Boeing CEO, Dave Calhoun na mabosi wengine watatu, wamefukuzwa kazi, hii ni baada ya whistleblower aliyefichua madudu ya kampuni hiyo kuuawa wiki jana. Nilimekuwa nikilalamika hapa kwa miaka zaidi ya miwili kuhusu ATCL kuendelea kununua hizi ndege za 737 MAX. Tena kuna watu hapa, mmoja wao akiwa ni
joto la jiwe alizitetea sana ndege hizi, akidai zimekarabatiwa.
Baadhi ya watu hawaelewi kuwa Boeing ni kampuni bomu kwa sasa. Hii ilikuwa ni kampuni nzuri sana zamani, enzi hizo wakiwa na kamsemo kao "Boeing is a company of engineers", dhana ilikuwa, "to build a good piece of engineering and they will come". Wakimaanisha kutengeneza bidhaa bora kuzingatia usalama na kila dhana ya kiuhandisi.
Mambo yalibadilika 1997 pale Boeing ilipoungana na McDonnell Douglas, kampuni iliyokuwa na dhana tofauti, yaani wao faida kwa stock holders ndo kila kitu, hata kama watatengeneza crappy products. Baada ya merging, vigogo wa McDonnell Douglas ndiyo wakawa waendesha kampuni, Boeing ikabaki jina tuu. Product ya viongozi wa McDonnell Douglas ndiyo haya majeneza yanayoelea yanayoitwa 737 MAX.
Watu wanaojielewa siku hizi hawapandi tena hizi ndege, including Boeing employees.