Baraza jipya la Mawaziri kujulikana Feb 12 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza jipya la Mawaziri kujulikana Feb 12

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Invisible, Feb 11, 2008.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Feb 11, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Taarifa kutoka Dodoma zinasema Baraza jipya la mawaziri litatangazwa muda wowote KESHO na si leo kama ilivyotarajiwa.

  Ni hayo tu... Just for your information.

  Invisible
   
 2. M

  Morani75 JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2008
  Joined: Mar 1, 2007
  Messages: 619
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu Invi..... Asante kwa taarifa manake tunalingojea kwa uchu mkubwa sana.... Lets wait and see!!
   
 3. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #3
  Feb 11, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Inaelekea kazi ya panga pangua imekuwa ngumu kutokana na kuwa rais anatakiwa kuhakikisha hawapi nafasi tena wanao-hisiwa (ama kutambulika kwake) kuhusika na ufisadi wa aina yoyote. Kumbuka ripoti ya BoT anayo na anawajua wahusika kadhaa wanaoguswa nayo.

  Ni mawazo tu
   
 4. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hii kweli Invisible?
  au umeamua tu kuturusha roho ndugu yangu?
  Kama itakuwa kweli mbona sasa kazi hiyo?
   
 5. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2008
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145

  Kazi ipo...

  Hili baraza tumelisubiria kwa hamu sana leo, anway Subira yavuta kheri... tutaendelea kusubiri.

  thanx for info mkuu
   
 6. m

  mwana siasa Senior Member

  #6
  Feb 11, 2008
  Joined: Aug 28, 2007
  Messages: 119
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  inahisi sasa hapa ndo kuna kukata majina na kuingiza majina mapya
  ,mana why ipelekwe kesho?kuna siri kubwa imefichika behind,ambayo wakubwa wenyewe ndo wanaijua siri hiyo.
   
 7. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2008
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,223
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Possibly,
  Unajua Wadanganyika wamekuwa wakilalamika na kuonya kwamba hawawataki barazani wale wote ambao wametajwa na tume. Hopefully hatutasikia jina la yoyote ambaye kaguswa katika tume zote zilizo kazini muda huu. Huenda hii ndio inayompa maumivu ya kichwa mkuu wa kaya, kwani wengine ni watendaji wazuri lakini tume zimewataja!
  Tusubiri tuone.
   
 8. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #8
  Feb 11, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Waliweka captions to that effect on TVT.

  Mara zote watu makini wanapofanya kazi, ukiulizwa ETA lazima utoe muda utakaokupa the high end of the estimated timeframe.

  Sasa kama administration hii tulivyozoea, wamesema watatoa baraza Jumatatu, creating false expectations kwa watu only to dissapoint.Kulikuwa na ulazima wa kuahidi baraza Jumatatu? Hii kazi ya kupanga timu siyo ndogo, ningeweza kuwapa a few days wamalize hilo.

  Next time wawe makini kuto create false expectations.I don't care much if it takes a day or three, lakini najua kuna mijitu presha inapanda by the hour huko.
   
 9. U

  Ufunuo wa Yohana JF-Expert Member

  #9
  Feb 11, 2008
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 317
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 35
  Baraza la Mawaziri limekuwa gumzo hasa; nasikia JK anafanya mawasiliano na Wapinzani kuwa ndani ya Baraza, sijui ni za kweli soma Tanzania Daima ya leo.
   
 10. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #10
  Feb 11, 2008
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,223
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama atawaingiza wapinzani barazani, huo utakuwa mseto sasa! Kama kuna mawasiliano anafanya na wapinzani, nadhani itakuwa ni kuomba ushauri wa "Watu gani wasio na mawaa mnaona wanafaa kuwa barazani?" Sidhani kama ni vinginevyo!
   
 11. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #11
  Feb 11, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Ndo taarifa nilizopewa na 'mwandishi wetu' aliye Dodoma. Inashangaza RTD nasikia wao wanadai 'taarifa za baraza jipya la mawaziri zitawajia pindi tukipata mawasiliano na Dodoma'.

  Ingependeza mheshimiwa Rais angeweka pembeni tofauti na akaangalia ndani ya wapinzani wale wanaotufaa kuwa mawaziri na akawapa fursa ya kuwatumikia watanzania. Huo ndio uzalendo! Siamini kama wapinzani hawawezi...

  Ni fursa nzuri sana kwa JK kurekebisha makosa
   
 12. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #12
  Feb 11, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Hapana invisible, sidhani kama chama tawala kimeishiwa watu hadi kufikia kuhitaji kukopa kutoka kwa wapinzani! Naamini CCM inao watu wa kutosha na waadilifu wa kupewa hizo nafasi za uwaziri. Wapinzani waendelee kufanya bidii, na siku moja inshaallah watashinda nao wataunda serikali yao. Mazingira ya sasa hivi hayatoi sababu yoyote ya kuunda serikali ya mseto, CCM ni chama tawala na kina asilimia kubwa sana ya wabunge. Upinzani ndio minority Bungeni. Sasa kama Rais atachukua tena hao minority awape uwaziri, atakuwa amezidi kufifisha upinzani. Awaache wapinzani waendelee kuisahihisha na kuikosoa serikali bungeni.
   
 13. C

  Chuma JF-Expert Member

  #13
  Feb 11, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Invisible na wengine...JK hana muda kushauriana na Wapinzani...hii ni kutokana na Jeuri ya CCM. kushauriana na Upinzani as if CC ya CCM haipo. Pia hio itahitaji baadhi ya vitu vya kikatiba..sina hakika kama katiba ya sasa inaruhusu au La..pengine CCM watakuja na kusema MSETO haukuwa ktk SERA zao.

  Pia Kama JK angekuwa na dhamira ya Kweli ya MSETO angeeza na ZNZ ambapo kuna sababu LUKUKI za kufanya mseto kule, lkn JEURI, UFISADI na mengineyo mnayoyajua ndio yamefanya tufike hapa tulipo. Baadhi ya wana CCM wao wanaona ushindi kuwashinda UPINZANI na si ROHO ZA WANANCHI wa Tanzania.
   
 14. M

  Middle JF-Expert Member

  #14
  Feb 11, 2008
  Joined: Feb 7, 2007
  Messages: 243
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  he he he heeee
  wameshindwa kuunda Zanzibar ao CCM wataweza Bara?
   
 15. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #15
  Feb 11, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Inaweza kuwa tactics za kuwaziba mdomo wabunge machachari.

  Inaweza pia kutoa access zaidi kwa wapinzani katika machinery ya serikali.

  Inaweza kuwa speculations za magazeti, but isn't Tanzania Daima supposed to be a reputable source?
   
 16. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #16
  Feb 11, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Namna bora ya wapinzani kuwa katika serikali ni kushinda uchaguzi, si kusubiri "kuzawadiwa" mseto, maana hiyo haitakuwa tofauti na ufisadi. Wakishazawadiwa huo mseto wapinzani wote watageuka "midebwedo"!
   
 17. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #17
  Feb 11, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Mheshimiwa hii sentensi yako inanishangaza sana. Ina maana JK alivyoteua Kabwe kwenye kamati ya madini ina maana CCM ilikuwa imeishiwa watu? Sidhani kama ni busara kuona kuwa watu kutoka CCM peke yao ndio wanaweza kufanya kazi kwenye serikali. Kwa maana nyingine unataka kama opposition wakishinda CCM wote waondolewe kwenye nyadhifa zao, hizi sio siasa njema, hizo ndio siasa za kale. Kama kweli JK akiingiza wawili au watatu opposition itakuwa precedence moja nzuri sana, na strategically ni hatua nzuri!
   
 18. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #18
  Feb 11, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  RTD ndo wamepata taarifa sasa na wame-confirm kuwa Baraza jipya litatangazwa KESHO na SAA YOYOTE na si leo kama ilivyotarajiwa.

  Hivi kukiwa na waziri toka Upinzani itakuwa ni kuufifisha upinzani mkuu Kithuku? Hilo sikujua, ila 'kwa fikra zangu' nilionelea kwakuwa hawa nao ni watanzania na wapo tunaokiri wenyewe kuwa wanafaa basi haina budi wapewe majukumu ambayo ni wazi wanaweza kuyabeba katika kulipeleka Taifa tunakotaka.

  Aidha binafsi naona ni fursa nzuri kwa JK kuwaweka kando wale aliokuwa akitanabaisha waziwazi kuwa wanamwangusha (japo bila kuwataja) na awaadhibu kwa kuwanyima u-waziri. Akifanya kweli basi watanzania watarejesha imani yao iliyoanza kupotea tokana na ugumu wa maisha ulosababishwa na mafisadi wachache (kama alivyosema Mama Malecela hawazidi 20 hivi).

  Tanzania yenye neema bado inawezekana! Ufanisi ama kuanguka kwa Tanzania kwa sasa kuko mikononi mwa JK na wasaidizi wake atakaotuletea kesho.

  Mungu ibariki Tanzania
   
 19. S

  Semanao JF-Expert Member

  #19
  Feb 11, 2008
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 208
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  So itakuwa kama serikali ya Kibaki. But, hata kama akiwaingiza wapinzani sitegemi wakapewa wizara nyeti sana sana watapewa wizara ya Afrika mashariki au utamaduni,michezo na vichekesho
   
 20. a

  africanus New Member

  #20
  Feb 11, 2008
  Joined: Feb 8, 2008
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kazi hiyo sio ndogo kutokana na CV za baadhi ya wanaotarajiwa kuchafuka, hivyo umakini mkubwa unahitajika. Ole wao watakaokimbilia Bagamoyo!!!!! Na kwa sera za CCM wapinzani kuwepo kwenye baraza si rahisi.
   
Loading...