Nikweli kabisa Kama unavyodai...Hii kitu matajili wanaitumia Sana...Inabadili Maisha ya binadamu kwa kiasi kikubwa Sana...Mimi nilipewa Kama mitishamba....Sema Ni vyema uzingatie dozi usizidishe...Kuna ule mmea ambao ukishika majani yake yanajikunja..Mizizi yake ina content nyingi....Ila cha ajabu pia mkonge una content pia...
Ni kweli kujua dozi sahihi ni muhimu sana, haya madude yanaweza kuua mtu kutokana na tabia yake ya kuongeza mapigo ya moyo. Watu wenye matatizo ya moyo, figo na ini wanatakiwa wamshirikishe daktari kwanza.
Mimi Niliitumia ya mkonge...
Hiyo ya mkonge ni san pedro cactus?
Je walichanganya na vitu vingine au ulikunywa maji ya mkonge pekee.
Umeishia katikati .. please.. the floor ..I mean the screen is yours.
Sent from my Infinix X650 using
JamiiForums mobile app
Tupeane maarifa hapa mkuu.
Psychedelics (ayahausca, mushrooms n.k) zina kemikali zinazopatikana kiasili kutoka kwenye mimea na fungae, ambapo zikiingia mwilini (kwenye ubongo) zina "reset" connections za neurons (seli za ubongo).
Kwa makabila ya watu wa Amazoni (Amerika kusini) ambao wametumia hizi dawa kwa miaka elfu na elfu, wanaamini ukinywa dawa hizi, zinakufanya uwe "in tune with nature".
Watoto (chini ya miaka 5) wanakuwa ni wa kiasili zaidi, wana furaha, wana imagination na hawaamini katika limitations. Dawa hizi zinakurudisha utotoni.
Ubongo wa mtoto unakuwa na network kubwa ya kusafirisha taarifa, ndiyo maana mtoto anaweza kujifunza lugha yoyote ile bila shida na kama akigombana na mwenzie baada ya muda anapotezea. Hii ni kwasababu ubongo wa mtoto hauna njia maalumu ya kupitisha taarifa, njia zote zinaweza kutumika.
Kadri mtoto anavyokua, ubongo unaanza kuwa na uvivu wa kutengeneza njia mpya za kupitisha taarifa, yaani bongo unaanza kutegemea zile njia zinazofahamika. Ndiyo maana kadri mtu anavyokua inakuwa vigumu kuacha tabia zake (mbaya au nzuri).
Psychedelic inachofanya ni kuangali zile njia zinazotumika mara nyingi kupeleka taarifa fulani (mfano hamu ya kutaka kuvuta sigara) na kuziziba. Psychedelics zinaweza kujua hivi kwa kuangalia kiasi cha damu inayopita sehemu hiyo (kulinganisha na sehemu nyingine) na kupunguza ili kiasi hicho kiwe sawa na kwingine.
Kwa kuwa ubongo ni "information superhighway", taarifa lazima ziende kutoka sehemu moja hadi nyingine. Na baada ya sehemu moja kuzuiwa na psychedelics, ubongo hutafuta njia mpya (ambayo zilikuwepo lakini hazitumiki) na kupitisha taarifa hapo. Muda mwingine zile taarifa (hamu ya kuvuta sigara) zikiwashwa zitapitia njia nyingine kabisa na hivyo kuufanya ubongo kuongeza network kuubwa ya kupitisha taarifa na kusababisha mtu kuacha addiction kabisa.
Kwahiyo baada ya kumaliza "trip" (kulewa), ubongo unakuwa "reset" kwa kujenga neuro pathways nyingi. Mtu anakuwa hana tena stress na worries. Na effect ya mimea hii (psychedelics) ni tofauti na ya drugs kama adderall, caffeine au hata cannabidiol (bangi) ambapo baada ya ingredients kuisha mwilini, mtu anarudia hali ile ile aliyokuwa nayo mwanzo.