Mkuuu nashukuru umekuja hapa, je ungeyajuaje kama sio ukaguzi , mambo mengi yaliibuliwa na ofisi ya Cag na yakafika bungeni wabunge wakajadili kwa uhuru.
Sasa nambie kipindi Cha magu ilikuwaje ? Magu alikubali mijadala kuwa wazi kama enzi za kikwete? Na kama kweli alikuwa anataka kudhibiti basi angeachia hiyo miradi ijengwe kwenye taasisi husika ila angebana na kuwachukulia hatu wakosefu
Mkuu raisi hawez kuwa sehem zote na ndo maana kukawa na taasisi kama usalama wataifa, pccp, Cag na kwa wakaguzi wandani wapo karibia Kila taasisi na ripoti zao hutoka Kila mwaka.
Nambie ni ripoti gani ya Cag iliyoibuliwa kipindi Cha magu akaifanyia kazi walau hata kuwaweka lockup wahusika.
Wananchi wanampenda sababu alizuia watu wasijue uchafu kwa hiyo ikaonekana yeye ndo Bora kwa sababu hawakuwa na taarifa