Bandari watumia bilioni 9.6 kikao cha siku moja

Bandari watumia bilioni 9.6 kikao cha siku moja

Entim

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2013
Posts
4,024
Reaction score
2,273
Wanajamvi,
Leo nimesoma kwenye magazeti kuwa mamlaka ya bandari imetafuna 9.6bilioni kwa kikao kimoja, nikakumbuka michango ya maabara tunaandamwa hadi tunakosa amani. Hizi si zigetosha ujenzi wa maabara shule za kata 1,000?
Kama ni kweli basi tutarajie maafa kama yale ya Burkina Faso.
Watu wameshalewa madaraka. Dr. Mwakyembe huwa nina imani kubwa sana na utendaji kazi yako kuliko hata Dr. J.P.Magufuli sasa huyo mkurugenzi mpya ulimpata kwa kupitia taratibu zote za ajira au ulishinikizwa na bosi wako?

deo-filikunjombe_300_172.jpg

​

OFISI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imemaliza kazi ya ukaguzi maalumu katika matumizi ya mabilioni ya shilingi katika Mamlaka ya Bandari (TPA). Akizungumza Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe alisema CAG amemaliza kazi yake na kukabidhi ripoti.

"Taarifa yenu ya mwaka jana ilikuwa na utata, ilionesha kulikuwa na matumizi ya fedha ya Sh bilioni 9.6 kwa ajili ya mkutano, Sh bilioni 9.4 kwa ajili ya matangazo na Sh bilioni 10 kwa ajili ya safari.

"Taarifa ya CAG tumeipata jana (juzi) hatujaisoma… natoa muda ili Kamati ipitie na pia na nyie muipitie vizuri," alisema Filikunjombe.

Akitetea hoja ya kuomba CAG akague hesabu hizo hivi karibuni, Filikunjombe alisema Kamati ya PAC ilipotembelea TPA, ilikuta kwa mwaka mmoja mamlaka hiyo imetumia Sh bilioni tisa kwa ajili ya mkutano mkuu wa wafanyakazi.

"Tukawauliza hawa wajumbe wa mkutano mkuu wa wafanyakazi, kwanza mlifanyia wapi? Hapa hapa ndani (ya nchi)? Wako wangapi? Wako 180. Mmelipanaje mpaka inafika Sh bilioni tisa?" Alihoji.

Mbali na fedha hizo za mkutano wa wafanyakazi, Filikunjombe alisema pia walikutwa wametumia Sh bilioni tisa kwa matangazo.

"Tukauliza, haya matangazo mmetangaza wapi? Nje au ndani? Kwa sababu kama ni nje, labda. Kama ni ndani ya Tanzania matangazo ya Sh bilioni tisa, kila mmoja leo hii hata mtu ambaye yupo tumboni angeijua TPA," alisema.

Kutokana na hali hiyo na kutokuwepo kwa muda wa kujadili taarifa hiyo ya CAG, Filikunjombe aliagiza Menejimenti ya Mamlaka ya Bandari (TPA) kwenda Dodoma kujadili ripoti hiyo na kutoa utetezi wao.

Wakati huo huo, Kamati hiyo imeitaka Bodi ya Chuo Kikuu cha Mzumbe, kufanyike uchunguzi katika ujenzi wa jengo la chuo hicho lililogharimu Sh bilioni 1.8, kama lilifuata taratibu za manunuzi.

Filikunjombe alisema wamefurahishwa na taarifa ya hesabu za chuo hicho, kwa sababu ni nzuri na mapato yao yalionesha kukua na kuongeza.

Kwa mwaka 2011-2012 mapato ya chuo hicho ya ndani yalionesha kufikia Sh milioni 600 ambapo kwa mwaka 2012-2013, yalipanda na kufikia Sh milioni 800.

Hata hivyo mwenyekiti wa bodi ya chuo hicho, Daniel Mkude alisema kuwa Mzumbe inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa walimu, hali iliyowalazimu wakati mwingine kuajiri walimu wasio na viwango na kuingia gharama ya kuwasomesha.

Chanzo:
Habari Leo
 
Yani hii habari imenisikitisha sana hivi watanzania mtafanyiwa hivi hadi lini.Kikao cha siku moja bandarini kimetumia billion 10

Bado mnaambiwa nchi masikini msipochukua hatua mtabaki masikini milele yani imeniumiza sana.

Source magazeti yote ya leo kasoro ya udaku na michezo.
 
Na ndio maana nikikuta jitu linasema bora CCM kuliko upinzani kwani nchi itakuwa kama somalia huwa natamani hata nimpige bomu afe kabisa.........vita si silaha tu kwa jinsi utawala wa ccm ulivyo umeharibu system zote hadi kuanzia mlinzi wa getini paka viongozi wakubwa . Na hii wanafanya wakijua hakuna wa kuwa fanya lolote lile. Paka leo kweli hakuna hata history ya wezi wa pesa zetu aliyetiwa ndani kweli hii ni nchi yetu au ?? sisi ni wakimbizi hii nchi ni ya kina kikwete na watu wake ndio ambao wamepewa mkataba na mungu wa kuishi hapa na kuwafanya watanzania wengine kama misukule yaani tukishiba na kulala tunashukuru mungu. Natamani siku ifike na hao wanaojitia na mitutu yao tuone sasa...hatua 30 kulinda kula zetu. Hatuna silaha wala mitutu ila wao watushikie tu mitutu yao......
 
Mmh. Hii itakuwa kali. Kama kweli basi ngumu kumeza. Bahati mbaya hakuna hatua huchukuliwa.
 
Usiwe na wasiwasi; Rais wetu atawachukulia hatua kali wale wote waliohusika na ufujaji huo.
 
Ndio maana ukitaka kutoa mzigo wako bandarini wanakutoza makodi makubwa kuliko ata thamani ya mzigo lengo ni kujilimbikizia tu harafu bado raia mnachangishwa pesa za mahabara eti nchi haina pesa
 
Yani hii habari imenisikitisha sana hivi watanzania mtafanyiwa hivi hadi lini.Kikao cha siku moja bandarini kimetumia billion 10

Bado mnaambiwa nchi masikini msipochukua hatua mtabaki masikini milele yani imeniumiza sana.

Source magazeti yote ya leo kasoro ya udaku na michezo.

daah dadeki halafu eti wanataka kukata mishahara yetu kuchangia ujenzi wa maabara....?!!!.....Yani mtu akigusa mshahara wangu namloga.
 
Mbinguni mahesabu MPwa mema
yanchi Duniani we endelekusubiri wenzio wanatimiza maandiko
 
Mmh. Hii itakuwa kali. Kama kweli basi ngumu kumeza. Bahati mbaya hakuna hatua huchukuliwa.

utasikia kamati inaundwa na watu watapiga tena pesa .Na hautosikia mkuu yoyote kufukuzwa na kufunguliwa mashtaka wala hautosikia pesa kurudishwa.Imepita hiyo sana sana utasikia waziri mkuu analalamika kama sisi
 
  • Thanks
Reactions: Pai
Na ndio maana nikikuta jitu linasema bora CCM kuliko upinzani kwani nchi itakuwa kama somalia huwa natamani hata nimpige bomu afe kabisa.........vita si silaha tu kwa jinsi utawala wa ccm ulivyo umeharibu system zote hadi kuanzia mlinzi wa getini paka viongozi wakubwa . Na hii wanafanya wakijua hakuna wa kuwa fanya lolote lile. Paka leo kweli hakuna hata history ya wezi wa pesa zetu aliyetiwa ndani kweli hii ni nchi yetu au ?? sisi ni wakimbizi hii nchi ni ya kina kikwete na watu wake ndio ambao wamepewa mkataba na mungu wa kuishi hapa na kuwafanya watanzania wengine kama misukule yaani tukishiba na kulala tunashukuru mungu. Natamani siku ifike na hao wanaojitia na mitutu yao tuone sasa...hatua 30 kulinda kula zetu. Hatuna silaha wala mitutu ila wao watushikie tu mitutu yao......

Mkuu, mgusi mukulu, hii MIPANYA BOOK ya CCM inaudhi sana.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom