President of China
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 31,766
- 89,791
Tarehe 19 Februari 2024 jijini London ulifanyika uzinduzi wa 'Documentary Film' iitwayo "Footsteps: Journey to the Engare Sero footprints" inayohusu Nyayo za binadamu zenye umri wa miaka 20,000 zilizopo katika eneo la Ngare Sero katika Wilaya ya Ngorongoro Kata ya Malambo Mkoani Arusha. Nyayo hizo zilitokana na binadamu waliokuwa wakikimbia kufuatia mlipuko wa volcano katika Mlima wa Oldonyo Lengai. Filamu hiyo imeandaliwa na Mtengenezaji filamu mkongwe (Film Director) Ndugu Ndugu Leander Ward- ambaye anafahamika katika tasnia ya filamu kupitia filamu ya The Crimson Wing: Mystery of the Flamingos (2008), Wild Side (1995) and Prince Valiant (1997).