babayao255
JF-Expert Member
- Apr 4, 2019
- 12,905
- 34,907
Cha ajabu hao wachina sasa hivi wanawapapasa wakenya balaa 



Hivi wewe unajua uhusiano wa China na Tanzania au unajiongelea tuu?
Watu tumekuwa na uhusiano na wachina toka 60's na kuwasaidia kupata kiti UN kwa ushawishi wa Nyerere chini ya Dr. Salim, bifu lilikuwa kubwa mpaka Ronald Reagan wakati huo governor wa California akachanganyikiwa na kumpigia simu Nixon akitukana (hizi recodi za sauti kutukana zimetolewa juzi tu hapa na library of congress).
Huyo Reagan mwaka 1982 akiwa Rais wa Marekani serikali yake ikapiga kura ya veto kumzuia Dr. Salim asiwe katibu mkuu wa UN kwasababu yeye ndiye aliyewawezesha China kuwa na kiti cha UN badala ya Taiwan, miaka 10 iliyopita. Halafu eti leo ninyi ndiyo wa kutufundisha kuhusu umuhimu wa China?
