Mkuu Invi..... Asante kwa taarifa manake tunalingojea kwa uchu mkubwa sana.... Lets wait and see!!
Taarifa kutoka Dodoma zinasema Baraza jipya la mawaziri litatangazwa muda wowote KESHO na si leo kama ilivyotarajiwa.
Ni hayo tu... Just for your information.
Invisible
Inaelekea kazi ya panga pangua imekuwa ngumu kutokana na kuwa rais anatakiwa kuhakikisha hawapi nafasi tena wanao-hisiwa (ama kutambulika kwake) kuhusika na ufisadi wa aina yoyote. Kumbuka ripoti ya BoT anayo na anawajua wahusika kadhaa wanaoguswa nayo.
Ni mawazo tu
Baraza la Mawaziri limekuwa gumzo hasa; nasikia JK anafanya mawasiliano na Wapinzani kuwa ndani ya Baraza, sijui ni za kweli soma Tanzania Daima ya leo.
Hii kweli Invisible?
au umeamua tu kuturusha roho ndugu yangu?
Kama itakuwa kweli mbona sasa kazi hiyo?
Ndo taarifa nilizopewa na 'mwandishi wetu' aliye Dodoma. Inashangaza RTD nasikia wao wanadai 'taarifa za baraza jipya la mawaziri zitawajia pindi tukipata mawasiliano na Dodoma'.
Ingependeza mheshimiwa Rais angeweka pembeni tofauti na akaangalia ndani ya wapinzani wale wanaotufaa kuwa mawaziri na akawapa fursa ya kuwatumikia watanzania. Huo ndio uzalendo! Siamini kama wapinzani hawawezi...
Ni fursa nzuri sana kwa JK kurekebisha makosa
Inaweza kuwa tactics za kuwaziba mdomo wabunge machachari.
Inaweza pia kutoa access zaidi kwa wapinzani katika machinery ya serikali.
Inaweza kuwa speculations za magazeti, but isn't Tanzania Daima supposed to be a reputable source?
Hapana invisible, sidhani kama chama tawala kimeishiwa watu hadi kufikia kuhitaji kukopa kutoka kwa wapinzani! Naamini CCM inao watu wa kutosha na waadilifu wa kupewa hizo nafasi za uwaziri. Wapinzani waendelee kufanya bidii, na siku moja inshaallah watashinda nao wataunda serikali yao. Mazingira ya sasa hivi hayatoi sababu yoyote ya kuunda serikali ya mseto, CCM ni chama tawala na kina asilimia kubwa sana ya wabunge. Upinzani ndio minority Bungeni. Sasa kama Rais atachukua tena hao minority awape uwaziri, atakuwa amezidi kufifisha upinzani. Awaache wapinzani waendelee kuisahihisha na kuikosoa serikali bungeni.
Baraza la Mawaziri limekuwa gumzo hasa; nasikia JK anafanya mawasiliano na Wapinzani kuwa ndani ya Baraza, sijui ni za kweli soma Tanzania Daima ya leo.
Mheshimiwa hii sentensi yako inanishangaza sana. Ina maana JK alivyoteua Kabwe kwenye kamati ya madini ina maana CCM ilikuwa imeishiwa watu? Sidhani kama ni busara kuona kuwa watu kutoka CCM peke yao ndio wanaweza kufanya kazi kwenye serikali. Kwa maana nyingine unataka kama opposition wakishinda CCM wote waondolewe kwenye nyadhifa zao, hizi sio siasa njema, hizo ndio siasa za kale. Kama kweli JK akiingiza wawili au watatu opposition itakuwa precedence moja nzuri sana, na strategically ni hatua nzuri!