Kwa namna mchakato wa kupata fedha unavyokuwa mrefu serikalini ni ngumu sana kuendesha huu mradi kwa ufanisi. Ni Bora serikali iendelee na ujenzi wa miundombinu ila upande wa waendeshaji wa mabasi waweke kampuni tofauti tofauti.
Serikalini Hela kuingia ni rahisi ila kutoka ni ngumu, pili watu wa kupiga kwa pet cash... Kwa biashara ya usafirishaji unatakiwa uwe na balance cash muda wowote kwa ajili ya dharura... Huwezi kuandika pet cash kila siku sijui bolts, oils, rangi, break pads,fluids etc... utachoka..
Halafu bado upigaji upo sana maana uwajibikaji ni zero....wahasibu wanadhani wakitoa Hela ni kama wanakupa ya kutumia,sio ya kufanyia kazi... Zile gari zingekuwa zinajichanganya mtaani wangekuwa wananyonya mafuta kila siku...ila wanaiba sana engine oils na lubricant... Wananunua ila hawaweki kwenye magari...yanakufa tu yenyewe hakuna anaejali...
Kampuni binafsi wanakuwa na uchungu na gari zao, service watazingatia, uendeshaji wa tahadhari watazingatia na mambo mengine.... Ile maintenance team pale ukienda kuwakagua sidhani kama wanajua kazi yao...kila siku wana outsource mafundi nje na bado wako na kitengo Cha Ufundi... Ni upigaji tu wa kifala...
Gari ni matunzo na service kulingana na ratiba, hizo za kwao hawatunzi kabisa na ni kwa sababu usimamizi hakuna... management Haina wataalam wa mambo ya magari na usafirishaji... Kiburi na fair of insubordination inapelekea kuua mradi..
Wabinafsishe tu...wanakie kutoza Hela ya njia.