mrangi
JF-Expert Member
- Feb 19, 2014
- 96,186
- 137,586
Hakuna nchi katika Afrika iliyokuwa na amani na utengamano wa kiuchumi kama Ivory Coast, tatizo kiongozi wa kwanza alijiangalia yeye na kujiona kama mungu mtu.
Leo hii hapa Tanzania zaidi ya 70% ya watu (wenye umri wa kupiga kura au kuandamana) wanajua ni nani wanafaidika na rasilimali za nchi. Subira yao (yetu) imekuwa kuwa labda siku moja nami nitaingia kwenye huo mtandao, lakini kwa miaka kama mitano sasa matumaini yanapungua na wengi wao wanaamini kuwa walio kwenye system ndio wataendelea kufaidi tu na mfano ni kama kilichotokea kwenye ajira za immigration, uteuzi wa nafasi utumishi wa umma, ugawanaji wa tenda za kazi nk.
Hiki ni kiasi kikubwa cha pesa kuliwa na watu wachache kiasi hiki na kwa muda mfupi hivi. Pia tukumbuke hizi ni audited reports hivyo pesa zinazoibiwa bila hata kujulikana zinaweza kuwa nyingi kuzidi hizi. Kubaliana na Rais Kagame alivyosema kuwa bandari pekee inaweza kuiendesha Tanzania wakati huo huo Pinda akiwa EU na JK akiwa China na mabakuli yao!
Kwa maana hiyo, hayatatokea ya Burkinafaso, hayatatokea ya Misri, Hayatatokea ya Rwanda nk lakini kuna kitu kinaweza kutokea kwa kigezo cha pengo la masikini na matajiri walioiba pesa likikolezwa kwa mbali na tofauti za dini. Makabili sio taizo.
chief ulichosema ni kitu sahihi kabisa cha kuongeza hii hii serikali wao ndiyo watakuja leta machafuko...na wakumbuke nguvu ya umma ikiianza haizuiliki vyombo vyote vya usalama wanaingiaga mitini...
viongozi na serikali wazipende kuishi kwa mazoeaaa kuwaona ah watz wapenda amani waoga...nani kwambia syo kweli kbsa hakuna watu mafia kama watz....
serikali ya tz na viongozi wake wakaye chini watafakari wapi wanakosea wajirekebishe maana mbeleni huko hali haitokuwa shwari wasiyonacho watawapora wenye nacho kwa nguvu yaani ni vurugu itakuwa
binadamu anachoka badilika siku moja dakika moja sekunde moja hafai anakuwa siyo yule tena