubwabwaja.

Hizi tuhuma za kujaribu kumuusisha Beni PM7 ni janja yenu ya kupakana matope ili muonekane wote hamfahi
sio rahisi kumtenganisha BEN SAA NANE na hiyo PM7 kwa kuwa ushahidi wa vidhibiti ambavyo mchange anasema anao unamgusa moja kwa moja BEN SAA NANE, ukiamua kumtetea hapa bila kujua ukweli utakuwa unapoteza muda tu, saa nane ameonyesha kukimbia kivuli chake na sasa amekubali kutumika kumchafua zitto tena anatumika vibaya sana.
Kwa hiyo unakubali kuwa kuna kikundi ambacho mmekianzisha cha kumnadi Zitto ndani ya chama. Je huoni kuwa huo ni uasi?
SAA NANE ndio anatakiwa atoe ufafanuzi zaidi juu ya huu mchezo wake wa kuigiza alioubuni kushirikiana na viongozi wa chadema wanaompinga zitto.
Ukisoma vizuri uandishi wa hawa matutusa utagundua wote yaani Zito, saanane, mchange ni wajinga wajinga tu...
si rahisi kuwaunga kundi moja hawa watu....SAA NANE amekwama kabisa.
 
Kama chama kinaweza kuvumilia watu wa aina yenu basi chama hakiwajibiki ipasavyo. Hiyo ni sawa na mmoja wa watoto katika familia aende akabwabwaje nje na bado akaonekana ni shujaa. Mnataka tuanze kuamini kwamba nyie hamna tofauti na UVCCM ambao kazi yao kulamba miguu ya wanasiasa wanaoutaka urais tena kwa vijisenti. Tofauti yenu na UVCCM itakuwa ni mavazi tu. Kwa nini msitumie muda wenu kukijenga chama badala ya kupiga kelele kwenye mitandao. Naona kila kona namsikia heche tu, utafikiri Heche ndiye BAVICHA,

Au mnataka tuzidi kuamini kwamba nyie wote mpo kwa kazi maalum ya kuisambaratisha CHADEMA. Kama mmoja wa wanafamilia kaenda kubwabwaja nje, je dawa yake ni kubwabwaja nje kama yeye? Au kwenda kumshitaki kwa wazazi.

Hapo ndio mnataka umri wa Urais ushushwe, sio ndio mwanzo wa kuwa na Raisi mbwabwaji na atakaye vuruga nchi
 
Tatizo la hiki chama hakuna adabu, na hiyo ndio inatofautisha CCM na CDM, pamoja na udhaifu wao ccm is well organised n more disciplined, hawaropoki ovyo ovyo tu kama hawa cdm yaani kila mtu anaropoka tuu, ovyo hakuna staha wala kujua nini cha kuongea mbele za watu na nini cha kuhifadhi twende kikaoni, ukiangalia hapa yupo mtu anaitwa Mchange, sijui juliana sasa hawa wote kwanini wasisemane kwenye vikao..nadhani hawa wanaojita vijana ni wavulana na wasichana sio vijana na sasa wanatumika kwa njaa njaa zao..

I can simply say you guys HAMTOSHI KABISA...

Mkuu Somoche, ccm ndio hakuna adabu kabisa. Hebu recall scenario ya majibu ya waziri wa sheria na mkuu wa nchi juu ya katiba mpya, matamko ya waziri na naibu wake kuhusu "uwekezaji" bandari ya Dar, kuvuana magamba n.k (na yote mbele ya waandishi wa habari)!!!!!
 
wewe mnafiki na msaliti mkubwa, hapa leo ni mbivu mbichi, jibunu hizo hoja hapa tuwaelewe na sio kuanza kutunga mashairi ya kuficha matunguri yenu hayo nyie masalia.
umeenda off-key kabisa kabisa...mimi si wa aina hiyo, weka mbele facts ntakuelewa, hasira zako subiri mijadala mnayokutana na watu wa aina yako na sio mimi.
HOJA HAPA NI KWANINI SAA NANE ALIKUBALI KUTUMIWA KUMCHAFUA ZITTO?. AMETUMIWA KWA MASLAHI YA NANI NA KWANINI?
 
Hakika dhambi ya usaliti haiwezi kuwaacha salama hawa wanafiki wote.

Hivi hamuoni hata huruma juu ya damu iliyomwagika Arusha, moro kwa ajili ya chama?
Hamuoni huruma juu ya wananchi masikini wanaotoa shilingi zao kwa ajili ya mabadiliko alafu leo hii mnadiliki kutusaliti?
 
Back
Top Bottom