mara huyu anamwagiwa tindikali, yule nyumba yaungua karatasi inapona, huku katibu anasema kuna magaidi anawajua lakini polisi haiwajui, na huyu naye anapanda na siraha jukwaa la siasa kana kwamba ni vitan, mpaka kuisha kampen hizi tutasikia na kuona mengi pengine kuliko kampen zozote zile.
Jamii za kisomali kama hizi zitatuletea matatizo sana hapa tz,maana wameshindwa kuishi kwao somalia,sasa wanataka kuleta instability huku kwetu,
huyu nae hashindwi kuleta mercenaries kutoka hapo somalia
Mkuu tayari waSomali wapo kibao Tanzania wamefanikiwa kuingiza fedha za uharamia [utekaji meli ipo thread hapa jamvini] kwenye uchumi wetu faida na hasara wanauchumi wanazijua lakini kisiasa tukilala hakika uchaguzi wa mwaka 2015 tutawashuhudia zaidi ya wasomali kumi mjengoni.Zipo jitihada za kuijumuisha Somalia kwenye EAC bila kujali hali ya ulinzi na usalama siku wakifanikiwa tutegemee instability ndani ya jumuiya.
Rage kafanikiwa kupenya ndani ya mifumo yetu ya uongozi kwakuwa iko weak sana majambazi wakiwa na fedha wanaingia halafu tuanategemea maendeleo.
View attachment 37697Source hiyo mwananchi ya leo
Hofu yangu mimi ni jinsi alivyoivaa kishamba namna ile kiasi kwamba unampiga ngwala kidogo tu unamnyang'anya na kuleta madhara makubwa kwenye watu wengi namna ile. Watoa leseni za kumiliki silaha toeni na mafunzo pia. JKT na mafunzo ya mgambo vimekufa.Hayo mambo ya kupanda na Bastola jukwaani yangefanywa na kiongozi au mbunge wa CHADEMA wangewaambia wananchi kuwa oneni jinsi vyama vya upinzani vinavyotaka kuvunja amani nchini. Kwa kweli wangeongea mengi hadi povu lingewatoka, Sasa wamefanya wao ngoja tuone wataongea nini katika hili.
Mkuu kama kwenye kitabu cha animal farm." All animals are equal but some are more equal than others"
Hayo maswali ni sawa kabisa, lakini kwa kufikiri kwa haraka haraka, NI KOSA ISIPOKUWA KWA WATU WA VYOMBO VYA ULINZI WANAPOKUWA KAZINI.Kabla ya kumshambulia Rage tungepaswa kwanza kufahamu sheria za umuliki wa silaha hapa Tanzania. Kwa mfano:Tukishazijua sheria za umiliki wa silaha tutakuwa na uwezo mzuri sana wa kuchangia hii mada. Naomba wataalm wa sheria watujuze zaidi.
- Je mtu anaruhusiwa kutembea na silaha anayoimiliki kihalali?
- Je ni makosa kuonesha silaha unayoimiliki kihalali hadharani?
As for me, sizijui hizo sheria ndio maana siwezi kusema kama Rage ana makosa au hapana.