Medical interns to earn Sh206,000 in salary deal
www-businessdailyafrica-com.cdn.ampproject.org
Ukisoma vizuri hii article utaona kwamba hiyo Kshs 206,000 sio basic salary, hiyo ni pamoja na allowances ambazo zinatofautiana sana, kwa mfano "call allowances", inatofautiana toka mwezi hadi mwezi na inategemeana na idadi ya doctors waliopo katika hospitali husika.
Kama unataka kulinganisha, ni lazima utumie basic salary ambayo ni constant kwa doctors wa nchi nzima, kumbuka doctors waliopo Wajir na Turkana hulipwa hardship allowances wakati wa Nairobi hawalipwi.
Kuhusu kulipa mishahara mikubwa, unapaswa ulipe kwa wote ili kusiwepo na gap kubwa kati ya mishahara ya watumishi, vinginevyo migomo haitokwisha na " inflation " itakuwa ikipanda sana. Kwa Kenya kutoa mishahara mikubwa inasababisha kupunguza uwezo wa serikali kufanya mambo mengine ya maendeleo kwa sababu 50% ya revenue inatumika kulipa wages, GoK inabaki na pesa kidogo kushughulika na miradi ya maendeleo.