Hayo mambo ya kwamba usipolipa utapokonywa unayaleta wewe...manake sidhani km kuna mkenya kayasema hayo..labda uwe una zuga tu...
Byda nani kakwambia km watanzania wana rent ardhi kutoka kw serikali...
Jombaaa, wacha kujitoa ufahamu, hapa tunaongelea leasing...
Na katika pachiko ilielezwa vizuri, mtu ana lease kutoka miaka 33, mpka 99..
Sasa nataka uje unieleze hyo leasing inamaana gani
Hakuna sehem article ya Tanzania land act inasema kuwa we lease land for 33 ,66 or 99 years.
Acha kujichanganya man.
Unapokodisha kama haujalipia inamaana utapokonywa kitu ulichokodi .
SURA YA PILI
MASUALA MUHIMU KATIKA SERA NA SHERIA ZA ARDHI NCHINI TANZANIA
SERA YA TAIFA YA ARDHI YA 1995
Sera hii inaweka kanuni za msingi zinazotawala mfumo mzima wa umiliki, usimamizi na matumizi ya ardhi nchini. Kanuni hizo ni pamoja na:-
· Kutambua kuwa ardhi yote ya Tanzania ni mali ya umma na kuwa imewekwa mikononi mwa Rais kama mdhamini kwa niaba ya raia wote.
· Kulipa fidia kamili, ya haki na kwa wakati kwa mtu yeyote ambaye haki miliki inafutwa matumizi yake.Pia kuwezesha ardhi kugawiwa kwa haki na kupatikana kwa raia wote
· Kuwawezesha raia wote kushiriki katika kutoa maamuzi ya mambo yanayohusiana na milki au matumizi yao ya ardhi.
· Haki ya kila mwanamke kupata,kumiliki,kutumia na kuuza au kuigawa ardhi kuwa sawa na haki ya mwanaume yeyote kwa viwango na masharti sawa
SHERIA ZA ARDHI ZA MWAKA 1999 NA SHERIA ZINGINE ZENYE MGUSO KATIKA ARDHI.
Maana ya ardhi
Ardhi ni ile inayojumuisha vitu vyote vilivyo juu na chini ya uso wa nchi vikiwemo majengo, uoto wa asili na maendelezo yote yaliyofanywa isipokuwa madini na bidhaa za mafuta na gesi.
Makundi ya ardhi
Ardhi imegawanyika katika makundi matatu ambayo ni:-
1. Ardhi ya kawaida/jumla: ni ardhi yote ya umma ambayo siyo ardhi ya hifadhi wala ardhi ya kijiji. Hata hivyo, kwa mujibu wa sheria ya ardhi Na.4,1999 inajumuisha ardhi ya kijiji ambayo haikaliwi wala kutumiwa na wanavijiji. Kamishna wa ardhi ndiye msimamizi wa kundi hili la ardhi.
2. Ardhi Hifadhi: ni ardhi iliyotengwa kwa shughuli maalumu kama vile hifadhi za misitu, barabara, vyanzo vya maji nk. Kundi hili liko chini ya usimamizi wa mamlaka mbalimbali za aina ya ardhi husika.
3. Ardhi ya Kijiji: hii ni ardhi iliyo ndani ya kijiji kilichosajiliwa na kubainishwa mipaka. Kwa mujibu wa sheria ya serikali za mitaa (Mamlaka za Wilaya), ya mwaka 1982 na kuwa chini ya usimamizi wa Halmashari ya Kijiji. Pia ardhi ya kijiji ni ardhi iliyotengwa chini ya sheria ya uundwaji wa vijiji,1965.Vilevile, ardhi ya kijiji ni ardhi ambayo si hifadhi, na kwa muda wa miaka kumi na miwili kabla ya sheria ya ardhi ya vijiji,Na.5 kutungwa, wanakijiji wamekuwa wanaikalia na kuitumia kama ardhi ya kijiji na pasipo kuwepo na aina yoyote ya umiliki au matumizi kabla au wakati wa ya kipindi hicho
MFUMO YA UMILIKAJI WA ARDHI
Kuna aina kuu mbili za umilikaji wa ardhi nchini Tanzania
· Umilikaji ardhi kimila: Huu ni utaratibu wa umilikaji ardhi kwa kufuata taratibu za kimila na desturi za jamii husika. Aina hii ya umiliki hutumika katika ardhi ya kijiji kama ilivyobainishwa katika sheria ya ardhi ya vijiji Na.5,1999
· Umilikaji ardhi kwa Hati: huu ni utaratibu wa hati unaotumika na kutolewa katika kundi la ardhi ya kawaida/jumla. Katika utaratibu huu mtu anaweza kumiliki ardhi kwa hati ya miaka 33, 66 au 99 na anakuwa na hadhi ya upangaji.
Upatikanaji wa Ardhi
Ardhi inaweza kupatikana kwa njia zifuatazo:-
i. Kurithi
ii. Kusafisha pori/eneo lisilo na mmiliki
iii. Kununua
iv. Kupewa zawadi
v. Kugawiwa na serikali
Mamlaka za usimamizi wa ardhi
1. Halmashauri ya Kijiji- Hii haimaanishi kuwa Halmashauri ya Kijiji ni mmiliki wa ardhi ya kijiji bali ni msimamizi tu na haina mamlaka ya kugawa ardhi au kutoa ruhusa ya kutumia ardhi kimila bila idhini ya mkutano mkuu wa kijiji.
2. Mkutano Mkuu wa Kijiji- ndicho chombo chenye madaraka ya juu kijijini juu ya masuala yote ya yakiwepo masuala ya ardhi kama vile kuthibitisha na kukubali au kukataa maombi ya ardhi ya kijiji.
3. Kamishna wa Ardhi- ndiye mtendaji na msimamizi mkuu wa makundi yote ya ardhi na amepewa majukumu ya kiushauri kwenye ardhi ya vijiji.
Ebu soma vema.
Hiyo miaka 33,66 na 99 ni muda wa hati miliki.
Halafu panda juu kasome ardhi ya jumla ikoje.
Na hii wala haikuondolei umiliki wa ardhi yako bali huleta shida tu ktk ulipaji kodi TRA basi.
Asa sijui wapi tunakodishiwa ardhi ebu nitafutie neno kuwa tunakodishiwa ardhi.
Na soma aina za upatikanaji wa ardhi.
Halafu usiwe kichaa kiasi hiko Tz wapo wanao rent ardhi serikalini ktk shirik la nyumba la taifa NHC.
punguza miraa na gongo buddah.