joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,111
- 46,621
Kama biashara Kati ya Kenya na Tanzania ilidorora kwa sababu ya Magufuli, vipi kuhusu biashara Kati ya Kenya na Uganda mbona inazidi kudorora?, au Magufuli amehamia Uganda?.Kwa hivyo hio $600 million pesa mnayopata kwa kuexport bidhaa Kenya ni takataka tu sio? Nyie hamuhitaji hio pesa kwa sababu nyie ni matajiri sana sio? Halafu wacha kusema kwamba Kenya haina umuhimu wowote kwa Tanzania. Bado trade statistics ya TZ ya 2021 haijatoka. Ikitoka nakuhakikishia kwamba Kenya itapanda kwenye jedwali hilo. Tangu Magu aingie Kenya ilianza kuteremka kwenye jedwali hilo kwa chuki na madharau aliyokuwa anatufanyia. Anyway tungoje tuone data zikitoka, Kenya lazima itapanda sana kwenye jedwali hilo, baada tu ya mwaka mmoja wa mama kushika usukani.
Ninyi wakenya ni watu wakorofi Sana, mnakorofishana na kila jirani yenu, ninyi mnahitaji watu wenye vichwa maji Kama Magufuli, hamna ustaarabu hata kidogo, mnajifanya wajuaji wa kila jambo, hovyo Sana ninyi.
Sijasema kwamba hiyo $600M tunayopata ni kitu kidogo, ninachosema ni kwamba, Kati ya Kenya na Tanzania, Kenya ndio inafaidika zaidi, kwasababu ninyi mnaokoa maisha ya wananchi wenu ambao wengi wangekufa kutokana na njaa. Hivi utalinganishaje $600M na maisha ya binadamu, kipi ni muhimu zaidi?, Viwanda vyenu vingi vitafungwa na uchumi wenu kusambaratika kabisa.
Kenya ninyi sio wastaarabu kabisa, biashara Kati ya Kenya na Uganda ilikua imesimama vizuri Sana, Mimi mwenyewe nilikua ninashangaa kwanini Uganda chini ya M7 ambaye kimsingi Tanzania ndiyo ilimuweka madarakani lakini anafanya biashara zaidi na Kenya kuliko sisi, kabla hata sijapata jibu, Kenya mkaanzisha fujo bila sababu za msingi, matokeo yake biashara Kati ya Uganda na Kenya inakaribia kufa kabisa. Wakenya lazima mjiulize na mjirekebishe, sisi tupo SADC, mkituzingua tunawaacha na kwenda SADC, ninyi zaidi ya sisi hapa Afrika, nchi gani nyingine mnayoitegemea zaidi?


