Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Alafu nyang'au analeta maneno ya kwenye khanga kua wao walishasoma sijui form one & two. Hajui ile ilikua ni introduction to...
 
Noma sana hiyo Hisabati. Mi sana sana najua tu kubonyeza kitufe cha camera tena sio sana . BTW did CBG lakini nilikimbizwa na Organic chemistry🤣, nikatorekea HGL piga one yangu ya point 6 nasurvive sasa hivi kama kawa .





 
Hahahaaaaaaaaaaa
Kaka unawaweza sana hawa nyang'au yaani unawagonga panapouma vilivyo.
Hawa jamaa viingereza viiingi basi mi hua nawachoraaa hawana lolote hawa. Utasikia mara ooh! Hiyo kwetu ni ya class four, wanadhani elimu ya bongo ni ya kitoto. Woote wamekimbia saa hizi, na tunataka wakirudi mjadala wa elimu uendelee kudaadek
 
mkuu nimesoma PCM kiukweli sitokuja kumshauli ndugu yangu wa karibu apitie hiyo level, katika maisha yangu sijawai kupitia kipindi kigumu kama iko cha miaka miwil yan mtu unasoma usiku na mchana ila unaishia kupata 30-40 za physics n math kuna kipindi kilifika adi nikawa najuta kusoma kiukweli advance ndio level ngumu katika ngazi ya elimu mtu unapewa kitabu kikubwa sana alafu unaambiwa hicho ni cha form five naapa mtu aliyepitia advance level ya tanzania naamini na akapata ufaulu mzuri basi anaweza kushindana na mwanafunzi wa shule yeyote africa
 
Alafu nyang'au analeta maneno ya kwenye khanga kua wao walishasoma sijui form one & two. Hajui ile ilikua ni introduction to...
Hawaujui mziki wake, yaani shule inaanza form V. Huko O level ni kupeana tu matumaini. Kuna jamaa mmoja tulianza wote 5 ila kufika mwezi wa 9 akaona ngoma ngumu na akifanya mchezo itakua 2 years fighting for food akatimkia zake diploma ya clinical medicine.
 
wakenya tunaomba muweke mtihani wa kidato cha nne ili tusonge
hahahaha.... wanarusha maneno tu hewani. wengi wao ni vilaza. elimu yao imejikikita katika kuwafanya wajue kuzungumza kingereza. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
mimi mwenyewe nakaa kando cos nipo allergic na numbers.... hapa namuachia Annael na magwiji wenzie wasimamie show.

nataka nione how intelligent this kenyans are in maths.
Hawa jamaa ukiwasikiliza kiingereza chao waweza dhania they're so bright minded kumbe just linguists only.
 
Nipo nasubiri. Mimi nimewahu kuwa teacher wa Mathematics A-level.
Wakenya leteni solutions zenu kwenye karatasi kisha pigeni picha.
Hata hivyo kuna watu kesho wataenda kutafuta msaada. Tutajua tu kama umepewa msaada. Maana tutakuuliza maswali ya ziada.
 
Hahaaa mkuu ktk kipindi kigumu nilichowahi kupitia kwenye kisomo jamani ni advance aiseeee duuuuuh! Akyanani jamani yale ni matesoo hayo ma organic, hayo ma mechanism ya Bios mwee mweeee
 
Haaaahahaaa! Mimi elimu yangu ya hesabu ni form 4 ya tz. hata hivyo hii paper naiona ni simple kabisaaa.
unachekesha au kisa umeona set na statistic apo pamoja na function yani hizo ndo z kuponea na mpaka ukutane nazo zinaenda il ukikaa vibaya nazo zinakupiga bt angalia na topic nyingne kama zinaenda mana hesabu ukiangalia kwa macho tuu mbona unapata 100
 
Hii kwa Sisi wazee wa BAM ni changamoto. Inaitwa Advanced Mathematics na kama wewe ulifanya paper imeandikwa basic Mathematics basi Kaa pembeni
 
vilaza wakubwa hawa.... elimu ya sekondari ya tz sio masihara. ni jiwe kweli kweli.

nimekaa na popcorn zangu nasubiri kuona mkenya anatuma picha au screen image inayoonyesha namna alivyo solve maswali na mpaka akapata jibu.
 
Tena ukose walimu na hukwenda tuition mbona utatoboka mpaka uumwe macho [emoji102] [emoji16] [emoji16] [emoji16]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…