Bandari watumia bilioni 9.6 kikao cha siku moja

Bandari watumia bilioni 9.6 kikao cha siku moja

Mkubwa Noti 10 za buku 10 ni sawa na 1m kimahesabu,1km sawa ni 1000m that means 1km ni sawa na noti 10,000 za buku 10,kwa mahesabu ya haraka 100millions ni sawa na 1km,kutoka magogoni hadi atown ni 685km that means kucover zote hizo km tunahitaji 100m mara 685km ambazo ni sawa na 0.685billions hawa jamaa wamepiga 10b inamaana ukizitandaza kuanzia magogoni hadi city centre ya arusha unapata mistari 15 ya buku kumi kumi aiseee hawa jamaa wamepiga hela jamani.

Hesabu za Mulugo hizo!! Kama huko uliko na Wewe ni mwalimu Wa hesabu basi ni janga! Maana kama 1km inakuwa na 100m itakuwaje 685km ziwe na mistari 15 katika kumaliza 10bln? Hata MOROGORO hazifiki kwa mstari 1!
 
utasikia kamati inaundwa na watu watapiga tena pesa .Na hautosikia mkuu yoyote kufukuzwa na kufunguliwa mashtaka wala hautosikia pesa kurudishwa.Imepita hiyo sana sana utasikia waziri mkuu analalamika kama sisi
Money Stunna nafikiri huko nje kumekuharibu,nani kakuambia kuwa hao wakuu ndio waliochukua hizo fedha...wao wamepata 10% tu nyingine kwa wa wenye nchi yaani wananchi
 
Last edited by a moderator:
Ccm chukua chako mapema shikamoo mwakyembe ndo zamu yako imefikia Richmond ilikuwa El sasa Na wewe Fanya kama mwenzio tu ujiuzulu
 
Nasikia ìcho kikao kilifanyika international space station sio hapa duniani.
 
Hivi bilioni tarakimu zake zinaandikwaje tena?

1/=........................................shilingi moja
10/=.....................................shilingi kumi
100/=..................................shilingi mia moja
1,000................................shilingi elfu moja
10,000/=...........................shilingi elfu kumi
100,000/=........................shilingi laki moja
1,000,000/=....................shilingi milioni moja
10,000,000/=.................shilingi milioni kumi
100,000,000/=..............shilingi milioni mia moja
1,000,000,000/=..........shilingi bilioni moja
10,000,000,000/=....shilingi bilioni kumi

hiyo niliyo'bold ndo iliyotumika kwenye kikao kimoja, ukipanga msimbazi msimbazi kuanzia ikulu ya magogoni zinaweza kufika arusha.


Acheni utani basi jamani,hivi Tzs 10 bil mnaifahamu kweli????



$$$$$$ Tanzania kuna PESA ZA BUREEEE $$$$$$$$$

This is only ONE FINANCIAL YEAR, July 2013/14

 Mungu baba tshs  9,600,000,000 mkutano tu

 Mungu wangu tshs  9,400,000,000 matangazo

 Yesu wangu tshs  10,000,000,000 safari tu...


TUTABAKIA MASKINI HADI MWISHO WA DUNIA...

TANZANIA KUJITOA KTK UMASKINI NI NDOTO ZA
ALI NACHA, i feel so much pain...hii Tanzania hii,
Mungu pekee ataivusha ktk WIZI NA RUSHWA...

In Tz...WIZI NA RUSHWA KUBWAAA = EBOLAA


Assume kila mmoja analipwa laki 3 kama wajumbe wa BMK, hao wafanyakazi waliotajwa (180) ili wazimalize hizo 10 Bilions, inabidi wakae vikao kila siku (isipokuwa Jpili) kwa muda wa miezi saba sawa na siku 185. Wao wameifyeka hiyo hela kwa kikao cha siku moja bila huruma.

Naomba atakaye pata hesabu tofauti na ya kwangu anirekebishe tafadhali.
 
Naona kama nchi yetu inachezewa na viongozi wasio na uzalendo kwa nchi hii na kwa vile hakuna hatua madhubuti inayochukuliwa ndio maana kila kukicha fulani katafuna mamilioni ya fedha mara fulani kauza nyumba ya serikali.
Nadhani kuna haja ya kuangalia sheria zetu hasa kwa watu wanaotafuna fedha nyingi namna hii yaaniTshs Bilioni 9.6 /= kwa watu 180 maana yake kila mmoja alijipatia Tshs milioni 53.333 ambapo ni kiasi kikubwa sana kwa mwaka maana kuna watu wanapata pension NSSF ya shs milioni moja na nusu kwa utumishi wa miaka zaidi ya thelathini je huu ni utu kweli. Maana naona kama ni kiini macho ndo maana watumishi wengine hawapati mishahara ya kutosha/kuridhisha (< Tshs 350,000/= kwa mwezi) na mafao ya kutosha kumbe kuna mchwa wanaokula utajiri wa nchi hii.
Hatua zichukuliwe na tuache kelele zisizo na maana maana kuna baadhi ya wizara zimepata fedha kama bajeti kwa mwaka kama kichekesho sasa kumbe kuna idara inayotumia mamilioni ya fedha zaidi ya wizara moja katika nchi hii. Tuangalie vipaumbele vyetu na kisha tuwe macho na idara zinazozalisha ili kuzisimamia vizuri tuache kutembeza bakuli nje ya nchi kuomba misaada kumbe ndani ya nchi kuna fedha za kutosha isipokuwa usimamizi ndo unakosekana.
Idara kama TRA, BOT, TPA, TANAPA,NCCA,TANESCO,PPF,NSSF nk zisimamiwe vizuri ili kuleta ufanisi na kuboresha maisha wananchi wote.
 
Unajua serikali imeshagundua wizi wa mahela makubwa sanaaaa hauwashtui wa Tanzania wengi kwa sababu hawawezi relate na hicho kiasi.

Yani asilimia 80 ya wananchi wetu ambao ni wakulima, hayo maswala sijui EPA billion 200, kikako kimoja TPA siku 1 billion 10, wao hawawezi kushtuka kwasbabu hawajui nini nini hasa.
Hawawezi kutengeneza picha halisi.

Lakini kwa mfano uwaambie kua jamaa kaiba million 2 za kijiji hivi, mweh lazima ashtuke na haki aitafute. Lakini ma billion kwake ni kama currency ingine. Kwanza anahisi sio zake na pili haelewi zikoje hivyo ni ngumu kushikwa na uchungu!

Mimi ndio maana nafikiri hata uvumbuke ufisadi wa kiwango gani hautaweza kuwashtua wakulima na wajinga wengi ambao ndio mtaji mkubwa wa ccm!



Mkuu nakupigia salute sana.
Hasa pale..... kwanza anahisi sio zake...........

Ni kazi nzito, kubwa sana kumwaminisha mtanzania wa kawaida kwamba fedha inayochotwa bank kuu au taasisi yoyote ya serikali kwamba ni zake/zinamhusu.

Hali ni hivyo kwenye chaguzi mbalimbali. Kura huwa ni "kumsaidia mtu apate uongozi" na sio "kumtuma mtu awakilishe"
Ndiyo maana ni watz wachache sana wanaohangaika na kile kilichofanywa/simamiwa na kiongozi husika.
Ndio maana ukienda kijijini hujapendeza, hujanyoa ndevu vizuri, hujavaa suti, huna sura nzuri, huna kitambi, gari nzuri hata kama wewe ni mwadilifu na mchapakazi hodari na mwenye record nzuri, hutaweza kumshinda fisadi mbobezi, nyang'au, kibaka mzoefu lakini mwwnye sifa zilizotajwa awali.

Ndio maana nasema wapinzani wangewekeza zaidi kwenye elimu, wananchi wajue wao ni kina nani kwenye nchi, watambue wao ndio mabosi, wamiliki wa nchi. Ndipo utaona watu wakiwa na uchungu na raslimali zao.
Mfano, kashfa ya ujangili dhidi ya Kinana ilimwongezea sifa ya ujasiri sehemu fulani(siitaji). Kwamba ni shupavu, mwenye uwezo wa kupambana na tembo. Nilipoanza porojo za umuhimu wa tembo kuishi, faida zake(utalii-mapato) somo halikueleweka. Badala yake maswali yaliibuka mengi, yasiyojibika. Mfano mtu anakuuliza; hivi unaweza kutoa hela yako kutazama tembo? Wazungu ni wajinga kiasi hicho? n.k
Elimu, elimu, elimu.
 
Kipindi cha mwisho mwisho kila mtu anabana pesa kwa nafasi yake,mida ya majeruhi hii.ndo maana JK kaamua kuingia front kuwa afisa manunuzi
 
1/=........................................shilingi moja
10/=.....................................shilingi kumi
100/=..................................shilingi mia moja
1,000................................shilingi elfu moja
10,000/=...........................shilingi elfu kumi
100,000/=........................shilingi laki moja
1,000,000/=....................shilingi milioni moja
10,000,000/=.................shilingi milioni kumi
100,000,000/=..............shilingi milioni mia moja
1,000,000,000/=..........shilingi bilioni moja
10,000,000,000/=....shilingi bilioni kumi

hiyo niliyo'bold ndo iliyotumika kwenye kikao kimoja, ukipanga msimbazi msimbazi kuanzia ikulu ya magogoni zinaweza kufika arusha.

Mmmhh....mh. zumbemkuu hapa ndo umetuwezesha,
 
Hakuna nchi katika Afrika iliyokuwa na amani na utengamano wa kiuchumi kama Ivory Coast, tatizo kiongozi wa kwanza alijiangalia yeye na kujiona kama mungu mtu.
Leo hii hapa Tanzania zaidi ya 70% ya watu (wenye umri wa kupiga kura au kuandamana) wanajua ni nani wanafaidika na rasilimali za nchi. Subira yao (yetu) imekuwa kuwa labda siku moja nami nitaingia kwenye huo mtandao, lakini kwa miaka kama mitano sasa matumaini yanapungua na wengi wao wanaamini kuwa walio kwenye system ndio wataendelea kufaidi tu na mfano ni kama kilichotokea kwenye ajira za immigration, uteuzi wa nafasi utumishi wa umma, ugawanaji wa tenda za kazi nk.
Hiki ni kiasi kikubwa cha pesa kuliwa na watu wachache kiasi hiki na kwa muda mfupi hivi. Pia tukumbuke hizi ni audited reports hivyo pesa zinazoibiwa bila hata kujulikana zinaweza kuwa nyingi kuzidi hizi. Kubaliana na Rais Kagame alivyosema kuwa bandari pekee inaweza kuiendesha Tanzania wakati huo huo Pinda akiwa EU na JK akiwa China na mabakuli yao!
Kwa maana hiyo, hayatatokea ya Burkinafaso, hayatatokea ya Misri, Hayatatokea ya Rwanda nk lakini kuna kitu kinaweza kutokea kwa kigezo cha pengo la masikini na matajiri walioiba pesa likikolezwa kwa mbali na tofauti za dini. Makabili sio taizo.

Sisi watz ni wapole, wavumilivu, watiifu kwa mamlaka yaliowekwa, wenye hofu ya Mungu, tunapenda umoja wetu, hata abdiko la bunge maalamu la katiba ni andiko la Mungu, hivyo tuseme ndiyo. atakayesema hapana haitakii mema muungano wetu tukufu. amen.
 
Kwa haraka tu watu wametumia fursa hiyo kuchomoa hela kwa ajili ya uchaguzi mwakani. Kuna mkuu wa IT dept, Phares Magesa anayejiandaa kwa nafasi ya Ubunge wa Kigamboni. Angalia dept yake ilichota kiadi gani katika 'mgao' huo.
Then taja wengine wenye interest hizo.
 
Ndivyo ilivyotokea na baadhi ya wakuu wa bandarini wameitwa dodoma kujieleza
Halafu wakishajieleza? Hawa Watusi mbona wanakosa akili ubadhilifu wa aina hii ilikuwa kuwasimamisha kasi kufunga account zao kuzuia hati za kusafiria wawekwe ndani ndipo mengineyo. Kuwaiti Dodoma si gharama nyingine tena?!! Hii nchi aendeshe mwendawazimu
 
Haya ya bandati na kipande tumeyaandika sana katika jamhuri. Wakaibuka watetezi wakasema tumetumwa. Tukaonekana jamnazo sasa afadhali wabunge wenyewe wamejionea. Nchi imekwisha ndugu zangu. Tuungane. Haya ni bandari, ya maliasili ni balaa zaidi. Kila mahali kumejaa wapigaji.
 
Wanajamvi,
Leo nimesoma kwenye magazeti kuwa mamlaka ya bandari imetafuna 9.6bilioni kwa kikao kimoja, nikakumbuka michango ya maabara tunaandamwa hadi tunakosa amani. Hizi si zigetosha ujenzi wa maabara shule za kata 1,000?
Kama ni kweli basi tutarajie maafa kama yale ya Burkina Faso.
Watu wameshalewa madaraka. Dr. Mwakyembe huwa nina imani kubwa sana na utendaji kazi yako kuliko hata Dr. J.P.Magufuli sasa huyo mkurugenzi mpya ulimpata kwa kupitia taratibu zote za ajira au ulishinikizwa na bosi wako?




Chanzo:
Habari Leo


Hizi pesa Lumumba wanafahamu zimekwenda wapi?
Hawana Pesa za Uchaguzi 2015 za kuwahonga wapigakura.

Fuatilia vijana wa Lumumba kuhusu thread hii utapata jibu.

Wajinga ndiyo waliwao-Wakati wa upigaji kura mijitu mengine inashabikia wezi hawa hawa bila hata aibu kisa wamepokea 5000ts= yaani kuwezeshwa kwenda choo ya siku moja mtu mzima anasahau miaka mitano ijayo.

 
Back
Top Bottom