Ila jengo la abiria lenye hadhi ni muhimu zaidi kwa sasa maana kama sikosei uwanja umeongezwa urefu upo around 2100 m! Umbali wa km 50 toka KIA si mbali hivyoo kama watu wanavyojiaminisha dunia nzima viwanja vikubwa viko nje ya majiji na isitoshe barabara ile kwenda KIA inapanuliwa na pia reli ya Moshi-Arusha haipiti mbali metro rail inaweza kuanzishwa! Unless turuhusu miradi ya ki-Chato!
Mimi binafsi nadhani Tanga city inahitaji uwanja wa kisasa nayo tena ukizingatia miradi mikubwa inayokuja yaani pipeline mbili ya gesi na ya mafuta na the largest crude oil terminal in east and central Africa! Kutakuwa na safari nyingi sana toka Kampala/Hoima kuja Tanga na pia kutoka Kigali, Bujumbura na eastern DRC kwa ajili ya port! Uwanja wa KIA japokuwa upo Kilimanjaro umewekwa strategic katikati ya Moshi town na Arusha city kuhudumia hizi sehemu mbili usisahau Mererani town stone throw away inajaribu kukuzwa pia!