Bandari watumia bilioni 9.6 kikao cha siku moja

Bandari watumia bilioni 9.6 kikao cha siku moja

Wanajamvi,
leo nimesoma kwenye magazeti kuwa mamlaka ya bandari imetafuna 9.6bilioni kwa kikao kimoja...nikakumbuka michango ya maabara tunandamwa hadi tunakosa amani. hizi zisi getosha ujenzi wa maabara shule za kata 1,000?
Kama ni kweli basi tutarajie maafa kama yale ya Burkina Faso.
watu wameshalewa madaraka. Dr. Mwakyembe huwa nina imankubwa sana na utendaji kazi yako kuliko hata Dr. J.P.Maguf... sasa huyo mkurugenzi mpya ulimpata kwa kupitia taratibu zote za ajira au ulishinikizwa na bosi wako?

Ndio tuchukue hatua sasa sio kila siku kulalamika.
 
Utashangaa majumba makubwa makubwa yanaporomoshwa Mungu wasaidie.Sasa basi maana inaanzia kwako tunaumwa magonjwa ya kutisha,ajali sisizokuwa na kichwa wala miguu,watoto wanavuta bangi au hawataki kusoma nk kiss maana ya Baba na mama zao kwani Mungu alisema "atawabatiliza Sana kizazi cha tatu mpaka cha nne cha wanichukiao..."
 
Wadau,hiyo ndio habari katika gazeti la Jambo leo na Habari Leo.

Viongozi wa bandari wameitwa Dodoma kwenda kujieleza kwenye kamati husika ya bunge.

Hivyo vilikuwa ni vichwa vya habari kama vilivyosomwa kwenye kipindi cha kutoka magazetini cha Channel 10, hivyo tafuta gazeti upate details zaidi.)

MY TAKE:
Hivi hii nchi ni masikini kweli?
 
Usiwe na wasiwasi; Rais wetu atawachukulia hatua kali wale wote waliohusika na ufujaji huo.

Rais gan unayemuongelea? Huyu Jk au? Km ni Jk nakupa pole xana!!! Hii nchi ni wassira, Riz1, Jk, Werema na wajanja wengne wa CCM!! Mungu atusaidie!! Ujinga wa wtz wengi ndo umetufkisha hapa
 

Halafu pesa za kujengea maabara,serikali haina.

Wakati huo huo wanafunzi wamekosa mikopo kisa budget finyu.

Tatizo hii nchi hatuheshimiani.
 
Hivi hawajatangaza nafasi za kazi hapo bandarini ,nikaombe kazi hapo hii ni neema
 
Ni watanzania wachache tu mnajua mambo kama haya yanatokea hii inasababishwa na watanzania wengi kutofatilia habari,kwa uchunguzi wangu mdogo niloufanya watu wa mikoa mengine hususani maeneo ya vijijini huwa habari kama hizi za mabilioni ya serekali kuchakuchuliwa huwa haziwafikii,Asilimia chache tu ya watanzania ndio mnaumizwa na vitendo hivi na msipofanya jitahada watz wengine wakajua nini kinaendelea kazi ya mabadiliko itakuwa ngumu,
Ili mabadiliko yatokee kuna haja ya kuhakikisha kili kaya tanzania ina kuwa na radio tena inasikiliza taarifa ya habari au habari za magazetini,
Kwa mwendo huo kila mtz atakuwa yupo na kiu ya kutaka kuona viongozi wasio waadilifu wakiwajibika.
Wasomi wetu zungukeni mikoani kufanya utafiti ili mjiridhishe kama wananchi hupata habari ambayo ni haki ya kila mmoja
Vyama vya siasa ombeni hata misaada ya radio ndogo mnapokuwa na wafadhili wenu au tumieni ruzuku kusaidia watu wa vijijini wanapata taarifa kama hizi.
 
Du aisee kuna watu kweli wanafaidi hii nchi.....Mwakyembe na Kipande wake watupe maelezo ya kina kuhusu hili jambo
 
Wana JF taarifa kutoka ndani ya mamlaka ya bandari wanasema ni mh Harison Mwakyembe aliyeomba hizo hela na kutoa maelekezo kuwa zionekane kama posho ya Vikao. Na inasemekana anataka kujitosa kwenye kinyang'anyiro cha Uraisi na ndio ameanza maandalizi. Bado kunaambazo zimechotwa TRL na zingine ATC mda si mrefu zitalipuka.

Mkuu mbona nimesikia ni billion wewe unasema ni million, vipi?

 
Mkuu ni billion 10, ni kweli kabisa mkuu, jana nilikuwa na yule jamaa wa civil society Foindation bwana John Ulanga, alikuwa moja wa wajumbe wa bodi ya TPA akaniambia ana ushaidi wa Mwakyembe kuchukua hizo fedha na jumatano ataweka mambo wazi
 
Back
Top Bottom