DOKEZO Tuwe makini na Mawakala wanaouza dada zetu wakidai wanawapeleka Uarabuni, Serikali iangalie

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kuna tukio limetokea kwenye familia yetu hivi karibuni (Februari hii 2024), baada ya kufikiria nikaona ni vema nishee na watu ili pengine inaweza kuwa sehemu ya kuiamsha Serikali na Jamii kwa jumla juu ya kinachoendelea baadhi ya maeneo nchini.

Dada yangu ni binamu hapa tumpe jina la “Bi Dada” mkazi wa Tabora alipata dili la kwenda Uarabuni kufanya kazi za ndani, kwa maelezo yake anasema alikubali dili hilo kwa kuwa lilikuja kupitia kwa mumewe.

Mumewe naye nilipozungumza naye alisema kuna Mwanamke mmoja wa hapohapo Tabora ndio alimpa huo mchongo na kumwambia kuwa mkewe akienda Urabuni atapata fedha nyingi.

Ku-make long story short, Bi Dada akapewa nauli na huyo Mwanamke wa Tabora (Wakala Namba 1) aliyetoa mchongo kwenda Dar es Salaam, lengo likiwa ni kufanyiwa mpango wa passport.

Mchongo ukafanyika wakati wa kuelekea Uhamiaji, wale wahusika wenye mchongo wakajitokeza wengine wawili, mmoja akidai yupo Zanzibar (Wakala Namba 2) na mwingine Mwanaume yupo Dar, wakamwambia Bi Dada akifika Uhamiaji aseme anaenda Kenya kwa mpenzi wake na sio Uarabuni.

Pia Bi Dada akajulishwa kuwa mchongo wa passport ukikamilika ataenda kupandia ndege Zanzibar na sio Dar kama alivyoambiwa awali.

Bi Dada anadai aliahidiwa kulipwa mshahara wa Shilingi 600,000 (laki sita kwa mwezi), kwa kuwa maisha yake ni ya kuungaunga akakubali lakini alivyoona wahusika wenyewe hawaeleweki mara wanamfundisha adanganye Uhamiaji, mara anaenda kupandia ndege Zanzibar, mara anaambiwa anaenda Kenya, akahisi kuna kitu.

Akaamua kushirikisha ndugu wengine ndipo wakagomea mchongo na dili likabuma.

Anadai kwa sasa mawakala hao wanouza watu wamekuwa wakimsumbua wakidai wanataka hela zao kwa kuwa wametumia gharama kubwa kumtoa Tabora hadi Dar pamoja na fedha za kuhonga maafisa wa Uhamiaji ili kukamilisha mchongo wa Passport.

Hicho ndicho inachoendelea, hivyo natoa wito jamani licha ya umasikini wetu tuwe makini, hatujui hao watu wanawapeleka wapi dada zetu au ndugu zetu wengine wanaochukuliwa, kwa kuwa kila siku tunasikia stori mbalimbali kuhusu wanaoenda nje ya nchini hasa Uarabuni kinyemela.

Nipo tayari kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi na mamlaka nyingine zinazoweza kuingilia suala hili na kukomesha watu hawa, kwani namba ya Wakala wa kwanza wa kuuz awatu ambaye makazi yake yapo Tabora ni hii 0699 302*** wakala wa pili ambaye alijitambulisha yupo Zanzibar 0689 092***.
 
Waziri wa habari yupo hapo kudili na mitandao peke yake, kwa nini asidili na huu uhuni sasa?
 
we Nawe ni mshamba tu, kama hujui unatulia ,watu wamejaa huko na wanapita hapohapo AIRPORT, hupati passport ukishasema unaenda uarabuni,hasa Oman, huyo aliyekuwa anashughurikia ni mgeni wa hizo mishe, wabobezi wanawatu wao kila idara
 
Back
Top Bottom