Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

ndio maana tunaona matokeo chanya Tanzania bila munkari!
 
ambayo hailipwi in full! hata sie tuna budget ya city/town/district councils pia!
Kwetu Tanzania Halmashauri zinakusanya mapato vizuri sana kwasababu yupo mratibu ambaye ni TAMISEMI, huko kenya mapato ya County yanasimamiwa na mwanasiasa ambaye ni Gavana, kwahiyo hapo hakuna utaalamu wowote.

Kwetu Meyor yupo kisiasa bali kuna mtu anaitwa Mkurugenzi. Makusanyo yetu na bajeti za Halmashauri zinakuwa chini ya baraza la madiwani na kapato hukusanywa kwa kutumia mfumo wa LGRCIS

Mfumo wa kenya unavutia sana ufisadi na rushwa. Hatutakiwi hata siku moja kuwa na mfumo kama wa kenya.

Check tofauti


KipengeleHalmashauri za TanzaniaCounties za Kenya
UsimamiziInaratibiwa na TAMISEMI (Moja kwa moja).Inaratibiwa na Gavana (Nguvu ya Kisiasa).
UvujajiMdogo (Mifumo ya kielektroniki imefungwa nchi nzima).Mkubwa (Mifumo ya kaunti inatofautiana na haina udhibiti mkali).
Gharama za UkusanyajiChini (Inatumia watumishi wa umma waliopo).Juu (Kaunti nyingi hukodisha kampuni binafsi kukusanya mapato).
 
In Ingekuwa tofauti wasingekuwa na allocation kwenda counties🤣.
Inshort bajeti yao ni ndogo sana, kupitia local governments zinatengenga fedha za maendeleo kulingana na mapato. Mfano dar , municipality zote zinatakiwa kutenga 70% ya makusanyo yao kwenye maendeleo huku wakitakiwa kuwa na 10% kwa ajili ya mikopo.
 
Leo hii ndio mmegundua mambo ya Bonds?😂😂😂.

By the way Kenya's financial assets are 10 times ya Tanzania.
Hizo assets na bado hata kufund simple stadium like Talanta mpaka mtapeliwe 10 times na mchina! 😢
 

Correction mfumo wa ukusanyaji mapato sasa hivi ni TAUSI hapa hakuna Cha kuforge risiti Wala nini.
Waziri wa tamisemi anaweza kuona makusanyo yote ya halmashauri na defaulters,
Bajeti target za makusanyo lazima zifikie walau kwa 60% ya makusanyo.
Kuna mapato lindwa na mapato yasiyolindwa.
Mapato lindwa ni ya vijiji na hospitali za wilaya na zahanati.
Mapato yasiyolindwa ni Yale ya halmashauri .
 

Inshort tukija kwenye local governments, Tanzania Ina perform vizuri sana, ni nadra kukuta shule za miti kama kenya
 
Wanafikiri oil tankers ni kama container ships 😂😂 hata Dangote akichagua Kenya, meli za mafuta hazotadock kwenye port berths kama wanavyodhani
 
Na usichojua kenya kuna budget ya serikali kuu na budget ya county

Kenya's FY 2026/27 budget​

Projections show total revenue at Sh3.6 trillion, creating a fiscal deficit of Sh1.1 trillion, equivalent to 5.3 per cent of GDP

by ROSA MUMANYI



Kenya’s proposed 2026/27 financial year budget will hit Sh4.8 trillion, with education receiving the largest allocation as the government prioritises learning, security and infrastructure.

Treasury projections show total revenue at Sh3.6 trillion, creating a fiscal deficit of Sh1.1 trillion, equivalent to 5.3 per cent of GDP.

Education has been allocated Sh668.3 billion, accounting for 28.5 per cent of the budget, followed by national security at Sh566.9 billion.

Roads will receive Sh230.3 billion while the health sector has been allocated Sh170.7 billion.


Treasury also revised Kenya’s projected economic growth downwards from 5.3 per cent to 5.0 per cent.


MY TAKE
Na hi kutoka treasury?
 
Leo nitaelezea tofauti ya serikali ya Kenya na ya Tanzania hususani Cabinet.

Kwa utangulizi Tanzania inafuata mfumo unaoitwa Fusion of Powers na Kenya inafuata mfumo unaoitwa Separation of Powers.

AKA Mfumo wa Tanzania (Westminster Model) na Mfumo wa Kenya (Pure Presidential System).

Tanzania tunaiga mfumo wa Uingereza lakini Kenya wameiga mfumo wa USA. Sasa naomba nieleze tofauti ya mifumo hii kiutendaji Kati ya Kenya na Tanzania:

Ulinganifu wa Mifumo ya Utawala: Tanzania (Fusion of Powers) vs. Kenya (Separation of Powers)​

Ili kuelewa kwanini Tanzania ina utulivu wa kiutendaji na Kenya ina mfumo wa ushindani mkali, ni lazima tuchambue kiini cha mifumo yao ya Baraza la Mawaziri (Cabinet).

1. Chimbuko la Mifumo (The Models)​

  • Tanzania: Inafuata Westminster Model (kutoka Uingereza). Huu unajulikana kama mfumo wa Fusion of Powers (Mshikamano wa Madaraka). Hapa, muhili wa Serikali na Bunge imefungamanishwa; huwezi kuwa Waziri kama wewe si Mbunge.
  • Kenya: Inafuata Pure Presidential System (kutoka Marekani). Huu unaitwa mfumo wa Separation of Powers (Utengano wa Madaraka). Mawaziri (Cabinet Secretaries) wako nje ya Bunge, na kuna ukuta mkali wa kisheria kati ya watunga sheria na watekelezaji.

2. Mwendelezo wa Taasisi na "Institutional Memory"​

Hapa ndipo penye tofauti kubwa ya kiutendaji ambayo huamua hatari au usalama wa miradi ya nchi:

Tanzania: Career Civil Service (Makatibu Wakuu kama Walinzi wa Dola)​

Nchini Tanzania, wizara inaendeshwa na Katibu Mkuu (Permanent Secretary).

  • Utaalamu (Technocracy): Hawa ni watumishi waandamizi wa umma ambao wamekulia ndani ya mfumo (Career Diplomats/Administrators). Sio wanasiasa.
  • Mwendelezo (Continuity): Katibu Mkuu ndiye "Accounting Officer." Hata Serikali ikimaliza muda wake au Baraza la Mawaziri likivunjwa, Katibu Mkuu anabaki ofisini. Miradi ya kimkakati haisimami kwa sababu "injini" ya wizara (Katibu Mkuu) haiondoki na wanasiasa. Hii inahakikisha kuwa nchi inaendeshwa kama Dola (State) na si kama kundi la kisiasa.

Kenya: Political Appointees (Wateule wa Rais)​

Nchini Kenya, mfumo unaruhusu Rais kuteua si tu Mawaziri (Cabinet Secretaries) , bali hata Makatibu (Principal Secretaries) kutoka nje ya utumishi wa umma.
  • Utii kwa Rais: Wateule hawa mara nyingi wanakuwepo kutekeleza ilani ya Rais aliyepo pekee. Hawana mizizi ndani ya utumishi wa umma.
  • Athari (Policy Rupture): Rais mmoja akiondoka madarakani, huondoka na timu yake yote hadi ngazi ya utendaji. Hii inasababisha nchi "kuanza upya" (Resetting) kila baada ya uchaguzi. Miradi mingi hukwama au kutelekezwa kwa sababu hakuna Makatibu wa kudumu wa kuilinda dhidi ya mabadiliko ya upepo wa kisiasa.

3. Uwajibikaji na Ufanisi wa Bajeti​

Tanzania: Uwajibikaji wa Pamoja (Collective Responsibility)​

Kwa sababu Mawaziri ni Wabunge, wanawajibika kwa wananchi na kwa Rais wakati mmoja.

  • Waziri anapokuwa Bungeni, analazimika kujibu hoja za kitalamu zilizotayarishwa na Katibu Mkuu wake. Hii inatengeneza muunganiko imara (Synergy) kati ya Siasa (Waziri) na Utaalamu (Katibu Mkuu).

Kenya: Utengano wa Kimamlaka (Check and Balance)​

Mawaziri wa Kenya huonekana kama "wafanyakazi" wa Rais kuliko wawakilishi wa watu.

  • Hii inasababisha msuguano wa mara kwa mara kati ya Bunge na Serikali. Bunge la Kenya linaweza kukataa bajeti au mipango ya Waziri kwa sababu tu hakuna ufungamanishi wa kikazi wa kila siku kati ya mawaziri na wabunge.

Mfumo wa Tanzania umelenga Uthabiti (Stability). Uwepo wa Makatibu Wakuu ambao ni watumishi wa kudumu unailinda nchi dhidi ya migogoro ya kisiasa. Miradi ya maendeleo nchini Tanzania inatambuliwa kama mali ya Dola, ndiyo maana hata awamu zikibadilika, mwelekeo wa kitaifa unabaki palepale.

Kenya, kwa kuiga mfumo wa Marekani, wameingia kwenye changamoto ya nchi kuendeshwa kwa "Msimu wa Rais" mmoja mmoja. Hii inapunguza kasi ya maendeleo ya muda mrefu (Long-term Development) kwani kila uongozi unakuja na watu wake wapya na vipaumbele vipya, huku ukiondoa watendaji wa zamani wenye uzoefu.

Kwa kifupi: Tanzania ina Mfumo (System) unaojiendesha, wakati Kenya ina Watu (Personalities) wanaoendesha mfumo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…