Duh, aisee. Kwa hiyo aliyeko Ubungo yuko jijini Dar es Salaam! Ngoja tusubiri izoeleke hii kitu.
Lakini why
Geza Ulole umeniita mbumbumbu? I know where many miss the point but neno mbumbumbu, I don't think it's appropriate.
mara ya pili hii nakuelewesha ila unazidi kupotosha sasa kama huna tatizo kichwani sijui! JPM kaondoa manispaa ya jiji aka-create city authority akaipa manispaa ya Ilala hiyo kofia ili kuondoa uwepo wa manispaa isiyo na eneo la utawala kwa maana yake masuala ya jiji la Dar linaloundwa na manispaa za Ilala, Temeke, Kindondoni, Ubungo na Kigamboni yatakuwa chini ya Mkurugenzi wa Ilala ambaye pia anashughulikia masuala ya manispaa ya Ilala! Ndo kilichofanyika! Kabla ya hapo Jiji lilikuwa na Meya na madiwani wasio na majimbo/kata yaani waliokuwa hawajachaguliwa kutokana na madiwani! Sasa hivi meya atatokana na madiwani wa kutoka wilaya zote tano wanye kata aliyechaguliwa na Wananchi na akachaguliwa na madiwani wenzie kuongoza Jiji. Mbumbumu ni asiyeelewana na asiyetaka kueleweshwa!
Jiji
Utangulizi
Jiji la Dar es Salaam lipo kati ya latitudo nyuzi 6 hadi 7 na longitudo kati 39.45 kwa upande wa Mashariki na nyuzi 39 kwa upande wa magharibi, Kusini mwa ikweta na upande wa magharibi, Kusini na Kaskazini. Jiji linapakana na Mkoa wa Pwani, upande wa Mashariki linapaka na Bahari ya Hindi. Jiji la Dar es Salaam lina eneo la ukubwa wa kilomita za Mraba zipatazo 1,800; kati ya hizo, kilomita za mraba 1,350 ni eneo la nchi kavu ikijumuisha visiwa vinane vilivyopo katika eneo la bahari ya Hindi. Jiji hupata joto la wastani wa kati ya nyuzi 25 hadi 33 na mvua katika misimu miwili ya vuli ambayo ni miezi ya Oktoba Desemba na Masika ambayo huanza miezi ya Machi Mei.
Halmashauri zilizokuwepo! 👇
Idadi ya watu
Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 Jiji lina idadi ya watu 4,364,541, ambapo kati yao wanaume ni 2,125,786 na wanawake ni 2,238,755.
Historia ya Halmashauri ya Jiji
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imekuwa inaliongoza Jiji kutoka mwaka 1961 mpaka mwaka 1972, ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilizivunja Halmashauri zote nchini na kuwa chini ya Usimamizi wa Serikali Kuu (Madaraka Mikoani)
Serikali Kuu ilizirudisha Serikali za Mitaa Nchini, Chini ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) na. 8 ya mwaka 1982, ambapo Halmashauri ya Jiji ilianza kutekeleza majukumu yake ya kutoa huduma kwa wananchi kuanzia mwaka 1983.
Mwaka 1996 Serikali Kuu iliivunja Halmashauri ya Jiji na kuunda Tume ya jiji la Dar es Salaam, kwa Tangazo la serikali Na. 110 na 111 ya tarehe 28 Juni mwaka 1996.
Tume ya jiji ilifanya kazi kwa kipindi cha miaka minne, ambapo mwaka 2000 Serikali iliunda mamlaka nne za Serikali za Mitaa za Mkoa wa Dar es Salaam kwa sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Na. 8 ya Mwaka 1982, kama ilivyo rekebishwa kwa sharia na. 6 ya mwaka 1999.
Utawala
Kiutawala Jiji limegawanyika katika Halmashauri sita za Serikali za mitaa ambazo ni:
• Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
• Halmashauri ya Manispaa ya Temeke
• Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni
• Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
• Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
• Halmashauri ya Manispaa ya Kigambomi
Mstahiki Meya ni Kiongozi Mkuu na Mkurugenzi wa Jiji ni Mtendaji Mkuu kwa upande wa Serikali za Mitaa.
www.dsm.go.tz
Kujua zaidi kuhusu Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam