Bandari watumia bilioni 9.6 kikao cha siku moja

Bandari watumia bilioni 9.6 kikao cha siku moja

Mhh kuna profesa anaitwa msambichaka kiongoz mkubwa sana pale alikuwa principal cjui chuo gan
 
Nadhani walihudhuria watu 8, wakalipwa KABILIONI kamoja kamoja tu, vijisenti vingine wakalipwa sekretarieti. Nani kakuambia Tz ni masikini?

Haaa !!haya ni maajabu ya Dunia,Si jawahi hata kufikiria acha posho,kwamba kuna Mshahara wa kiasi hicho kwa mwezi,

Pole Nchi yangu.
 
Wadau,hiyo ndio habari katika gazeti la Jambo leo na Habari Leo.

Viongozi wa bandari wameitwa Dodoma kwenda kujieleza kwenye kamati husika ya bunge.

Hivyo vilikuwa ni vichwa vya habari kama vilivyosomwa kwenye kipindi cha kutoka magazetini cha Channel 10, hivyo tafuta gazeti upate details zaidi.)

MY TAKE:
Hivi hii nchi ni masikini kweli?

Inasikitisha sana mkuu.Hao wakuu wa bandari ndo wanaongoza kwa kuhonga wadada magari na kuwapangia nyumba mpaka mabinti wanne kwa mpigo kila mtu na nyumba yake kwa kweli pesa za vikao zinafanya kazi.
Hizo pesa bora zitumike kujenga maabara jamani kuliko kuwakata mishahara wafanyakazi.
 
Dr JK anaangushwa na watendaje wake
 
Ndio maana ukitaka kutoa mzigo wako bandarini wanakutoza makodi makubwa kuliko ata thamani ya mzigo lengo ni kujilimbikizia tu harafu bado raia mnachangishwa pesa za mahabara eti nchi haina pesa

Watu wanatoza kodi kwa kukomoana aisee yaani mpaka watu huwa wanawasusia mizigo yenyewe wanaamua kuiacha.
Halafu na sio harafu.
Maabara na sio mahabara.
 
Hadi tutakapokuja kushtuka nchi itakuwa imekwisha na hapo sasa ile amani tuiimbayo itatoweka kwa kugombania rasilimali chache zilizobaki

This is Tanzania
 
Jana Mr Pinda alikua anaongoza harambee ili zipatikane milion 500 kwa ajili ya madawati. Waliochanga nawashauri wakadai pesa zao na ambao waliweka ahadi wasichangie tena.
 
Mmmmh kweli kikulacho kinguoni kwako!!!

10,bn as sitting allowance for a single day meeting!!
 
Nilivyoisikia hii habari asubuhi nikadadisi haraka nikadhani labda ni TPA ya meneja aliyefukuzwa, Mgawe kushtuka haya yamefanyika chini ya meneja aliyewekwa na Dr. Mwakyembe kwa mbwembwe Eng. Kipande!
Na mara nikawaza haya yamefanyika chini ya Waziri gani ....Dr. Mwakyembe!!!
Kwa maani hii ni kuwa haya matumizi ni 'afadhali' ukilinganisha na uongozi uliopita maana wanasema hii timu imepangwa na watu makini!!
Hapa ndipo tukubaliane kimsingi kuwa kisheria ccm wanatutawala lakini wamepoteza uhalali (legitimacy)wa kutawala.
 
daah dadeki halafu eti wanataka kukata mishahara yetu kuchangia ujenzi wa maabara....?!!!.....Yani mtu akigusa mshahara wangu namloga.

Hivi mishahara inakatwa lazima!?Hapana huo ni uonevu mkubwa.mimi sikubali
 
Mh. Deo kuja DODOMA ni kufanya wajitengee tena fedha ZA nauli, POSHO za kujikimu, mawasiliano, machapisho, etc. Deal lingine Hilo tena TPA.
 
Back
Top Bottom