Bastola iliyoua wawili Sinza ni dili kishirikina, lakini pengine pia imebeba mikosi na laana

Mshana, ungefanya pia jambo jema mwishoni kwa kuweka tahadhari pia kua: anayeona kuwa post haimfai na haamini katika haya basi apite salama na asijisumbue hata ku-comment!!
BabaDesi bado haisaidii hata kama ningeweka mwanzoni mwa mada katikati na mwishoni
Kikubwa cha kufanya ni kujaribu tu tena na tena kuwaelimisha kwa upole na busara kwakuwa natambua sio kosa lao bali ni uelewa finyu juu ya haya mambo
 
Mkuu Mshana Jr silaha si ni object inakuwa vipi na bahati?
Yeah object ni yabisi.. Yabisi kiroho zinabeba bahati na laana pia
Waulize wafanyabiashara wa magari utakuta kuna baadhi ya gari anazipenda sana kwakuwa hazimsumbui kwa ajali, vipuli wala madereva
Wawindaji nao hivyohivyo kuna silaha hazilali njaa
Hata ardhi pia kuna vipande hutoa mazao mengi nknk
 
Alikuwepo jamaa alionesha kitambulisho,huyo angekuwa kwetu Risasi ya kwanza ya pili angepigwa kama Kuku.
Muda huu angekuwa anasimulia ndugu zake yaliyomkuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…