Mkuu, kitendo Cha kuweka screenshot ni dalili kwamba kuna kitu unaficha, weka link tusome kinachoendelea.
Ukweli ni kwamba hii kesi haihusiani kabisa na DPW, hii ni "personal". Huyu dada alikua mfanyakazi wa DPW lakini inaonekana pia anahusika na mambo ya Ujenzi. DPW haijashitakiwa kama kampuni, ila huyu dada ama mtu binafsi, ndio sababu amefungwa yeye Kama yeye. Kampuni halifungwi ila linafukuzwa nchini na kulipa fidia, au kufutiwa leseni.
Mkuu, tuonyesha wapi DPW Kama kampuni limeshitakiwa na serikali au kampuni lingine kwa kitendo Cha kutoa au kupokea rushwa Ili DPW wapate kazi ktk nchi yoyote hapa duniani. Mkuu sisi ni watu wazima na wasomi, tafadhali tuonyeshe ukomavu katika mijadala yetu.