Kwa mujibu wa wataalam wa Uchumi wanasema leo hii Tanzania ikifanya GDP rebase itaongezeka kwa 50% to 60%. Nigeria walifanya na uchumi wao ukaongezeka kwa 89%
Hapa tunasema hivyo kwanini:-
1.
Mobile Money Ecosystem - Hii kwa kuangalia transaction zilizowekwa na TCRA unaona namna ya miamala inavyoongozeka kila kukicha. Hii huwa haiingizwi kwenye GDP ya sasa kwa sababu Base yake haikutambua haya mambo
2.
TIPS & GePG - Ukiangalia malipo yote ya huduma zinazotolewa na serikali zinalipwa kwa kupitia GePG. Hii nayo ni namna ya kupata expenditure nayo inaongeza GDP
3.
Masoko ya Madini - Kwa sasa zaidi ya kila eneo kuna masoko ya madini. Taarifa za wachimbaji wadogo zilikuwa haziwekwi kwenye GDP lakini kwa sasa zinapatikana.
4.
AMCOS Data Aggregation: Agricultural Marketing Co-operative Societies hii imesababisha mauzo ya mazao yawe ya wazi na kuondoa walanguzi.
5.
Stakabadhi Ghalani - Hii nayo ni sehemu inaongeza GDP
6.
The 130% Food Self-Sufficiency Surplus - Kwa sasa Tanzania tunajitosheleza kwa chakula, na hii ni maana halisi ya per capita kubwa
7.
The Short-Form Content & Media Explosion: Kwa sasa Google, Facebook, Tiktok na mitandao mingine ipo intergrated na mifumo ya TZ kwahiyo hizo views na megine vinakuwa calculated kwenye GDP
8.
Bodaboda and Bajaji networks: Hii nayo ni moja ya namna GDP inaweza kuongezeka
Haya ni machache tu lakini inaelezwa kuwa Tanzania ikifanya rebase GDP itakuwa $155B na per capita itakuwa $2,200