Nimefanya kazi hapo Nairobi kama mfanyakazi wa shirika la wamarekani, ninafahamu jinsi mnavyobaguana kwa misingi ya ukabila katika sectors zote, kuanzia elimu, ajira, maeneo ya kuishi watu na hata katika nyumba za ibada, kwahiyo acha kutudangaya kwamba ubaguzi ni wakati wa uchaguzi pekee.
Kuhusu maendeleo, Tanzania ipo mbali sana na kamwe hamuwezi kuifikia tena. Kwetu tunapima maendeleo ya nchi katika mambo yafuatayo,
1)Uwezo wa wanainchi kupata lishe bora
2)Uwezo wa wananchi kuwa na makazi yenye hadhi ya kuishi binadamu
3)Uwezo wa wananchi kupata matibabu bora
4)Upatikanaji wa ajira kwa wananchi walio wengi
5)Kupungua kwa kiwango cha umasikini miongoni mwa wananchi
6)Kupunguza tofauti ya kipato kati ya masikini na tajiri
Katika hayo, onyesha ni wapi Kenya imeizidi Tanzania?. Au wewe sema maendeleo ambayo unayasema wewe ni yapi?