Kweli nchi itaendelea kuwepo bila kujali mtu, lakini kasi na muelekeo wa maendeleo unatokana na aina ya uongozi.
Uongozi mbovu anaweza kurudisha nyuma maendeleo na hasa unapokuwa na uongozi usio na dira. Unapobariki watu kuiba kwa urefu wa kamba zao, uongozi wa namna hiyo unatengeneza hali ya kuongezeka rushwa na wizi.
Tulikuwa tumeshasahau mgao wa umeme, lakini uongozi mbovu ukaleta watu wabovu kama Januari waliotuletea mgao. Ni biashara ngapi zimekufa kutokana na kukosa umeme? Kuna wanafunzi wangapi wameshindwa kusoma vizuri usiku kwa kukosa umeme? Ni kiasi gani cha wagonjwa hali zao zilikuwa mbaya au hata kufa kwa kukosa huduma iliyohitaji umeme?
Kama huoni umuhumu wa kiongozi bora, basi utakuwa na tatizo mahali.