ATCL wapo makini sana katika kufungua njia mpya, Magufuli alishawaambia kwamba hataki kusikia kitu hasara kinatokea tena ATCL. Katika akili ya biashara, ni kosa kubwa kuanza na njia ambazo kuna competition kali, njia ya Nairobi, Ethiopia, Qatar, Instambul Uturuki, hizo njia sio za kuanza nazo kama ndege zako ni chache, lazima uwe na ndege za kutosha kuingia katika hizo njia.
ATCL itafanya kosa kubwa sana kuanza route ya Nairobi bila kujiimarisha kwa idadi ya ndege na logistics zingine, vinginevyo lazima watapata hasara kama inavyopata hasara Rwandair na KQ.