Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,309
- 18,490
Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) amewaomba wananchi na wanachama wa CCM kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi la upigaji wa kura Oktoba 29, 2025 ili kukiwezesha chama hicho kupata ushindi wa heshima na wa kishindo.
Dkt. Samia ameyasema hayo Septemba 10, 2025 wakati akizungumza na maelfu ya wananchi wakati wa kampeni za chama hicho wilayani Igunga mkoani Tabora, akiahidi pia kuendelea kuwatumikia kwa juhudi zaidi katika kuwaletea maendeleo.
"Mtakapokuja na ushindi wa heshima kwa jina jingine ushindi wa kishindo wa Chama Cha Mapinduzi tutaweza kuziba midomo wale wengine lakini la pili inapendeza sana kuona wananchi mnajaa sana kwenye viwanja vya mikutano namna hii, sasa idadi iende ikajionesshe kwenye masanduku ya kura vinginevyo wenzetu watatucheka".