Wana JF:
Naamini tulio wengi tumeona picha kubwa katika gazeti la mwananchi leo 23/9/2011 ikimuonesha mbunge wa Tabora mjini (ccm) Ismail Aden Rage akipanda jukwaani na bastola kiunoni. Ni ishara ya shari.
Lakini kwa upande mwingine katibu mkuu wa ccm, Mkama kaja na suala la ugaidi. Anadai CDM wamepeleka makomandoo waliopata mafunzo Libya na Afghanstan kwa ajili ya kufanya fujo igunga. Hii ni kauli nzito, si ya kuipuuza kwani imebeba dhamira hatari kwa usalama wa taifa letu. Japo Polisi wamekana kupewa vielelezo, nadhani iko haja ya vyombo vya usalama kuchukua hatua zaidi.
Binafsi napata hisia, zinazochochewa na vitendo vya ccm, kuwa chama chao kiko tayari kuivuruga amani ya nchi ili kulinda utawala wake. Sitashangaa wakileta makombora na mizinga siku chache kabla ya uchaguzi wa igunga tayari kuanzisha vita na watu wa igunga.
Watu wa Zambia wameonesha mfano, watanzania tusitishwe na propaganda za ccm wala tusikubali kugawanywa kwa misingi ya dini.
"Tukiamua kumuua panya kwa sumu, lazima tuwe tayari kunusa harufu ya mzoga wake kwani ni ya kitambo kidogo tu".