Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Mida jngine mnapuuzwa tu
emoji23.png
emoji23.png
View attachment 1758063View attachment 1758064View attachment 1758065
Hivi haya masufuria mliyopachika brand za watu huwa hawawezi kuwashtaki kwa defamatory prejudice? Sasa huo msufuria wa Fuso Tipper na Benz wapi na wapi?
 
Haha sasa hayo masufuria unamtambia nani? Mmepigwa mpaka mmepoteana kwenye hata nusu ya companies za mabus hazijafika tayari chali

Mmebaki kurudia masufuria yenu tu upande wa kushoto kulia nyuma mbele,

Barabara zenyewe hamna
Watusumbuaa na masufuriaaa yaoo wanaona kama ndo ndo gariiii kwao inawezekan ndio luxury huko kwaooo
 
Battle ya uzuri na wingi wa mabasi mgeipotezea tu maana tunawagaragaza. Mabasi yetu bongo ni more beautiful than yours. Pia ni mengi sana ikilinganishwa na ya kwenu. Hii ni kwa kuwa uchumi wa Tanzania umesambaa kila kona ya nchi hivyo miji ni mingi. Wingi wa miji unapelekea demand kubwa ya inter-city/upcountry transportation.

Ila; nasema ila!

Sisi wabongo tunalo somo kubwa sana la kijifunza kwenye hii battle ya mabasi. Wingi wa mabasi kutoka nje (Chinese buses) una madhara hasi kwenye sekta ndogo ya bus manufacturing/assembly.

Tuko chini sana kwenye uundaji mabasi in both terms of quality and quantity. Najua wapo producers wazuri wachache kama Dar Coach na JN Coaches ila tuwe macho na haya mabasi ya hawa rafiki zetu wa China.

Automobile assembling and manufacturing haihitaji mtaji kubwa sana bali ambition and planning. Mfano ni huyo mkali wa JFA assemblers aliyeanzisha assembling plant kwa tune ya below TZS 5bn na itagharimu 12bn mpaka kukamilika.

Hayati Reginald Mengi naye alikuwa kwenye mchakato na Foton Motors kabla ya umauti kumfika.

Kuna watu wetu kama akina Hanspaul wakiwezeshwa vizuri watatutoa kimasomaso.

Iko hivi. Viwanda vingi vya China "havizalishi" hayo mabasi bali vinafanya tu assembling. Mfano mzuri ni yale mabasi yetu ya mwendokasi. Golden Dragon kwa sehemu kubwa ni body makers. Engine zilitengenezwa na Kemix ya Marekani. Gear box na Diff zilitengenezwa Germany.

Tukiamua tunaweza. "Matatu" za Kenya hazivutii lakini ile kwamba ziko manufactured Kenya inawapa benefits nyingi ambazo ziko wazi.

Pia kwenye eneo la mini-bus tunapigwa na wajapani. Mimi nimekua kwenye biashara ya "macoaster na vi-hiece". Pale kinachofanyika ni dumping ya magari chakavu na mabovi ya Japan ambayo hayako designed kufanya kazi kwenye miundombinu kama ya kwetu.

Pia mengi kule yanafanya shughuli binafsi ila huku tunayatwisha mzigo wa commercial transportation. Hivyo yanachoka haraka.

Jana PM aliahidi kuwatembelea JN Coach tar 26. Alinikosha sana.
 
Sasa wewe ulitembea na Vi shuttle Nissan, sio bus, kuna tofauti ujue! 🤣
Ndio usafiri wenu mkuu mzee kwann ubishee😂😂😂 riftvalley shuttle mnapandia afya centre jengo la kijani 14 seater nauli 800 mpaka eldy sijui nakuru
 
Back
Top Bottom