Game Theory
Platinum Member
- Sep 5, 2006
- 8,545
- 835
Mzee Game
No country for oldmen, nadhani hiyo movie Mzee Kingunge ataipenda sana!
Ni kweli kabisa maaana hata mimi nilipoona Ardhi niliogopa sana MAGUFULI pekee ndo anapopaweza.... sasa nyamagana imeshauzwa
Watanzania bwana !!!!!!!!!!!!.
Wakati wa kipindi cha Mkapa, Magufuli alikuwa wizara ya Ujenzi. JK alipomchagua kuwa wizara ya Ardhi watu walilalamika kuwa angebaki ujenzi. Alipofika wizara ya ardhi na kuonyesha uwezo wake, watu hamtaki aondoke na kwenda wizara nyingine. Kinachotakiwa ni kila mtu katika nafasi yake afanye juhudi za kufanya kazi kama Magufuli.
Msolla ni Prof wa Kilimo..asipoweza kutumia akili yake hapo sasa basi sijui watanzania tumfanye nini..!!
Msolwa Yupo, Waziri kamili wa Kilimo na chakula
kweli wabunge wa ccm hamna kitu....kiasi cha kuwa JK anapata tabu ya kuchagua watendaji na anatufanyia recycle za pale kwa pale kila siku
Aaaahhh aaaahhaa aaaahhhaa. Sometime Mh. Kikwete anatakiwa awe serious. Sasa kumrudisha mtu kama Chenge kwenye baraza hilo ina maana hakukuwa na watu wengine ambao wana-fit hiyo nafasi? Si huyu ametajwa kwenye baadhi ya scandal tena anarudi. Aliwahi kumtishia Mh. Slaa kuwa angekwenda mahakamani kwa kumzulia ufisadi na hadi mwaka kesho hataenda kufungua hayo mashitaka. Hapa kuna kitu JK anajaribu kufunika au..........??? Au ndiyo fadhila yenyewe ya SISIEM.
U know what, ngoma mdundo..... Tutaendelea kuwaumbua tu na ufisadi wao. Naamini kama JK hataki kumuweka kando huyo Chenge basi JF kwa kushirikiana na wenye uchungu na nchi watamuondoa kama walivyoondoka wenzake. Eti Nchimbi naibu wa Wizara ya Ulinzi, mmmh ndo fadhila hizo JK hakuna anayeshangaa lakini angalia sana Mheshimiwa sana maana mabomu yatazidi kuja. Ukiendekeza ushikaji mwaka 2010 utauona mgumu sana. Yaani muundo huo wa baraza pamoja na kutafakari kwa zaidi ya masaa 48 still wizara ya kilimo hukuweka naibu bila kuzingatia kuwa hiyo vilevile ni wizara nyeti especially kwa nchi yetu. Mmmh labda kutakuwa na mabadiliko mengine hivi karibuni, WHO KNOWS!!
Msolwa kwani yupo?
Kwni hajapigwa chini?
Ni kweli kabisa maaana hata mimi nilipoona Ardhi niliogopa sana MAGUFULI pekee ndo anapopaweza.... sasa nyamagana imeshauzwa
Ifuatayo ndiyo orodha sahihi ya Baraza la Mawaziri na Majina Sahihi ya Wizara zao.
BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI NI:
1. WAZIRI OFISI YA RAIS (UTAWALA BORA SOFIA) - Sophia SIMBA
2. WAZIRI OFISI YA RAIS (MENEJIMENTI YA UMMA) HAWA GHASIA
3. WIZARA OFISI YA MAKAMU WA RAIS (SHUGHULI ZA MUUNGANO) MOHAMED SEIF KHATIB
4. WIZARA YA UTALII NA MAZINGIRA DK. BATILDA BURIANI
5. WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA NA URATIBU WA BUNGE) WAZIRI PHILIP MARMO
6. WIZARA YA TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA WAZIRI STEVEN WASSIRA NAIBU SELINA KOMBANI
7. WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO WAZIRI MUSTAFA MKURO NA
MANAIBU NI JEREMIH SUMARI NA OMARI YUSUF MZEE
8. WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII WAZIRI PROFESA DAVID MWAKYUSA NAIBU NI AISHA KIGODA
9. WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI WAZIRI JOHN CHILIGATI
10. ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI WAZIRI PROFESA JUMANNE MAGHEMBE NAIBU GAUDENSIA KABAKA NA MWANTUMU MAHIZA
11. WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA WAZIRI SHUKURU KAWAMBWA NAIBU NI DK. MAUA DAFTARI
12. WIZARA YA MIUNDO MBINU WAZIRI ANDREW CHENGE NAIBU DK. MAKONGORO MAHANGA
13. WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO WAZIRI KAPT. GEORGE MKUCHIKA NAIBU JOEL BENDERA
14. WIZARA YA KAZI, AJIRA NA MAENDELEO YA VIJANA WAZIRI PROFESA JUMA KAPUYA NAIBU HEZEKIA CHIBULUNJE
15. WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI WAZIRI PROFESA MARK MWANDOSYA NAIBU ENG. CHRISTOPHER CHIZA
16. WIZARA YA KILIMO NA CHAKULA, USHIRIKA WAZIRI PROF. PETER MSOLLA, NAIBU DR. MATHAYO DAVID MATHAYO
17. WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO WAZIRI MARGARETH SITTA NAIBU NI DR. LUCY NKYA
18. WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI WAZIRI JOHN POMBE MAGHUFULI NAIBU JAMES WANYANJA
19. MALIASILI NA UTALII WAZIRI NI SHAMSA MWANGUGA NAIBU EZEKIEL MAIGE
20. WIZARA YA MAMBO YA NDANI DR. LAWRENCE MASHA NAIBU NI HAMISI KAGASHEKI
21. WIZARA YA MAMBO YA NJE USHIRKIANO WA KIMATAIFA WAZIRI NI BENARD MEMBE NAIBU SEIF ALI IDDI
22. WIZARA YA NISHATI NA MADINI WAZIRI WILLIAM NGELEJA NAIBU ADAM MALIMA
23. WIZARA YA SHERIA NA KATIBA MH. MATHIAS CHIKAWE
24. WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA DK. HUSSEIN MWINYI NA NAIBU EMMANUEL NCHIMBI
25. WIZARA YA AFRIKA MASHARIKI DK. DEODATUS KAMALA
26. WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA MASOKO DK. MARY NAGU NAIBU CYRIL CHAMI
Ukitaka kujua ni kwanini watu wanaquestion, angalia perfomance ya wizara ya ujenzi tangu magufuli aondoke, na baada ya muda mfupi uangalie tena wizara ya Ardhi itakavyokuwa, the qustion is, kama aliiweza ya ujenzi kwanini ahamishwe? Kama ya Ardhi ameiweza kwanini anahamishwa? What about Membe ina maana yeye ndiye ameiweza zaidi wizara ya mambo ya nje?