Bastola iliyoua wawili Sinza ni dili kishirikina, lakini pengine pia imebeba mikosi na laana

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,791
Silaha tajwa tayari imeshaondoka na roho mbili na tayari iko mikononi mwa jeshi la polisi.. Haijajulikana kama mmiliki alinunua 'used' au brand new!
Kama kanunua mtumba ni kwamba hapo kabla ilishawahi kutumika mostly ilishauwa.. Wangapi? Haijulikani..labda mpaka kupata historia yake..! Kama kanunua mpya na yeye ndio mtumiaji wa kwanza basi kama sio silaha yenyewe basi pesa iliyotumika haikuwa na baraka.. Ilikuwa na mazonge..Na tayari silaha husika imeshaingia kwenye ulimwengu hasi
Kimsingi hakuna kesi tena ...! Muuaji naye kajimaliza.. Jalada litafunguliwa kisha baada ya muda litafungwa! Hakuna mshtakiwa...kidhibiti kinaweza kuwa huru na kuingizwa kwenye mirathi ama vinginevyo
Kama kitaingizwa kwenye mirathi kitakuja kuuzwa kama mali za marehemu .. Silaha hairithishwi.. Mnunuzi anaweza kutafutwa na ndugu na itauzwa kupitia jeshi la polisi na kitakachopatikana atakabidhiwa msimamizi wa mirathi

Silaha iliyoondoa uhai wa mtu hasa at close range ni dili sana kwa majambazi na wezi wanaotumia silaha kupora ama wauaji wa kukodishwa! Hiyo tayari ina damu kubwa hivyo kafara lake ni rahisi.. Silaha iliyouwa maranyingi zaidi kishirikina ina thamani kubwa zaidi kuliko ile ambayo haijawahi kuondoka na roho hata moja! Hivyo hii silaha ya Sinza inaweza kuwindwa na watu wabaya...!

Kwa upande mwingine ile silaha inawezekana kabida ina nuksi, laana ama imebeba maagano mabaya hasa kama ilikuwa mtumba...! Kuna vitu ni mali ya kuzimu na kazi yake ni kuharibu na kuumiza tuu..Ndio maana kuna watu hawapendi kabisa kununua vitu mtumba..vingi vimebeba nuksi laana na maagano kama nilivyosema hapo juu..!

Tukio limeshatokea na kuzua mijadala mingi mitandaoni.. Pengine kuna watu watawajibishwa hasa kama utaratibu wa kummilikisha mhusika silaha haukufuatwa inavyotakikana
Niandikapo haya kuna familia mbili ziko kwenye msiba mzito.. Wa kuondokewa na baba, kaka mume nknk.. Tayari kuna maisha mapya wanaenda kuyaanza bila mhimili wa familia.. Ni hali ngumu sana..
Haya yote yatasahaulika baada ya muda.. Na itafika mahali kama silaha husika haitateketezwa na jeshi la polisi basi itaingizwa kwenye mirathi na kuuzwa kwa mwingine...

Kuna maroho na mapepo ya kuzimu yapo duniani kuharibu na kutesa na hujipenyeza kwenye vitu na watu... Haya mavitu ya mtumba tunayotumia hatujui huko nyuma yalipitia mikono gani na yalinenewa nini.. Kuna baadhi vimebeba mapepo mapepo na maroho mabaya
Kuna baadhi vimelaaniwa na wamiliki wa kwanza au wa pili nk
Kuna baadhi vimenenewa vibaya
Kuna baadhi vimetumika kwenye madhabahu za kishirikina
Jitahidi unapopata kitu cha mtumba kitakase kwa imani yako

Nimeandika mada hii kwa mtazamo wa kiroho.. Wanaoona ni tukio la kawaida wasione ni kituko kuwaza tofauti na wao..!

View attachment 1858067
 
Nimeelewa ndio maana nikauliza.

Kwani silaha zilizoondoa roho za watu ni hiyo tu?
Kuna silaha unakuta imeua zaidi ya watu 20 lakini haihusishwi na mambo ya kishirikina. Kwanini iwe hii tu?
Silaha hii nimeitumia kama kiwakilishi tu cha kuelezea tafsiri za kiroho kwenye matukio kama hayo.. Na zaidi nimeandika mengi nje ya hiyo silaha naona hukuyaona, hukuyazingatia au hukuyaelewa
 
Silaha hii nimeitumia kama kiwakilishi tu cha kuelezea tafsiri za kiroho kwenye matukio kama hayo.. Na zaidi nimeandika mengi nje ya hiyo silaha naona hukuyaona, hukuyazingatia au hukuyaelewa
Brother hii sio poa bwana, yani watu walewe wauane wewe uje uhusishe na ushirikina kweli?

Itafika mahali sasa hata ukipaliwa na maji utasema ni ushirikina... Penye wengi pana mengi.
Uwingi wa watu duniani lazima kuwe na matukio ya tofautitofauti ya vurugu, furaha na mengine mengi
 
Mleta mada umeandika vyema kabisa.

Kuna mambo hata kama mtu haamini lakini hawezi kukwepa madhara ya kile asichokiamini.

Ulimwengu huu una kanuni zake.
Tuliwahi kununua bastola pale Obay na raia mmoja wa nje.. Shida tulizopata na ile silaha sitakaa nizisahau....kuja kupata historia yake ya kweli niliogopa na kutishika mno...
 
Brother hii sio poa bwana, yani watu walewe wauane wewe uje uhusishe na ushirikina kweli?

Itafika mahali sasa hata ukipaliwa na maji utasema ni ushirikina... Penye wengi pana mengi.
Uwingi wa watu duniani lazima kuwe na matukio ya tofautitofauti ya vurugu, furaha na mengine mengi
Ndio maana nikasema hukusoma na kuelewa nilichoandika... Mwisho wa mada nilimalizia na kifungu hiki

Nimeandika mada hii kwa mtazamo wa kiroho.. Wanaoona ni tukio la kawaida wasione ni kituko kuwaza tofauti na wao..!
 
Back
Top Bottom