UKWELI UPO HAPA BAINA YA RUSSIA NA U.S.A
Sijui kama watu wanakumbuka tukio la Cuban missile crisis USSR la October - November 1962, Soviet katika kilele cha nguvu zake na ubabe duniani waliweka makombora (missile) Cuba, kama eneo muhimu la kueneza Ujamaa Amerika ya Kusini na Kaskazini pia, Marekani walipofahamu tu jambo hili, ukaibuka mvutano mkubwa duniani uliohatarisha vita kuu ya pili duniani, Marekani walikizunguka Kisiwa cha Cuba kwa Meli na ndege kwa mwezi mzika, na mwisho makombora hayo yaliondolewa na Russia baada ya majadiliano ya mezani kama wakubwa sio vinginevyo.
Marekani waliona ni hatari kwa usalama wao Soviet kuweka kituo chao cha Kijeshi Cuba, Tambua Cuba ilikuwa nchi huru kama Ukraine, yaani Cuba ileile ya mjamaa halisi Fedel Castro ambae alikuwa ni adui mkubwa wa Marekani hadi kufa kwake. Sasa anayeamini kuna uhuru wa nchi mbele ya Super power countries huyo bado ni mtoto duniani, akae kitako tuendelee kumfundisha kwamba uhuru unaojadiliwa na kusimuliwa ni ule wa kisiasa wa ndani tu wa vyama vya siasa na wa kuzungumza, nje ya hapo dunia ya tatu haiko huru na haitakuwa huru. Uhuru ni dhana pana sana. Haihusiani na Maslahi ya nchi kwa Marekani, Urusi na Uchina japo uchina bado hajajikomboa kufika viwango vya hawa wawili.
Sehemu ya mahojiano hiyo Jasusi huyu anarejea kwenye hoja zangu za kufafanua na kukazia, anasema;
Colonel Douglas Macgregor anasema kuwa Marekani ina nafasi ya kuepusha vita na Putin (Russia). Jambo la kwanza wanalopaswa kufanya Wamarekani ni kukiri na kukubaliana na nukta ya msingi ya Putin (Russia), ambayo serekali ya Russia imeiweka wazi kwa zaidi ya miaka 25 sasa. Nukta yenyewe ni kuwa Russia hawataki majeshi ya Marekani, mizinga ya Marekani, na majeshi ya NATO kwenye mpaka wake na Ukraine (Mashariki ya Ukraine kwenye majimbo yaliyotangazwa huru na Putin).
Colonel Douglas akaendelea kusema: Kiukweli kabisa hata sisi Wamarekani hatukuyataka majeshi ya Russia na mizinga yake ndani ya Cuba (mwaka 1962), Putin naye hataki mambo hayo mashariki mwa Ukraine. Lazima tukubali madai hayo. Tuache kujifanyisha kuwa madai hayo hayana maana (ni ya kipuuzi).
Retired US Army Col. Douglas Macgregor told "Tucker Carlson Tonight" that he was concerned President Biden didn't take Putin seriously enough.
www.foxnews.com
Sent from my SM-A025F using
JamiiForums mobile app