Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Bahati mbaya kigezo sio kimoja na vigezo vinabeba weights tofauti.

By the way size ya Manispaa ya Moshi vs size ya Mbeya ni vitu vitu 2 tofauti.
Vigezo hivi vinaitupa nje Mbeya, Mbeya ni shamba la nchi

2. Shughuli za kiuchumi
Uchumi imara wenye biashara, viwanda, huduma, masoko, benki, na mapato ya ndani ya kutosha.
Uwezo wa kukusanya mapato ya kuendesha huduma za jiji.

3 .Miundombinu
Barabara za uhakika
Maji safi
Umeme
Hospitali
Shule
Mfumo wa taka
Huduma za usafiri

4. Mpango wa matumizi ya ardhi
Urban planning/master plan rasmi
Maendeleo yaliyopangwa badala ya makazi holela
 
Ukiangalia kwa umakini Manispaa ya Moshi inaizidi Mbeya kwa vigezo karibia vyote.
Kwenye miundombinu Moshi ipo juu sana kuizidi mbeya, huu ni ukweli
Maspana ya Moshi Iko kwenye daraja la pili ambapo inatakiwa kutumia 60% ya mapato yake kwa ajili ya maendeleoa inamaaa mapato yake hayajafika bil 9.
Mbeya Iko daraja la kwanza ambapo inatumia 70% ya mapato yake kwenye maendeleo Ina maana mapato yake ni zaidi ya bil 9 . Moshi bado Iko nyuma sana ndugu
 
Vyanzo vya mapato jiji au mbeya jiji sio kilimo , kilimo hakifanyiki mjini.lazima kwanza ujue mbeya jiji inaanzia wapi na kuishia wapi.
Mapato ya jiji mara nyingi ni leseni, service levy ,parking , hotel levy na kadhalika. Ila mara nyingi majiji au manispaa karibia zote vyanzo vyake sio mazao ya kilimo bali uzalishaji na viwanda na majengo au hotel
 
Mbona unachagua kaka vigezo. Vigezo umeweka mwenyewe. Nimeongelea Kigezo nambari 3 kama ulivyosema. Moshi ipo na miundo mbinu na services bora sana Mbeya haiwezi hata kukaribia. Je unakubaliana na mimi Mbeya inazidiwa miundombinu na Moshi?
 
Mbona unachagua kaka vigezo. Vigezo umeweka mwenyewe. Nimeongelea Kigezo nambari 3 kama ulivyosema. Moshi ipo na miundo mbinu na services bora sana Mbeya haiwezi hata kukaribia. Je unakubaliana na mimi Mbeya inazidiwa miundombinu na Moshi?
Miundombinu kwako ni kama ipi kwanza tuanze , barabara ,majengo na kadhalika si ndo hivyo? Je una idadi ya barabara za Rami kwa mbeya versus Tanga, au unamaanisha vitu kama umeme? Bado hata tukisema tuangalie umeme bado tunaweza Fanya comparison ya matumizi ya umeme kwa mbeya versus Tanga hasa kwa eneo la t1 ili tuweze pata wapi kuna viwanda vingi au matumizi mengi yanayotokana na uzalishaji.
Kuhusu vitu kama hospitali au shule .
Moshi bado italabaki nyuma ndugu.
Hivi vitu usivipime kwa macho data zipo na Kila siku ziko updated.
 
Kaka sidhani kama unaifahamu Moshi. Moshi ndiyo inaongoza kwa kuwa na shule nyingi hapa Tanzania. Ndani ya manispaa ya Moshi Lami ni nyingi ukilinganisha na Mbeya. Hospital Moshi inaipita Mbeya. Hotels za kutosha moshi kuzidi Mbeya. Kaka moshi ipo na miundombinu bora kuzidi Mbeya. Tukija kwenye planning moshi imepangiliwa vyema kuzidi mbeya. Mbeya haipo planed

Tuje kwenye upande wa Tanga. Kwa upande wa Infrustructure and planning Tanga ipo mbele mno zaidi ya Mbeya. Ukija viwanda Tanga ipo na viwanda vikubwa japo kuwa huko mbeya kuna wafugaji lakini kiwanda kikubwa cha maziwa kipo Tanga nk.
 
Hii point yako ya mwisho imenichekesha sana.. eti “japokua huko Mbeya kuna wafugaji lakini kiwanda kikubwa cha maziwa kipo Tanga”. 😂😂😂 dah Mbeya inachekesha sana.
 
Mkuu unazijua main source ya mapato ya mbeya na Moshi au Tanga ni zipi ?
Unajua mbeya jijini mapato makuu hayatokani na kilimo Wala ufugaji.
Issue unangalia majengo tu ila ukija kwenye economic activities mbeya Iko mbali sana , ungesema arusha au mwanza sawa ila Tanga na Moshi bado sana .
 

Mimi huko natembelea na hii kazi ya tathmini tunaifanya sana naweza kukuambia mpaka mwakani au 2026/2027 inajikadiria kiasi gani Cha mapato ila wewe utategemea kupata data za mtandaoni.
Siri moja nikupe tu mwaka karibia majiji yote yata double mapato ila Tanga haiatavuka bil 27 ila mbeya itazid hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…