Udini au ubaguzi wowote, unafanya kazi kama kuna homogeneous society yenye mgawanyiko wa wazi. Unakuta kuna kundi la pure Muslims au Christians ndani ya jamii moja, hawachangami wala kukaa chungu kimoja. Ni kama ilivyokuwa Sudan.
Kwenye jamii hizo, watu hawashirikiani katika mambo ya kijamii, kisiasa, na kiuchumi. Hawashirikiani kwenye harusi, misiba na hawana shule za pamoja n.k
Watanzania ni tofauti sana, wameoleana sana, wamesoma pamoja, wanashiriki punlic holidays pamoja n.k. 8 out of 10 ya watanzania wana ndugu au marafiki wa damu wa dini tofauti na yao, tena kuna sehemu kama usukumani huwezi juwa dini ya mtu kwa jina lake.