Ujamaa villages, perfect illustration of DAR es Salaam living and housing.
View attachment 2686041
View attachment 2686043
Hakuna shida katika kuishi Kwa kujenga community — watu kusaidiana, kuwa na ujirani, kutembeleana, kucheza na kufurahia pamoja. Kwa karibu, kila kitu cha muhimu kipo karibu na makazi. Kanisa, shule, soko — vyote vipo karibu na nyumba. Akili yako imekuwa brainwashed kufikiri kuwa maisha mazuri ni kuishi ndani ya gate na fence na kuendesha gari kwenda sokoni, which is clearly a sad, lonely life compared to what is happening in the drawings.
Tatizo kuu kwenye hizi picha ni umasikini na miundombinu mibovu. Kama kungekuwa na paved roads, street lighting, running water and power, transit system (railway), community centers kama library basi hii ingekuwa jamii bora.
King Charles (then Prince Charles of Wales) aliona Uingereza inabadilika na kuacha tamaduni za ujenzi wa miji yenye community na principles za kila huduma muhimu kuwa karibu na maisha ya watu. Modernism iliikamata dunia nzima kuanzia miaka ya 1950s - 1960s na kufikia 1980s, shopping malls zilikuwa zinajengwa ku-replace maduka ya mitaani. Mixed-use buildings zilikuwa zinabomolewa kujenga suburbia (aka nyumba zenye fence na mageti).
Charles akaamua kuanzisha mji unaitwa Poundbury kurudisha tamaduni za ujenzi wa jamii. Ni mji ambao kila kitu unachohotaji kipo karibu yako na hautahitaji gari kufikia huduma muhimu.
Kama tungesimamia aina hii ya community building Kwa kujenga miji yenye huduma Za muhimu karibu na makazi na kuboresha miundombinu basi quality of life inge-improve. Kwa jinsi Tanzania ilivyo, kila mtu anafikiri success ni kuwa na nyumba yenye gate na kumiliki gari. Haitawezekana kuwa na miji bora kwa land use ya aina hii. Europe success ni kuishi kwenye miji yenye ACCESSIBILITY. Treni na trams na buses zinabeba watu wenye vipato vya aina zote bila kubagua. Community centers kama library zinajenga elimu kwenye jamii. Computer labs zinasaidia watu kujifunza teknolojia na kujiendeleza kielimu. Vitabu vinaongeza hekima. Parks and recreation zinakusanya watu pamoja na kuleta a sense of community. Ninaweza kuongea siku nzima kuhusu makosa yanayofanywa kwenye ujenzi wa miji. Hata miji mipya kama Dodoma bado makosa yanaendelea kufanywa. What a shame!
Some pictures of Poundbury, England
This particular picture looks a lot like the drawings you posted. The irony is Poundbury was designed by world renowned architects and urban planners.