Ukiiangalia hii juju unaona ni ubabe tuu wa serikali ya awamu ya tano lakini ukielewa kiundani utaona serikali iko sahihi. Na inachofanya ni kuweka ushindani halisi.
Baada ya soko huria kuanza '92 kukatokea makabaila (monopoly) wachache ambao walikuwa wanatumia nguvu yao kuhonga maafisa wa serikali ili waendelee kuhodhi uchumi.
Mfano mzuri ni biashara ya mafuta, zamani serikali ilikuwa ndiyo inayoagiza mafuta nje na bei ya mafuta nchini ilikuwa inaenda sambamba na ile ya OPEC.
Waliporuhusu makabaila kuagiza mafuta, tena bila kulipa kodi, jamaa wakaanza kuota mapembe kiasi cha kuigomea serikali, kuna kipindi walikuwa wanagoma kuuza na kuleta taharuki nchini. Leo hii mafuta yanauzwa chini ya $20 kwa pipa lakini jamaa bado wamekomalia kuuza kwa bei ile ile ya $53 kwa pipa.
Kwenye sukari ilikuwa hivyo hivyo jamaa walikuwa wanaficha ili kutengeneza uhitaji mkubwa (scarcity) na kuongeza bei, walikuwa na kiburi wakiigomea serikali ya Kikwete na serikali haikuwa na ubavu wa kukataa.
Sasa serikali haiwezi kuacha mambo yaende kiholela huku wananchi wengi wakiumia. Kuna wafanyabiashara wa vyakula huwa wanaongeza bei wakati wa mfungo wa Ramadhani, kila mwaka. Sasa serikali iache watu wake waumie kwa uhuni wa watu wachache?
Hata Amazon imezifunga account za watu wanaolangua bei ya sanitizers na Trump pia mwezi jana alikataza watu kufanya ulanguzi kwa bidhaa tiba wakati huu wa Corona.
Ndiyo maana nilisema, nchi zenye akili huwa haziachi mambo yaende kiholela.