Sijawahi kubaliana na aina ya miradi ya serikali ya ccm maana mingi ni miradi ya show off na kujitutumua ambayo kimsingi itasababisha hali ya maisha ya watzn kuwa ngumu kuliko kuwasaidia
Haiingii akilini kuhangaika na midege,sgr,sijui umeme wa matrioni wakati hata mgwatt 1360 za sasa zina soma surplus,hizo zingine zote za kazi gani? Madaraja ya kuvuka maziwa na bahari ya kazi gani? Hivi tunavyoongea barabara ni kero kubwa sana kwa nchi,mahospitali na shule usiseme kuna msongamano ni hatari yaani serikali inachojigamba ni kitu kidogo sana ukilinganisha na mahitaji halisi na kasi ya kuzaliana.
Juhudi zingeelekezwa kwenye miradi ya msingi ya kumsaidia mwananchi directly yaani kinachotusaidia watzn ni ahueni ya mazingira sio harsh kama Kenya,Ethiopia na nchi zingine za pembe ya Africa vinginevyo tungesaga meno