Bandari watumia bilioni 9.6 kikao cha siku moja

Bandari watumia bilioni 9.6 kikao cha siku moja

utasikia kamati inaundwa na watu watapiga tena pesa .Na hautosikia mkuu yoyote kufukuzwa na kufunguliwa mashtaka wala hautosikia pesa kurudishwa.Imepita hiyo sana sana utasikia waziri mkuu analalamika kama sisi

hizo hela zinaingia kwenye chama kupitia mgongo wa kikao ni bahati mbaya sn walalahoi tumeinyaka issue hyo. Wajumbe watakuwa wamepewa posho ya kawaida tu.. Nakumbuka kwenye bunge la bajet walijaza mihela idra ya usalama wa Taifa wapinzan wakashtukia
 
Hicho kikao kilihudhuriwa na watu wangapi? Maana billion 10 ni nyingi 🙁
 
Du aisee kuna watu kweli wanafaidi hii nchi.....Mwakyembe na Kipande wake watupe maelezo ya kina kuhusu hili jambo

Hapo unaweza ukakuta ni order toka juu,yaani unaweza kuta wameambiwa kila idara wachangie pesa si unajua tunaelekea uchaguzi mkuu? hao jamaa wa bandari unaweza kuta wamepata kiasi kidogo tu zingine zikapelekwa panapostahili huwezi sikia hatua yoyote imechukuliwa dhid yao kwa sababu hayo ni maeneo ya kukusanyia pesa kwa ajili ya uchaguzi! na habari kama hizi tutaziskia nyingi tu kutoa idara mbalimbali!
 
Hicho kikao kilihudhuriwa na watu wangapi? Maana billion 10 ni nyingi 🙁

Nadhani walihudhuria watu 8, wakalipwa KABILIONI kamoja kamoja tu, vijisenti vingine wakalipwa sekretarieti. Nani kakuambia Tz ni masikini?
 
haaahaaaaaahaaaaaaaaaaa! mbona ba'riz yy karibia kila mwezi anatumia zaid ya mill.600tsh, kwa ajili ya kwenda kutanua nje, achen na sisi tufaid nahakuna ata kiongozi wa ccm wa kutuhoji maana wote ni dizain yetu :A S wink:
 
Hongereni wazee wa bandari meli hiyoooooooo! Semina elekezi ni muhimu sana endeleeni na warsha,mafunzo,vikao,semina 10b kwa siku ni ndogo sana inabidi muwe mnatumia trillioni moja kwa siku.
 
Unajua serikali imeshagundua wizi wa mahela makubwa sanaaaa hauwashtui wa Tanzania wengi kwa sababu hawawezi relate na hicho kiasi.

Yani asilimia 80 ya wananchi wetu ambao ni wakulima, hayo maswala sijui EPA billion 200, kikako kimoja TPA siku 1 billion 10, wao hawawezi kushtuka kwasbabu hawajui nini nini hasa.
Hawawezi kutengeneza picha halisi.

Lakini kwa mfano uwaambie kua jamaa kaiba million 2 za kijiji hivi, mweh lazima ashtuke na haki aitafute. Lakini ma billion kwake ni kama currency ingine. Kwanza anahisi sio zake na pili haelewi zikoje hivyo ni ngumu kushikwa na uchungu!

Mimi ndio maana nafikiri hata uvumbuke ufisadi wa kiwango gani hautaweza kuwashtua wakulima na wajinga wengi ambao ndio mtaji mkubwa wa ccm!
 
siku moja 10b?
hicho kikao kwanza walikuwa wangapi?
kama kwenye kikao walikuwa elfu moja kila mtu karamba milioni kumi ya kikao siku moja, dah! bongo raha
 
Wanajamvi,
leo nimesoma kwenye magazeti kuwa mamlaka ya bandari imetafuna 9.6bilioni kwa kikao kimoja...nikakumbuka michango ya maabara tunandamwa hadi tunakosa amani. hizi zisi getosha ujenzi wa maabara shule za kata 1,000?
Kama ni kweli basi tutarajie maafa kama yale ya Burkina Faso.
watu wameshalewa madaraka. Dr. Mwakyembe huwa nina imankubwa sana na utendaji kazi yako kuliko hata Dr. J.P.Maguf... sasa huyo mkurugenzi mpya ulimpata kwa kupitia taratibu zote za ajira au ulishinikizwa na bosi wako?

Nina wasiwasi kuwa hii imekosewa labda ilibidi iwe 9.6milioni na sio 9.6bilioni
 
Acheni wale jamani. Huwa nikisikia jambo kama hilo nafurahi sana,tena sana. Nawaomba bandari waitishe kikao kingine wale hata 50b.

Nafurahi kwa sababu majinga yanakufa kwa umasikini wajanja twala nchi. Watu wenyewe wametaka wawe masikini utawalazimisha utajiri?.

Siku nikisikia hata waziri ameondoka na bajeti yote kwenda marekani ntafurahi sana.
 
Hivi bilioni tarakimu zake zinaandikwaje tena?
1/=........................................shilingi moja
10/=.....................................shilingi kumi
100/=..................................shilingi mia moja
1,000................................shilingi elfu moja
10,000/=...........................shilingi elfu kumi
100,000/=........................shilingi laki moja
1,000,000/=....................shilingi milioni moja
10,000,000/=.................shilingi milioni kumi
100,000,000/=..............shilingi milioni mia moja
1,000,000,000/=..........shilingi bilioni moja
10,000,000,000/=....shilingi bilioni kumi

hiyo niliyo'bold ndo iliyotumika kwenye kikao kimoja, ukipanga msimbazi msimbazi kuanzia ikulu ya magogoni zinaweza kufika arusha.
 
Walim wa shule moja jijin dar es salaam,waligawana shilingi 600/= kila mmoja kama posho ya kikao,ambapo me binafsi nilichukua 500/= kwa kukosekana kwa chenji
 
  • Thanks
Reactions: Pai
Kama ni kweli safari hii watazitema asee.

thubutu!! waziteme kwa wewe kukaa kwenye keyboard tu? chukua hatua kwa nafasi yako ukitegemea kundi flani lipiganie haki yako hutakaa uipate milele pambana mwenyewe!
nchi ngumu hii sijapata kuona
 
Back
Top Bottom