Yote hayo wanayajua vizuri sana, Dr. David Ndii anawaambia kila mara lakini hawasikilizi, kuna wakati aliwaambia kwamba ni vema hiyo SGR ikaishia Nairobi, kutoka Nairobi hadi Kampala, waikarabati RVR, hawamsikilizi, ndiyo sababu anakua na hasira muda na anaongoza kampeni ya kujitenga.
Kenya wakumbuke kwamba, Geographically ina bahati mbaya sana, kupakana na Somalia, South Sudan na Ethiopia, zote hizo hazina biashara ya maana, badala yake ni vita na maugomvi ya koo za mipakani, nchi pekee wanayotegemea ni Uganda, pia nchi yao Mungu hakuijalia mali asili nyingi kama Tanzania, viongozi wa Kenya walipaswa kulijua hilo na kufanya miradi ambayo uchumi unaweza kuhimili, wao wanadhani kushindana ili kuonekana wapo mbele ndiyo muhimu, ni sawa na Hiace kukimbizana na Range Rover, hata kama imetangulia umbali gani, itapitwa wakati mwenye Range wala hajui kwamba mwenye Hiace anashindana.